Makazi ya Askari Polisi Msimbazi Kariakoo-Dar es salaam
Makazi ya Askari Polisi katika wilaya ya Rombo-Kilimanjaro
Baadhi ya skari polisi wameiomba Serikali kuangalia jinsi ya kuboresha nyumba
wanazoishi walinzi hao wa usalama wa raia kutokana na kile walichodai kuwa zimechakaa kupita kiasi na kwamba hali ya sasa haioneshi kuwa zinafaa
kukaliwa na binadamu.
Askari hao wanaoishi katika kambi mbalimbali haswa zile za jijini Dar es salaam waliieleza Maisha Times kwamba nyumba hizo kwa sasa kuta zake zimepasuka, vyoo na bafu zake ake zimebomoka na hivyo kutishia usalama wa afya zao na hata maisha yao kwa ujumla.
Wakizungumza na blog hii, baadhi ya askari ambao hawakutaka
kuandikwa majina yao walisema kwamba wameamua kuzungumzia hili katika vyombo vya habari kutokana
na hali halisi ya mazingira wanayoishi kambini humo, kitendo ambacho
wamekielezea kuwa kinawakosesha raha na moyo wa uwajibikaji inavyotakikana.
Waliendelea na kuongeza kuwa, kutokana na uchakavu wa nyumba hizo zilizojengwa karibu
miaka 70 iliyopita, enzi za ukoloni, kuna kila sababu ya msingi ya kuzifanyia
ukarabati mkubwa, au kuzibomoa kabisa na kujenga nyingine mpya ambazo zitaweza kukidhi mahitaji yao.
“Kama ulivyoshuhudia tu mwenyewe mwandishi wa habari, sisi ndo tunaishi katika mazingira haya, inasikitisha sana,” alisema mmoja wa askari hao aliyeongeza kuwa, kutokana na hali hiyo, baadhi ya askari wanalazimika kupanga uraiani ili kuepukana na adha ya mazingira ya sasa na pia udogo wa nyumba hizo jambo ambalo linachangia ugumu zaidi wa maisha ukilinganisha na vipato vyao.
*Kwa muda mrefu sasa makazi duni ya askari yamekuwa ni moja ya changamoto kubwa zinazolikabili Jeshi hilo muhimu kwa
usalama wa raia na mali zao.
No comments:
Post a Comment