Advertise with Us

Advertise with Us

DHall

DHall

Pages

Showing posts with label Politics. Show all posts
Showing posts with label Politics. Show all posts

August 30, 2015

HOTUBA YA MGOMBEA URAIS KUPITIA CHADEMA MHE. EDWARD LOWASA!

HOTUBA YA MGOMBEA URAIS KUPITIA CHAMA CHA CHADEMA NA UKAWA MH. EDWARD NGOYAI LOWASSA
 YA KUZINDUA ILANI NA KAMPENI YA UCHAGUZI MKUU
Jangwani-Dar-es-Salaam, 29 AGOSTI 2015


Ndugu Wana Dar es salaam na Watanzania wenzangu
 1. Leo ni siku ya kihistoria. Baada ya miaka ishirini na tano tangu mfumo wa vyama vingi urejeshwe, vyama vya upinzani wa CHADEMA, CUF, NCCR na NLD umeungana chini ya Umoja wa Katiba ya Wananchi kupigania uchaguzi mkuu wa mwaka huu na kuwa na mgombea mmoja katika ngazi zote.
 2. Miaka zaidi ya hamsini ya utawala wa serikali za CCM na waasisi wake, umekuwa utawala wa wachache walio hodhi madaraka na mali za nchi.
 3. Leo tunaanza safari ya uhakika ya kuleta mabadiliko ya kweli nchini.
 a. Mabadiliko yaletayo neema na kujenga upya mfumo wa uchumi, haki na sheria nchini.
 b. Mabadiliko ya kuimarisha huduma za jamii kama elimu, afya, maji na makazi.
 c. Mabadiliko ya kuondoa umaskini.
 d. Mabadiliko tunayatoahidi ni mabadiliko ya kurejesha matumaini kwa Watanzania kwa kubadili hali zao za maisha.
 4. Kila mwaka hali na ubora wa maisha ya Watanzania imeshuka wakati tunaambiwa kuwa pato laTaifa linakuwa.
 5. Lakini Watanzania wanachotaka siyo takwimu bali kuona kipato chao kinakua, shule, hospitali na barabara bora zinajengwa.
 6. Wanataka kupata maji safi na salama ya kunywa. Wanataka makazi bora.
 7. CHADEMA na UKAWA, tuna dhamira ya kuleta mabadiliko ya kweli ili kuona azma ya Watanzania tangu uhuru ya kuondoa umaskini, maradhi,na ujinga inahitimishwa.
 8. Ili tufanye hivyo tuahitaji tufanye mabadiliko ya fikra, uongozi, sera na utendaji.
 9. Leo Tanzania inakabiliwa na changamoto nyingi za ki-uchumi, kisiasa na kijamii. Changamoto hizi ni matokeo ya sera za utawala wa Chama kimoja wa miaka hamsini. Sote ni wahanga wa siasa na sera hizi.
 10. Miaka Hamsini ya CCM imetosha. Tunataka mabadiliko na siyo ahadi zile zile kila mwaka.
 11. Tusidanganyike, CCM hawana jipya.
 12. Chagueni UKAWA wenye dira ya kubadili maisha ya wananchi.
 13. Mimi ninauchukia umaskini na mimesimamia maendeleo kwa vitendo. Nilipokuwa Waziri Mkuu nilijaribu kubadili hali hii. Nilisimamia ujenzi wa shule za kata, Chuo Kikuu cha Dodoma. Nilihakikisha mikataba mibovu ya maji inavunjwa na sasa wananchi wa kanda ya ziwa wanapata maji safi.
 Ndugu watanzania
 14. CCM wanauliza tuna mpango gani wa kumaliza umaskini. Sisi hatuahidi tu. Tutatenda.
 15. Ilani yetu ni dira ya kuondoa umaskini kwa mikakati sahihi na siyo nadharia.
 16. Mkakati wa kuondoa umaskini si wa sekta kwa sekta bali wa sekta zote kwa pamoja. Ni ujumla wa utendaji na utekelezaji wa sera za kila sekta utakao leta maendeleo.
 17. Mkakati wangu na UKAWA wa kuondoa umaskini utakuwa na nguzo tano:-
