Advertise with Us

Advertise with Us

DHall

DHall

Pages

July 19, 2012

AJALI ZA MAJINI: SERIKALI BADO TU KUJIFUNZA..??..

1. MV. BUKOBA 21/05/1996
 
 Mv. Bukoba ambayo ilizama mnamo mwaka 1996 katika ziwa victoria na kuua watu zaidi ya 1000.


2. MV SPICE ISLANDER 10/09/2011

MV Spice Islander iliyozama katika bahari ya hindi huko Nungwi wakati ikiwa njiani kutokea Dar es Salaam kuelekea Pemba mnamo mwaka jana 2011 na kuua watu zaidi ya 250.


3. MV. SEAGULL 18/07/2012

Mv. SeaGull ambayo imezama leo mchana katika bahari ya hindi na kuua watu zaidi ya 200.

ILIANZA AJALI YA MELI YA MV. BUKOBA, IKAFUATIA MELI YA MV. SPICE ISLANDER, LEO MELI YA MV. SEAGULL. HIZI NI BAADHI YA AJALI ZILIZOWEZA KUBAHATIKA KUSIKIKA NA KUTANGAZWA NA VYOMBO VYA HABARI!

JE SERIKALI NA JESHI LA UOKOAJI WA MAJINI BADO TU KUJIFUNZA NA KUTAMBUA WAJIBU WAKE KABLA YA MADHARA AU MPAKA MAAFA YATUKIE..??..
 
USHAURI WA BURE: Ni wazi kwamba kuna haja na umuhimu mkubwa sana kwa Serikali kutupia jicho na kuwekeza katika sekta hii ya majini haswa kwa upande wa vyombo vya kisasa vya mawasiliano na vile vya uokoaji kwani ajali zimekuwa ni nyingi na zenye kuhitaji vyombo vya kisasa vya uokoaji ukilinganisha na vyombo duni vinavyotumiwa na Jeshi la uokoaji wa majini.

No comments:

Post a Comment