Advertise with Us

Advertise with Us

DHall

DHall

Pages

June 11, 2013

Breaking News: Wilfred Lwakatare aachiwa huru kwa Dhamana!


Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Wilfred Lwakatare

Jitihada za mawakili wa Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Ndg. Wilfred Lwakatare kumtoa kutoka mahabusu zimezaa matunda mchana huu baada ya Hakimu anayesikiliza kesi ya hiyo kumaliza kupitia jalada la kesi hiyo ambayo Lwakatare anatuhumiwa kwa kosa la kujaribu kumwekea sumu mhariri wa gazeti la Mwananchi Ndg. Denis Msaki. Hakimu anayesikiliza kesi hiyo Aloyce Katemana alisema masharti ya dhamana hiyo ni wadhamini wawili wafanyakazi kila mmoja aweke bondi ya shilingi milioni 10 na wawe na uthibitisho wa barua na mihuri ya ofisi wanayofanyia kazi. Hakimu katamana alitoa muda mpaka saa nane kwa wahusika kutimizwa kwa masharti hayo jambo ambalo lilifanyika na hatimaye Lwakatare kuachiwa huru.

Hii ni habari njema kwa sana kwa Uongozi, Wanachama, Wapenzi, na Mashabiki wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA)

No comments:

Post a Comment