Advertise with Us

Advertise with Us

DHall

DHall

Pages

June 24, 2013

Mwanafunzi aliyedaiwa kupigwa risasi na kufa yu mzima na anaendelea vizuri na matibabu!



 Siku ya Tukio ilivyokuwa

Mwanafunzi wa chuo kikuu Chuo kikuu cha Dar es salaam (Alex Robert) anayedaiwa kuvamiwa na majambazi na kuporwa baadhi ya vitu zikiwemo Computer-Laptop3 kisha kupigwa risasi ya tumboni na majambazi na kufa wakati walipokuwa na wenzake wakijisomea kwa maandalizi ya mitihani ya mwisho ameibuka na kusema kwamba yeye hajafa na yu mzima akiendelea vizuri na matibabu ya jeraha la risasi katika Hospital ya Muhimbili. Akiongea na chanzo chetu Alex amesisitiza kwamba wale wote wanaoeneza habari kwamba amekufa ni wazushi na waongo hivyo na kuwataaka waache mara moja kumzushia jambo ambalo sio la kweli.

Inadaiwa kwamba tatizo kubwa ni kwa polisi wa chuo hicho (auxiliary) ambao hawakuonyesha ushirikiano katika kuwasaka majambazio hao ndani ya muda husika, habari zaidi zinasema matukio ya aina hiyo yamekuwa yakijitokeza mara kwa mara chuoni hapo pasipo polisi hao kutoa ushirikiano wa kutosha kwa wale wanaovamiwa.

No comments:

Post a Comment