Advertise with Us

Advertise with Us

DHall

DHall

Pages

June 1, 2014

Breaking News: Mama mzazi wa Zitto Kabwe afariki dunia!

Mwenyekiti wa Chama cha Walemavu Tanzania, (Chawata), Shida Salum ambaye pia ni ambaye ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema ambaye ni mama mzazi wa Mbunge wa Kigoma Kaskazini Mhe. Zitto Kabwe.
Mama mzazi wa mbunge wa Kigoma kaskazini Mh Zitto Kabwe ambaye alikuwa mwenyekiti wa Chama cha Walemavu Tanzania, (Chawata) na Mjumbe wa Bunge maalum la Katiba Bi Shida Salum amefariki dunia akiwa katika chumba cha wagonjwa wanaohitaji uangalizi maalumu (ICU) katika Hospitali ya Ami, Masaki, Dar es Salaam akisumbuliwa na maradhi ya saratani. 
Hii ni status ya Zitto Kabwe aliyoiandika dakika chache zilizopita katika ukurasa wake wa Facebook akisema "My mother has just passed away. Inna lillah wainna illaih raajiun"
Bi Shida ambaye mpaka kifo kinamkuta alikuwa ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema  alilazwa hospitalini hapo wiki kadhaa zilizopita. Alianza kusumbuliwa na maradhi hayo mapema Agosti mwaka jana lakini hali yake ilibadilika mapema mwaka huu akiwa mjini Dodoma akisubiri kuapishwa pamoja na wajumbe wengine wa Bunge Maalumu la Katiba.
Akizungumza hospitalini hapo tarehe21, Zitto alisema baada ya hali ya mama yake kuwa mbaya alishindwa kuendelea kukaa Dodoma kusubiri kuapishwa na alipelekwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), ambako aligundulika kuwa na saratani ya shingo ya kizazi na kupatiwa tiba kwa mwezi mmoja kabla ya kupelekwa India kwa matibabu zaidi.
Alisema kabla ya kupelekwa hospitalini hapo, alikuwa akiendelea kupata matibabu akiwa nyumbani, lakini hali yake ilibadilika tarehe 20 mei 2014.
Zitto alisema hali ya mama yake haikutengemaa tangu aanze kusumbuliwa na maradhi hayo. Alisema kutokana na maradhi hayo ya mama yake, ameshindwa kuhudhuria Bunge la Bajeti linaloendelea mjini Dodoma.
Tangu kuanza kwa Bunge la Bajeti, Zitto alionekana Dodoma mara moja tu, siku ilipowasilishwa Ripoti ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG).

No comments:

Post a Comment