Advertise with Us

Advertise with Us

DHall

DHall

Pages

June 21, 2013

News Update: Waliomshambulia Mhe. Machalli wakamatwa na Jeshi la Polisi Mkoani Dodoma!

Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma Kamishna Msaidizi Mwandamizi Bw. David Misime
Mbunge wa jimbo la Kasulu mjini kupitia Chama cha NCCR-MAGEUZI Mhe. Moses Machali
  Jeshi la Polisi Mkoani Dodoma linawashikilia watu wawili Jeremia Lawrent Mkude na Charles Chikumbili kwa tuhuma za kumvamia na kumshambulia Mbunge wa jimbo la Kasulu mjini kupitia Chama cha NCCR - MAGEUZI Mheshimiwa Moses Machali wakati akiwa njiani kuelekea nyumbani kwake. 
Hayo yamesemwa na kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Jeshi la Polisi Bw. David Misime ambaye alifafanua na kusema kwamba tukio hilo limetokea jana tarehe 20.06.2013 majira ya saa moja usiku katika eneo la Area 'E' Manispaa ya Dodoma na kwamba baada ya msako mkali uliofanyika mpaka usiku wa manane hatimaye baadhi ya watuhumiwa waliohusika na tukio hilo walikamatwa. 
Mheshimiwa Machali amelazwa katika hospitali ya Mkoa wa Dodoma akiendelea na matibabu.

No comments:

Post a Comment