 a. Kupunguza matumizi ya serikali na mashirika yake na kuimarisha utendaji na uwajibikaji.
 b. Kukuza pato la serikali kwa kudhibiti ukwepaji na misamaha ya kodi holela na kuhakikisha nchi inawekeza katika sekta muhimu na inapata gawio halisia kutoka wawekezaji
 c. Kukuza uchumi kwa sera na sheria endelevu ikiwa ni pamoja na kukuza biashara na uwekezaji hasa katika sekta za madini, kilimo, viwanda, ufugaji na uvuvi na kuondoa kodi kwa wanyonge.
 d. Kuimarisha huduma za umma kama elimu, afya, maji na makazi, na mazingira
 e. Kuimarisha utawala bora na mfumo wa haki na sheria chini ya Katiba ya Wananchi.
 18. Chini ya misingi hii na ili kufanikisha mkakati wa kuondoa umaskini, serikali yangu itafanya yafuatayo:-
ELIMU BORA KWA KILA MTANZANIA
 Nimelisema hili huko nyuma. Nalisema tena leo. Elimu kwanza, Elimu kwanza, Elimu kwanza.
 Kwa hiyo mkakati wetu wa msingi utakuwa kutoa Elimu itatayogharamiwa na serikali kwa kila Mtanzania kutoka elimu ya msingi hadi Chuo Kikuu na pia:-
 1. Kuimarisha elimu ya teknolojia, ustadi na ufundi inayojenga uwezo wa kujiajiri na ushindani katika soko la ajira.
 2. Ujenzi na uimarishaji wa miundombinu ya elimu ikiwa ni pamoja na shule za Kata.
 3. Kusimamia ubora wa viwango vya elimu kote nchini.
 4. Kuimarisha taaluma na mitaala katika mashule.
5. Kuondoa utoro darasani, na kuboresha afya za wanafunzi.
 6. Kuboresha maslahi na vitendea kazi kwa walimu ikiwa ni pamoja na nyumba, posho ya kufundishia, usafiri na zana za teknolojia.
 7. Kufuta michango ya maabara ya shule za kata
AFYA
 1. Afya na tiba ya kila Mtanzania itagharamiwa kupitia bima za gharama nafuu na mifuko ya hifadhi ya jamii
 2. Tutaimarisha afya ya msingi pamoja na kinga kupunguza gharama za tiba.
 3. Serikali itahakikisha kuna uwiano na upatikanaji wa watumishi wa afya katika kada mbalimbali ili kuleta tija na huduma stahiki.
 4. Itaimarisha miundombinu ya afya pamoja na kujenga hospitali za kisasa ili kusogeza huduma za afya karibu na jamii na pia kuepukana na tiba za nje ya nchi.
 5. Tutarejea kwa lengo la kuboresha maslahi na vitendea kazi katika sekta ya Afya ikiwa ni pamoja na nyumba na usafiri.
 6. Tutathibiti ongezeko la gharama za huduma za afya bila kuathiri uendeshaji wa watoaji huduma za afya kama vile serikali na hospitali za sekta binafsi.
ARDHI, MAJI NA KILIMO
 1. Tutaimarisha mfumo wa umiliki wa ardhi kwa Watanzania na kudhibiti migogoro ya ardhi hasa kati ya wakulima na wafugaji.
 2. Tutapima ardhi yote ya Tanzania na kumilikisha vijiji na wakulima kwa hati za serikali ili kuipa thamani.
 3. Tutaleta mapinduzi ya kilimo kwa kuimarisha elimu, ufundi na teknolojia ya kisasa na kumkomboa mkulima kutoka jembe la mkono.
 4. Tutasimamia kilimo, ufugaji na uvuvi wa kisasa na kuunganisha sekta hizo na ya viwanda.
 5. Kuhakikisha kuwa wananchi wanatunza na kulinda vyanzo vya maji.
