Advertise with Us

Advertise with Us

DHall

DHall

Pages

March 23, 2012

CCM YAPANGA KUTUMIA RUSHWA YA KIMILA KAMA NJIA YA USHINDI UBUNGE JIMBO LA ARUMERU MASHARIKI!

Kwa habari za kiutafiti zilizoifikia Maisha Times hivi punde kutoka katika chanzo kimoja kilichoko Arumeru Mashariki zinasema kwamba timu maalumu ya kampeni za Chama Cha mapinduzi [CCM] iko katika "mpango mkakati" wa kugawa Rushwa ya hela katika dakika za mwisho za upigaji kura ili Wananchi waweze kukipigia kura na kumchagua Mgombea Ubunge kupitia chama hicho Siyoi Sumari anayeonekana wazi kubanwa vilivyo koo na Mgombea Ubunge kwa Tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo [CHADEMA] Joshua Nassari.

Kwa ufupi Mwananchi yeyote atakayepokea Rushwa hiyo utaapishwa kwa kulamba maziwa ili usikiuke makubaliano. Katika jamii ya wameru KULAMABA MAZIWA halafu ukaenda kinyume na makubaliano uliyoyafanya inaaminika kwamba ni LAANA.
Tayari mpaka dakika hii wameshaandaliwa wazee zaidi ya 200 kwaajili ya kuitekeleza kazi hiyo.

Maisha Times itazidi kuwapasha habari zaidi kutoka Arumeru kadiri habari zitakavyokuwa zikipatikana.

No comments:

Post a Comment