Advertise with Us

Advertise with Us

DHall

DHall

Pages

May 19, 2013

Jiulize- Pindi ukifariki Mrithi wa salio lako la "Tigo Pesa, M-Pesa, EzyPesa, & Airtel Money" anakuwa ni nani?!



Swali Muhimu kwa wateja/watumiaji wa mitandao ya simu nchini.

Huduma za utoaji na upokeaji wa fedha nchini kwa njia ya mitandao zinazotolewa na makampuni mbalimbali ya simu za mikononi nchini ikiwemo kampuni ya Tigo na huduma yake ya Tigo Pesa, Vodacom na Huduma yake ya M-Pesa, Zantel na huduma yake ya EzyPesa, Airtel na huduma yake ya Airtel Money zimekuwa ni huduma muhimu na za haraka katika maisha ya kila siku ya wananchi ambazo kwa ujumla zimeweza kurahisisha sana upokeaji na utumaji wa fedha nchini kuliko huduma nyinginezo za aina hiyo. lakini swali la msingi kutoka kwa Ndugu Salvatory Mkami ni: 

Pindi inapotokea mteja wa mtandao wa simu amefariki je mrithi wa salio la hela katika akaunti-line yake/zake za simu (Tigo Pesa, M-Pesa, EzyPesa, & Airtel Money) anakuwa ni nani ilihali Namba ya siri "Password" ni siri ya mmiliki wa simu hiyo ambaye kwa wakati huo anakuwa ni marehemu?!

Natumai makampuni ya Simu nchini Tanzania yatalipokea swali hili la msingi na kulifanyia kazi na baadaye kuja na majibu ambayo yatakuwa ni yenye faida kwa wateja na kampuni husika. 
 

No comments:

Post a Comment