 6. Tutakuza kilimo cha umwagiliaji kwa kuwapa wakulima elimu na mikopo ya riba nafuu ya kuvuna maji na kujenga miundombinu husika.
 7. Tutaweka mazingira rafiki yatakayomhakikishia kwa kila Mtanzania kupata maji safi na salama. Kumaliza kero za maji nchini kutamkomboa mwanamke kutokana na adha ya kuchota maji kwa kichwa
 8. Nitafuta kodi zote za mazao na mifugo kwa wakulima na wafugaji.
 9. Tutasimamia kilimo cha biashara kinachozingatia maslahi ya nchi na ya Watanzania.
 10. Tutaanzisha programu maalum ya kufufua mazao asilia ya Tanzania hususan mkonge.
 11. Tutaanzisha Benki ya Maendelo ya Ufugaji na Uvuvi.
MIUNDOMBINU
 1. Tutaboresha bandari zilizopo na kujenga mpya kama vitega uchumi vya Taifa ili kurejesha biashara tulizopoteza kwa bandari za nchi jirani.
 2. Tutajenga barabara nchini kwa kuzingatia ubora hasa zile za vijijini.
 3. Tutajenga reli ya kati kwa viwango vya kisasa
 4. Tutajenga shirika la Ndege la Taifa linalojiendesha kwa misingi ya faida.
 5. Tutajenga miundombinu ya kisasa na kuondosha misongamano ya magari hasa katika majiji ya Dar es salaam, Mwanza, Mbeya na Arusha
 6. Tutaimarisha uzalishaji na usambazaji wa umeme vijijini ili kufikia zaidi ya asili mia sabini na tano ya Watanzania
VIWANDA
 1. Tutaimarisha sekta ya viwanda kuwa mhimili wa uchumi kwa uzalishaji wa bidhaa na ajira endelevu
 2. Tutajenga viwanda vipya vya kusindika mazao ya kilimo, uvuvi na ufugaji.
 3. Tutahakikisha kuwa ndani ya miaka mitano mali ghafi zote za Tanzania zinasindikwa kabla ya kusafirishwa nje ili kuongeza mapato na ajira ya mamilioni ya vijana.
 4. Tutaanzisha Benki ya Ukuzaji wa Viwanda
UCHUMI
 1. Tutabadili mfumo wa Uchumi wa nchi ili kuhakikisha kuwa mfumo wa uchumi wa Tanzania unakuwa ni wa soko-kijamii ambapo nguvu za soko zitatumikia jamii kwa serikali kuweka uwiano wa mapato unaohakikisha huduma za kijamii zinapatikana kwa ufanisi.
 2. Tutalinda sekta binafsi na bidhaa za ndani kwa kuwapa Watanzania upendeleo wa maksudi kwa kipindi cha mpito ili waimarike na waweze kuhimili ushindani. Tutawapa wafanyabiashara wetu upendeleo katika manunuzi ya serikali na kuwajengea mazingira mazuri ya biashara na kodi endelevu.
 3. Tutawawezesha Watanzania kupata mitaji ya biashara kwa masharti nafuu kabisa.
 4. Tutavutia uwekezaji na wawekezaji wenye tija. Kuweka udhibiti wa wahamiaji wasioleta tija wala maslahi kwa Taifa.
 5. Tutaimarisha sera ya ubia baina ya Serikali na Sekta binafsi kwenye maeneo muhimu ya kiuchumi na kibiashara. Pia, kuwawezesha Watanzania kuwekeza kwa njia ya ubia na wawekezaji wenye mitaji mikubwa bila kujali wanapotoka.
 6. Tutaimarisha usimamizi kwa kubadilisha mfumo wa Vyama vya Ushirika nchini ili utokane na uendeshwe na wakulima wenyewe ikiwa na pamoja na kuwawezesha kuboresha makazi kwa mpango wa kushirikiana kujenga nyumba bora
 7. Tutaanzisha na kuwezesha uanzishaji wa viwanda vidogovidogo vinavyotoa ajira kwa wingi kwa kuvihusisha na vyuo vya ufundi na benki maalum kwa lengo hilo.
