Advertise with Us

Advertise with Us

DHall

DHall

Pages

June 4, 2013

Hii ndivyo hali ya Maandamano inavyoendelea huko nchini Uturuki!

Maandamano yameingia siku ya 50!
Waandamanaji wamejipanga kisawasawa, Wanatembea na Maduka ya bidhaa mbalimbali na huduma muhimu.
 
Maandamano ya wananchi dhidi ya serikali yaUturuki, yamechukua sura mpya na kuenea karibu katika maeneo yote ya nchi hiyo. Ilielezwa mwanzoni mwa kadhia hiyo kwamba, ukandamizaji mkubwa wa polisi dhidi ya waandamanaji, ndio uliopelekea kushtadi machafuko na maandamano hayo. Ukandamizaji wa polisi umekuwa wa kupindukia mpaka ambapo mbali na kukosolewa na mashirika mbalimbali ya haki za binaadamu kote duniani, pia umemlazimu Waziri Mkuu wa Uturuki Recep Tayyip Erdoğan kusema kuwa unafaa kufanyiwa uchunguzi. Pamoja na kwamba, polisi ya Uturuki imelazimika kupunguza makabiliano dhidi ya waandamanaji, lakini maandamano hayo yaliyoanzia mjini Istanbul, ambao ni kitivo cha uchumi wa nchi hiyo, taratibu yameenea hata katika miji mingine ukiwemo mji mkuu Ankara na miji mingine muhimu kama vile, Konya na Izmir.
Aidha maandamano hayo yamewafanya raia katika baadhi ya nchi za dunia kufanya maandamano yenye lengo la kuyaunga mkono maandamano ya wananchi wa Uturuki. Pamoja na hali hiyo, Recep Tayyip Erdoğan, amesisitizia azma yake ya kuendelea na mpango wake wa kuharibu bustani ya Gezi mjini Istanbul na kuweka mahala hapo kituo cha kibiashara. Kuhusiana na suala hilo wapinzani wanasema kuwa jambo lililowafanya kumiminika barabarani ni kiburi cha serikali ya Erdoğan cha kufumbia macho matakwa ya wananchi. Erdoğan ambaye kwa miaka kadhaa sasa anatambulika na vyama vya upinzani na fikra za waliowengi nchini Uturuki, kuwa mtu jeuri na dikteta, hivi sasa anakabiliwa na upinzani mkali wa wananchi. Upinzani huo unatajwa kuwa haujawahi kuonekana katika historia ya nchi hiyo. Hata katika migogoro ya kiuchumi iliyowahi kutokea nchini Uturuki katika muongo wa 90 Miladia, hakukushuhudiwa maandamano makubwa mithili ya yale yanayoshuhudiwa sasa nchini humo.
Ni kwa ajili hiyo ndio maana duru mbalimbali za kisiasa nchini Uturuki na ulimwenguni kwa ujumla zikajikita katika kuakisi radiamali na hasira za wananchi wa nchi hiyo. Baadhi ya duru hizo zinaamini kuwa, jamii ya Waturuki imekuwa ikikabiliwa na hali mbaya katika kipindi chote cha utawala wa chama cha 'Uadilifu na Maendeleo' kinachoongozwa na Recep Tayyip Erdoğan. Duru hizo zinaamini pia kwamba, katika kipindi cha utawala wa kijeshi nchini humo, Uturuki haikushuhudia hali mbaya kama ya sasa. Wakati huo huo, duru nyingine za kisiasa zinaamini kuwa, hasira za wananchi wa nchi hiyo, zimetokana na hatua ya kupuuzwa upinzani wao dhidi ya uingiliaji wa serikali ya Ankara katika mgogoro wa Syria.
Kwa upande wake Bülent esin, Mkuu wa chama cha Wafanyakazi nchini Uturuki amesema kama ninavyomnukuu: "Kile kinachojiri nchini Uturuki ni upinzani dhidi ya udikteta wa miaka 11 na siasa mbaya za chama cha Uadilifu na Maendeleo hususan kuhusiana na Syria." Mwisho wa kunukuu. Kwa mtazamo wa wapinzani, hatua ya serikali ya Ankara ya kuyaunga mkono makundi ya kigaidi nchini Syria na kufuata siasa za kuzusha mifarakano katika nchi hiyo na huko Iraq, ni sababu kuu iliyoibua vitendo vya kigaidi na mifarakano ya kikabila na kimadhehebu katika nchi hizo.

Kupata habari zaidi juu ya sababu zilizopelekea maandamano hayo makubwa ambayo hayajawahi kutokea nchini Uturuki bofya link hii http://www.guardian.co.uk/world/blog/2013/jun/04/turkey-protests-whats-happening-open-thread

No comments:

Post a Comment