Advertise with Us

Advertise with Us

DHall

DHall

Pages

October 20, 2012

-}i{- Shyrose Bhanji na Sophia Simba almanusura wazichape kwenye mkutano mkuu wa "UWT"!



Wajumbe wa mkutano mkuu wa UWT, wakiwasili mjini Dodoma tayari kwa uchaguzi unaofanyika Jumamosi Oktoba 20, 2012.

 Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wanawake ya CCM, (UWT), ambaye anamaliza muda wake, Sophia Simba, akiingia ukumbi wa Mipango tayari kwa uchaguzi mkuu wa Jumuiya hiyo mjini Dodoma, Jumamosi Oktoba 20, 2012


Makamu wa Rais, Dkt. Ali Mohammed Shein, (Kulia),  Makamu wa Mwenyekiti wa CCM, (Bara), Pius Mekwa, (Kushoto), na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wanawake, UWT, Sophia Simba, mwanzoni mwa kikao cha uchaguzi cha Jumuiya hiyo, mjini Dodoma, Jumamosi Oktoba 20, 2012.

 Shy-Rose Bhanji, (Kulia), akionyesha uso wa hasira huku akitulizwa na mjumbe mwenzake, kufuatia tafrani kati yake na mwenyekiti wa Jumuiya ya Wanawake Tanzania UWT), Sophia Simba

Mbunge wa bunge la Afrika Mashariki, Shy-Rose Bhanji, (Aliyekaa), akitulizwa hasira na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Uwkezaji na Uwezeshaji, Dkt. Mary Nagu, wakati wa kikao cha uchaguzi mkuu wa Jumuiya ya Wanawake ya CCM, UWT, kwenye ukumbi wa chuo cha Mipango Dodoma Jumamosi Oktoba 20, 2012.

CHANZO ni swali ambalo Syrose alimuuliza Simba. "Wewe ukiwa mwenyekiti wa UWT kwa kipindi cha miaka minne iliyopita hatujawahi kukuona ukisimama jukwaani kutetea Chama."

Kimsingi swali hili lilikuwa ni swali makini, lililoulizwa wakati muafaka na kwa mtu sahihi kabisa anayetaka kupewa tena fursa ya uongozi.

Badala ya kujibu swali la Shyrose, Sophia Simba akajiuliza swali lake mwenyewe na kuja na majibu haya “Inaonekana aliyeuliza swali hajakomaa katika siasa za nchi, ndio maana ameambulia kuzomewa na wajumbe wa mkutano huu. Habwatuki bungeni au majukwaani kwa vile yeye ni serikali, na hata mbunge wa CCM hapaswi kukikosoa chama chake. Mimi si mithili ya upinzania kukaa na kukiosoa chama napaswa kukitetea. Anayesema Sofia Simba hajafanya kitu anajidanganya kwani wapiga kura wako kwenye matawi, kata, wilaya na mikoa, hao ndio wapiga kura wa chama na mimi kama mwenyekiti wa UWT nilijiimarisha katika ngazi za chini.”
 

Sophia Simba ambaye ni Waziri wa Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto, anakabiliwa na upinzani mkali kutoka kwa mbunge wa Same Mashariki, Anne Kilango Malecela.

No comments:

Post a Comment