Advertise with Us

Advertise with Us

DHall

DHall

Pages

November 21, 2012

Dk. Slaa: Safu Mpya ya CCM imejaa Taswira ya Ufisadi!

Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo [CHADEMA]
Dk. Willibrod Slaa

 Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo [CHADEMA], Dk. Willibrod Slaa, ameichambua safu mpya ya uongozi wa Chama cha Mapinduzi [CCM] iliyoundwa hivi karibuni mjini Dodoma, akisema wana taswira ya ufisadi.

Amesema kuwa hali hiyo inatokana na baadhi yao kuhusika kwenye matukio kadhaa ya kifisadi moja kwa moja.

Akizungumza kuhusu mtazamo wake kwa safu hiyo mpya ya uongozi wa CCM iliyoundwa na Mwenyekiti wake, Rais Jakaya Kikwete, katika mkutano mkuu uliomalizika juzi, Dk. Slaa alisema haoni jambo jipya.

“Nadhani hakuna jambo jipya, kipya ni kwamba wameteuliwa jana, lakini wote ni wazoefu wachafu,” alisema.

Katika safu hiyo, Kikwete anasaidiwa na makamu wawili, Philip Mangula wa bara na Dk. Ali Mohamed Shein wa visiwani na pia alimteua kada mkongwe, Abdullahman Kinana kuwa Katibu Mkuu mpya wa CCM. Wengine wanaounda Sekretarieti ni Zakhia Meghji, Mwigulu Nchemba, Asha-rose Migiro, Vuai Ali Vuai, Nape Nnauye na Mohamed Seif Khatib.

Akimchambua mmoja baada ya mwingine, Dk. Slaa alimtuhumu Mangula kuwa ni mmoja wa watu waliohusika na ufisadi wa fedha za Akaunti ya Malipo ya Nje(EPA) katika Benki Kuu ya Tanzania.

“Makamu Mwenyekiti Mangula anahusika na EPA, vimemo vingi vya kutaka fedha za EPA vimetokea kwake…sioni leo atajisafishaje kuleta tumaini jipya kwa Watanzania,” alisema.

Kuhusu Meghji, Dk. Slaa alisema huyo ndiye aliyeandika barua na kudanganya kuwa fedha hizo za EPA zimetoka kwa ajili ya Usalama wa Taifa.

“Sasa mtu kama huyo aliyedanganya, leo hii ukamweka kwenye fedha maana yake ni ku-‘recycle material’ ile ile,” alisema Dk. Slaa.

Akimchambua Katibu Mkuu, Kinana, alisema kigogo huyo ana mkono katika biashara chafu za makampuni ya meli na kwamba hajakanusha mpaka sasa.

Dk. Slaa alisema Kinana ambaye alikuwa meneja kampeni wa mgombea urais wa CCM mwaka 2010, katika chaguzi hizo CCM imeshutumiwa kwa kuiba kura, hivyo uteuzi wake ni kukubali kuzika demokrasia nchini.

Alisema timu hiyo imeundwa mahsusi kwa ajili ya kujiandaa kuiba kura mwaka 2015. Dk. Slaa aliongeza kuwa baada ya uchaguzi, CCM walitumia fedha nyingi kwa ajili ya kwenda kufanya utafiti wa kukijenga upya chama chao, ambao uliozaa kauli mbiu ya Kujivua Gamba’, kwamba pamoja na kazi ya kitaalamu wameshindwa kuvuana magamba.

Alifafanua kuwa hatua hiyo inatokana na ukweli kwamba walioitwa magamba sasa wamo kwenye safu mpya ya uongozi wa CCM. Katika kile kinachoonekana kuwa ni kumjibu Rais Kikwete hasa kutokana na kauli yake kuwa wapinzani wanafanya kazi ya kueneza uongo na kuwataka makada wa CCM kujibu mapigo, Dk. Slaa alimtaka aache kuwadanganya Watanzania.


Chanzo:
Tanzania Daima

No comments:

Post a Comment