Advertise with Us

Advertise with Us

DHall

DHall

Pages

August 30, 2012

Vita ya Bashe, Dk Kigwangala yaibuka tena-Nzega

Kigwangala akanusha kukamatwa kwake, asema Bashe ndiye aliyekamatwa!

                        Dk Hamisi Kigwangala                                                     Hussein Bashe
 
MCHAKATO wa kuwania uongozi ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), umeshika kasi baada ya mahasimu wawili wilayani Nzega mkoani Tabora, Hussein Bashe na Dk Hamisi Kigwangala kujitokeza kwa nyakati tofauti kuwania nafasi ya Ujumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (Nec).
Mbali na mahasimu hao wawili, vigogo wengine waliojitokeza kuwania nafasi mbalimbali ndani ya chama hicho ni Mwenyekiti wa CCM mkoani Dodoma, William Kusila na Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki, Adam Kimbisa ambao wanataka kuwania uenyekiti wa mkoa huo.
Kigwangala ni Mbunge wa Nzega ambaye upinzani kati yake na Bashe, ulianza katika Uchaguzi Mkuu wa 2010, baada ya Bashe aliyeshika nafasi ya kwanza katika kura za maoni ndani ya CCM, kutopitishwa kwa madai kuwa hakuwa raia wa Tanzania.
Kigwangala ambaye alishika nafasi ya tatu katika kura za maoni, alipewa nafasi ya kugombea ubunge, badala ya Lucas Selelii ambaye alishika nafasi ya pili.
Akichukua fomu, Bashe alisema imani yake ni kuwa wanachama wa CCM watachagua kiongozi bora ambaye atakisaidia kufanikisha maendeleo na siyo wale ambao wanataka uongozi kama sehemu ya majaribio.
“Tunapochagua viongozi wa chama, hatuchagui mtu kwa majaribio. Kuna watu wanapita mitaani na kufanya kampeni ili wachaguliwe wao na ndugu zao ambao nao wanagombea. Chama siyo mali ya familia, naombeni sana msichague viongozi kwa misingi ya kifamilia,” alisema.

CHINI- Maneno ya Dk Kigwangala kutoka katika Ukurasa wake wa Facebook
"Sijakamatwa mimi wala Mke wangu mpenzi, na wala hatujahojiwa na TAKUKURU, na sijui ofisi ya TAKUKURU ikoje! Hizo ni fitna za magazeti yanayotumiwa na wanasiasa uchwara kwa kulipwa vimlungula kidogo. Nashukuru vyombo vya habari vimenipa umaarufu wa kisiasa kidogo, lakini huu wa kijinga namna hii siuhitaji! Aliyekamatwa akigawa Chai na Maandazi ni Hussein Bashe na hivi tunavyoongea mgombea na mpambe wake mkuu wa kike "

No comments:

Post a Comment