Advertise with Us

Advertise with Us

DHall

DHall

Pages

October 13, 2012

-}i{- BREAKING NEWS! RPC wa Mwanza SACP Liberatus Barlow auawa na wanaodaiwa kuwa ni majambazi!


 Aliyekuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza Kamishna Mwandamizi wa Polisi (SACP) Liberatus Barlow enzi za uhai wake.

Habari zilizoifikia Maisha Times Blog Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza Kamishna Mwandamizi wa Polisi (SACP) Liberatus Barlow ameuawa usiku wa kuamkia leo katika tukio linalohusishwa na ujambazi.

Taarifa kutoka Mwanza ambazo zimethibitishwa na Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini zinasema kuwa Kamanda Barlow aliuawa baada ya kumrudisha dada yake kutoka katika kikao cha harusi ya ndugu yao huko Kitangili. Hata hivyo, taarifa hizo bado hazijaweza kuchunguzwa na vyombo vya habari.

Kufuatia mauaji ya Kamanda wa Polisi mkoa wa Mwanza, ACP, Liberatus Barlow, Inspekta Jenerali wa Polisi, Said A. Mwema ametoa taarifa rasmi kuhusu tukio hilo kama ifuatavyo:

1. Ndugu wananchi. Napenda kutumia fursa hii kuwapa taarifa kuhusu tukio la mauaji ya aliyekuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza Kamishina Msaidizi wa Polisi Liberatus Barlow yaliyofanywa na watu wanaosadikiwa kuwa ni majambazi usiku wa kuamkia leo tarehe 13/10/2012 majira ya saa saba usiku Mkoani Mwanza.

2. Tukio hilo limetokea wakati kamanda huyo akitokea kwenye kikao cha harusi ya ndugu yake eneo la Frolida hotel Mwanza mjini, akiwa na ndugu yake waliyeongozana nae kutoka kwenye kikao hicho. Wakati akimshusha huyo ndugu yake eneo la Kitangiri Minazi Mitatu, walitokea watu wanaosadikika kuwa ni majambazi, na kumvamia na kuanza kumshambulia kwa risasi na kumuua papohapo.

3. Ndugu wananchi, kufuatia tukio hilo, tayari nimemtuma Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai DCI Robert Manumba kwenda mkoani Mwanza kwa lengo la kuimarisha ulinzi na upepelezi wa tukio hilo.

4. Najua tukio hili limetushitua na kutuhuzunisha wote. Hivyo, wakati tukiendelea na taratibu zingine kuhusiana na tukio hilo, niwaombe wananchi wote kuwa watulivu na kutoa ushirikiano kwa Jeshi la Polisi, utakaowezesha kuwabaini wahalifu hao.

No comments:

Post a Comment