Advertise with Us

Advertise with Us

DHall

DHall

Pages

November 12, 2014

Samson Mwigamba atimuliwa uongozi ACT-Tanzania, Prof.Kitila, Mchange wapewa karipio kali!

Katibu Mkuu wa ACT- Tanzania Samson Mwigamba (Katikati)

Katibu Mkuu wa ACT- Tanzania Samson Mwigamba amesimamishwa uongozi ndani ya chama hicho kwa tuhuma za ukiukwaji wa maadili,kuvunja katiba na ubadhirifu ndani ya chama hicho.

Taarifa kutoka kwa waasisi wa chama hicho ambao ni Greyson Nyakarungu na Leopold Mahona zinasema mbali na Mwigamba pia chama hicho kimetoa karipio kali kwa viongozi waandamizi wa chama hicho Professor Kitila Mkumbo na Habib Mchange kwa tuhuma mbalimbali.

Ikumbukwe Samson Mwigamba,Prof Kitila Mkumbo na Zitto Kabwe walitimuliwa uongozi ndani ya CHADEMA mapema mwaka huu kwa tuhuma kama hizi na kusababisha kukimbilia chama cha ACT Tanzania.

Chanzo:Mtanzania Jumatano

Habari zaidi

 Habib Mchange

Kitila Mkumbo

Zitto Kabwe

Waasisi wa ACT Tanzania Greyson Nyakarungu na Leopold Mahona waliwaambia waandishi wa habari jana kuwa waliwakaribisha Kitila Mkumbo na Samson Mwigamba ndani ya chama hicho kwa nia njema kumbe ni wasaliti na walaghai wakubwa.


Alisema kwanza kina Mwigamba wanajivika uasisi wa ACT huku wakijua si kweli. Pia kina Mwigamba wanatuhumiwa kwenda ofisi ya Msajili kubadili nembo ya chama kinyume cha utaratibu. Pia wanatuhumiwa kusajili katiba nyingine kinyume na Katiba waliyoandaa waasisi na kupatia chama usajili.

Nyakarungu amesema tayari Waasisi halali wa ACT wameshamwandikia barua msajili wa vyama kumuelezea juu ya uasi unaofanywa na Mwigamba na Kitila.

1 comment:

  1. Ogopa sana mtu huyu Habibu Mchange! Anaogopwa pia na Polisi ya nchi hii! Alishakwenda kwenye kituo kimoja cha TV hapa nchini na kudai yeye ndiye aliyetumwa na Chadema kuratibu mpango wa mauaji ya Daudi Mwangosi! Lakini polisi walimgwaya!

    ReplyDelete