Advertise with Us

Advertise with Us

DHall

DHall

Pages

June 21, 2013

Benki ya CRDB yazindua Huduma mpya ya "FahariHuduma"!


Mkurugenzi mtendaji wa Benki ya CRDB Dkt. Charles Kimei alipokuwa akielezea kwa ufupi Huduma itolewayo na Benki ya CRDB ijulikanayo kama "FahariHuduma"

Msanii wa muziki wa kizazi kipya Mataluma akiwa na wacheza shoo wake wakitoa burudani katika uzinduzi wa huduma za kibenki kupitia mawakala (FahariHuduma) kutoka Benki ya CRDB.

Afisa wa Benki ya CRDB anayehusika na huduma za uwakala wa Benki, Donat Mushi akielezea juu ya njia hiyo mpya ya utoaji huduma kupitia kwa mawakala iliyoasisiwa nchini jana na Benki ya CRDB. 

Jana Benki ya CRDB ilizindua kwa mara ya kwanza nchini njia mpya ya utoaji huduma za kibenki kupitia mawakala iliyopewa jina la FahariHuduma ikiwa na kauli mbiu ya Ulipo Tupo ambapo Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB hiyo Dkt. Charles Kimei alielezea sababu kubwa ya kuanzishwa kwa njia hiyo ni kwa lengo la kuwafikia watanzania wengi zaidi ambao bado hawajafikiwa na huduma za kibenki pamoja na kusogeza huduma karibu zaidi na wateja.
 

No comments:

Post a Comment