Advertise with Us

Advertise with Us

DHall

DHall

Pages

May 28, 2013

A True Love Story!


Mimi na girlfriend wangu tulikuwa tunapendana sana, tulikuwa tumeishakuwa pamoja kwa muda wa takriban miaka minne hivi, na hivyo tukawa tumeamua kuoana. Kulikuwa na jambo moja dogo tulililokuwa likinisumbua sana; mdogo wake wa kike ambae alikuwa mzuri sana. Huyo binti (shemeji yangu) alikuwa na umri wa miaka ishirini na moja hivi (21), muda wote alipendelea kuvaa sketi fupi sana
na fulana nyepesi au blauzi zinazoonesha mwili wake na jinsi kifua chake kilivyo, alikuwa hahitaji kuvaa sidiria. Pamoja na binti huyu kuwa mwembamba kiasi, alikuwa na umbo la ajabu. Kiuno chake kiliumbwa mithiri ya "nyingu weusi" Tatizo ni kwamba mara nyingi binti alipokuwa akiniona alikuwa na tabia ya kujipitisha pitisha na kuinama mbele
yangu ili kunionesha mtaji wake. Kusema kweli nilikuwa navutiwa sana na uzuri wake. Na pia nilijua alikuwa ananifanyia makusudi maana alikuwa hafanyi hivyo kukiwa na watu wengine...bila shaka alikuwa ananitaka. Siku moja binti huyo alinipigia simu niende nyumbani kwake nikaangalie kadi za mialiko ya arusi alizokuwa amechapisha.
Nilipofika (wakati naingia ndani) akaninong'oneza kuwa ananitamani sana na kamwe hawezi kujizuia. Akaendelea kunieleza kuwa anahitaji tufanye mapenzi kabla sijafunga ndoa nadada yake ili nisijisikie vibaya kwamba natoka nje ya ndoa nilipigwa na bumbuwazi na hasa kutokana na nguo za nusu uchi alizokuwa amezivaa. Kabla sijamwambia lolote akaniwahi "Mie natangulia juu (ghorofani) kwenye chumba changu, kama unahitaji nikupe kitu kitamu njoo haraka kabla mashetani yangu hayajapoa. "akageuka na kukimbilia chumbani kwake Haraka nikageuka na kuelekea mlango mkubwa wa kutoka nje. Nikafungua na kutoka kuelekea kwenye gari yangu. Loh! kwa mshangao mkubwa nikaona pale nje familia yote imekusanyika na waliponiona nikitoka wakanipigia makofi na vigelegele kwa furaha. Huku machozi yakimtoka kwa furaha mchumba wangu, mama mkwe na baba mkwe akaniambia"Tume furahi sana kwamba umeshinda mtihani mdogo wa uaminifu ulioandaliwa na familia". Lakini niseme tu ukweli kwamba kutoka kwangu nje si kwamba nilikuwa naondoka bali nilikuwa nafuata Condom kwenye gari ili nirudi ndani kula vitu vitamu vya mdogo wake na mchumba wangu!

By Salvatory Mkami

2 comments:

  1. Anonymous2:19 PM

    mtihani gani huo mfyuu wizi mtupu

    ReplyDelete
  2. Anonymous7:35 PM

    Mtihani huo kiboko

    ReplyDelete