Advertise with Us

Advertise with Us

DHall

DHall

Pages

October 30, 2012

-§- Rushwa ya ngono katika "soko la ajira na kwenye elimu" Suluhisho ni lipi?



Kulingana na hali halisi ya kimaisha ilivyo kwa sasa labda kutokana na ugumu wa ajira nk. tabia ya baadhi ya waajiri katika mashirika na kampuni mbalimbali kuwatongoza au kuwadai rushwa ya ngono wale wanaokwenda kuomba kazi haswa haswa wanawake imekuwa inatishia hata baadhi ya watu [wanawake] kwenda kuomba kazi katika mashirika na makampuni mbalimbali kutokana na kuogopa kukumbana na dhahma za aina hiyo. Tukiachilia mbali maofisini pia vyuoni nako rushwa ya ngono imekuwa ni kama njia mojawapo inayotumiwa na wahadhiri [lectures] wa vyuo wasio waadilifu ili kupata wanachuo wa kike wanaokuwa labda wamewatamani au kuvutiwa nao kimwili na hivyo kutumia kigezo cha kuwabana/kuwafelisha kwa makusudi au kwa bahati mbaya katika mitihani yao na hatimaye kuweka makubaliano ya kuwabeba katika masomo au mitihani yao kulingana na somo husika. 

Kwa hakika rushwa ya ngono ni tatizo linaloendelea kukua na kushika kasi kubwa sana karibu katika kila nyanja ya ajira nchini kwani karibu kila mwanamke ambaye nimebahatika kuzungumza naye kuhusiana na maswala ya ajira amekuwa akilalamikia tabia hii, na papohapo bado kuna janga la gonjwa hatari wa ukimwi ambalo kiuhalisia halimtambui wala kumbagua mtu yeyote awaye.

Swali la msingi ni ni hili: Ni kwa vipi Serikali pamoja na wananchi tutaweza kukabiliana kulimaliza kabisa tatizo hili ambalo licha ya kuchangia Kudorora kwa kazi maofisini na kuongezeka kwa maambukizi ya gonjwa hatari la ukimwi lakini pia limekuwa likichangia kwa kiasi kikubwa kuvunjika kwa mahusiano-ndoa nyingi na mimba zisizotarajiwa?

No comments:

Post a Comment