Advertise with Us

Advertise with Us

DHall

DHall

Pages

February 19, 2013

Utabiri wa kutokea kwa "Vita" Tanzania katika siku za Usoni!




Natabiri "Civil War" kutokea Africa ndani ya miaka michache ijayo na kuiathiri zaidi nchi ya Tanzania ambayo ndiyo haswa inayogombewa na nchi tajiri kutokana na wingi wa rasilimali zake zenye utajiri mkubwa ambao kiuhalisia Serikali yetu imejiaminisha kwa 100% kwamba haiwezi kufaidi matunda ya rasilimali hizo hata kidogo pasipo wawekezaji ambao mara nyingi na kwa kiasi kikubwa tumejikuta tukiwanufaisha wao zaidi kuliko hata sisi wenyewe.

Kama ilivyokuwa enzi hizo wakoloni walipokuwa wanakuja Afrika kwaajili ya kutafuta rasilimali mbalimbali ndivyo hali ilivyo hata sasa na hakuna mabadiliko makubwa wala mbinu zenye utofauti kubwa wakoloni hao wanazozitumia bali ni zilezile kwa kuamini kwamba pasipo akili-elimu yao sambamba na vitendea kazi vyao kuendelea kwa nchi za kiafrika ni ndoto! jambo ambalo kutokana na upofu na udhaifu wa Serikali za nchi mbalimbali barani Afrika mf. Tanzania, Congo nk. limeonekana kuwa ni la kweli na hata kukubaliana nalo na kupelekea Viongozi wa nchi zetu sio tu kutafutwa bali wao wenyewe na heshima zao kuwatafuta na wenda kupiga goti kuwaomba Wakoloni hao walioficha sura zao nyuma ya kivuli cha wawekezaji "Investors" kutoka nchi tajiri kuja kujichukulia rasilimali zetu kwa bei sawa na bure huku sisi wenyewe tukipata faida ndogo isiyoelezeka sawa na bure [Pitia mikataba mbalimbali ya madini, Gesi, Mafuta-kati ya wawekezaji na Serikali ya Tanzania kama utabahatika kuupata kwani Mikataba hiyo hufichwa na kufanywa "Siri" kwasababu imejaa uozo mtupu].

Daima ili Nchi tajiri/Wawekezaji waweze kuiba Rasilimali kutoka katika nchi yoyote ya Afrika njia pekee ni kuvifadhili baadhi ya vyama vya Kisiasa au vikundi mbalimbali vya Kidini, Kikabila au Ukanda nk. kuhakikisha kwamba vinaanzisha harakati mbalimbali ambazo malengo makubwa na mwisho wake huwa ni vita jambo ambalo nchi tajiri kutumia nafasi hiyo ya Migogoro, Vita nk. kupenya na kuchukua kile wanachokitaka mf. Madini, Gesi nk. kadiri watakavyo kwa kuamini kwamba muda huo Serikali yaa nchi husika hatakuwa makini bali itakuwa imeelekeza zaidi nguvu kubwa katika vita dhidi ya vikundi ambavyo kinyume chake vinakuwa vimefadhiliwa na nchi hizo tajiri ili kuhakikisha kwamba vita haikomi mpaka pindi malengo ya nchi hizo tajiri yanapokuwa yametimia. [Congo ni moja ya nchi ambazo waasi wake wanafadhiliwa na nchi tajiri lakini ukichunguza kiundani utagundua kwamba nchi tajiri inachokitaka ni madini ya nchi hiyo na sio kitu kingine tofauti. Baada ya Congo hali hiyo [Vita] itafuata kwa nchi ya Tanzania]

Kinachoendelea Tanzania-Chokochoko za Udini, Ukabila, Ukanda Siasa chafu nk. ni sehemu ya juhudi za nchi za Magharibi kuvifadhili vikundi mbalimbali vya Kidini, Kikabila, Ukanda nk. ili kuhakikisha kwamba machafuko yanatukia kwa faida yao. Na kwakuwa Serikali yetu nayo imeshafungwa mdomo, miguu na mikono kwa kamaba iitwayo "misaada" inashindwa kuchukua hatua mathubuti za kukomesha hali hiyo kutokana na kubanwa na nchi tajiri-wafadhili na mashirika ya kimataifa ya misaada kufuata masharti yao hata kama yanalenga katika kupelekea matatizo na kuwaathiri wananchi jambo ambalo linaiwia Serikali ugumu kuwatetea wananchi wake kwa kule kuogopa kuwekewa vikwazo na nchi hizo tajiri sambamba na mashirika ya kimataifa. Nchi hizo tajiri na mashirika ya Kimataifa ambayo ukichunguza kwa umakini unagundua kwamba yako chini ya nchi hizo kupitia wawekezaji ambao nyuma ya pazia ndio yanayotumiwa na nchi hizo tajiri kuzinyonya nchi masikini kama Tanzania na ndio sababu mpaka sasa ukiachilia mbali kisingizio cha kodi ambayo bado nayo ni kidogo ukilinganisha na kile wawekezaji wanachokipata lakini kama ukiuliza wawekezaji katika sekta ya madini wameweza kuisaidia vipi jamii na nchi kwa ujumla bado hautaweza kupata majibu yanayoeleweka na hii ndio sababu ya kile kinachopiganiwa kule mtwara kuhusiana na bomba la gesi kwa wananchi kusahau kwamba Serikali haiko pale kwaajili ya kuwatetea wao bali wawekezaji ambao kiuhalisia wanalindwa na masharti ya misaada mbalimbali nchi inayoipata kutoka katika nchi hizo tajiri ambazo ndizo zinazozunguka kwa kivuli cha wawekezaji na kuja kutunyonya.
 

No comments:

Post a Comment