Advertise with Us

Advertise with Us

DHall

DHall

Pages

November 5, 2012

-§-Justin Timberlake na Jessica Biel wafanyia "Honey Moon" yao Tanzania!


 Maharusi Justin Timberlake (31) na Jessica Biel (30) wakionekana walipokuwa wakishuka kwenye uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro International Airport (KIA) kwa ajili ya safari ya fungate lao la siku tano baada ya kufunga ndoa mjini Puglia, kusini mwa Italia October19.

  




 Picha iliyopigwa siku ya harusi ya Justin Timberlake na Jessica Biel.

Wanandoa hao waliofunga ndoa mbele ya ndugu na jamaa zaidi 100 kwenye hoteli ya Borgo Egnazia ya mjini Puglia, kusini mwa Italia October19 hivi karibuni walichukua ndege binafsi na kuingia nchini Tanzania kupitia uwanja wa ndege wa KIA na kuelekea katika reserve ya Singita Grumeti yenye hoteli ya kifahari ya Sakawa logde iliyopo katika mbuga ya wanyama ya Serengeti kwaajili ya fungate lao la siku tano (Honey Moon)

Hii ni mara ya pili kwa Msanii Justin Timberlake kuja nchini kiutalii baada ya kuja mara ya kwanza mwaka 2010 alipopanda Mlima Kilimanjaro kwa ajili ya kuchangisha fedha kwa ajili ya mpango wa maji safi duniani akiwa na Emile Hirsch, Isabel Lucas, Santigold, na Lupe Fiasco.
Wananchi wengi haswa wale walioko katika mitandao ya kijamii wameonekana wakitoa maoni na mchango wao wa mawazo huku wakiishauri serikali kutumia nafasi hizi kuitangaza Tanzania kimataifa.

No comments:

Post a Comment