AJIRA
 1. Tutasimamia swala la ajira hasa kwa vijana kwa kukuza elimu ya ufundi ili waweze kujiajiri
 2. Tutazipa kipaumbele sekta zinazozalisha ajira kwa wingi hasa za viwanda, kilimo, ufugaji, uvuvi na utalii na kuzipa unafuu wa kodi ili zikue kwa haraka.
 3. Tutawapa wawekezaji wakubwa katika sekta hizi upendeleo maalum na viwango vya kodi nafuu.
NISHATI NA MADINI
 1. Serikali itashiriki kikamilifu katika uzalishaji wa nishati
 2. Itatengeneza mazingara mazuri ya kisera yatakayovutia na kuwezesha ushiriki wa Watanzania na ubia kati yao na wageni.
 3. Serikali yangu itaupa uzalishaji mkubwa wa umeme wa maji kipaumbele namba moja, umeme wa makaa ya mawe kipaumbele namba mbili, umeme wa gesi asilia kipaumbele namba tatu na umeme wa urana kipaumbele namba nne.
 4. Serikali itatoa vipaumbele muhimu kwenye usambazaji wa huduma kubwa ya umeme sehemu za uzalishaji uliyolenga masoko ya ndani, ya nchi jirani na ya nchi za kigeni.
 5. Itapitia upya mikataba yote mikubwa ya nishati na madini ili kubaini iliyo mibovu na kuifanyia maboresho.
 6. Serikali yangu itatumia sehemu ya hisa zake kwenye raslimali kubwa ya gesi asilia iliyopatikana hapa nchini kama rehani kwenye kujichukulia mikopo kwa ajili ya ujenzi wa miundo mbinu ya mabomba ya gesi.
 7. Serikali itatoza kodi na ada ndogo zaidi kwa wazawa wenye ubia kati yao na wageni kuliko zitakazotozwa kwa wageni wasiowekeza kwa kushirikisha wazawa.
 8. Serikali itasitisha utoaji wa misamaha ya kodi isiyo lazima kwenye sekta ya madini, na badala yake itawekeza kwenye kuongeza thamani ya raslimali zake za madini.
 9. Tutakuza nishati mbadala kutamkomboa mwanamke kutokana na adha ya kukata kuni
MALIASILI NA UTALII
 1. Tutasimamia uvunaji na matumizi ya rasilimali za Taifa kwa manufaa ya kila Mtanzania wa kizazi hiki na kijacho
 2. Tutapiga vita ujangiri na kuimarisha utunzanji wa hifadhi za taifa na mazingira
 3. Tutachochea ujenzi wa miundombinu ya utalii nchini ikiwa ni pamoja na ujenzi wa mahoteli na kuimarisha mafunzo
 4. Tutaongeza idadi ya watalii kufikia milion mbili ifikapo 2020.
UTAWALA BORA, ULINZI WA NCHI NA USALAMA WA RAIA
 1. Tutasimamia Katiba mpya inayolinda haki za msingi za wananchi na kuweka bayana mipaka ya madaraka ya serikali na viongozi, Bunge na Mahakama.
 2. Tutaboresha miundobinu ya sheria na kuimarisha utendaji wa Mahakama na maslahi ya wafanyakazi
 3. Tutasimamia haki za raia na kuangalia upya sheria kandamizi ili wananchi kama Masheik wa Zanzibar hawasoti jela kwa sababu za kisiasa.
 4. Tutaimarisha mafunzo ya vyombo ya Polisi hasa wapelelezi na waongoza mashtaka ili wapate uwezo wa kusimamia utoaji wa haki.
 5. Tutavipa vyombo vyote vya ulinzi na usalama nyenzo na kuboresha mazingira yao ya kazi na maslahi

UZALENDO, UTENDAJI NA UWAJIBIKAJI
 1. Tutajenga uzalendo ili kila Mtanzania aweze kutathmini mchango wake kwa taifa kila siku
 2. Tutaimarisha nidhamu, utendaji na uwajibikaji katika Sekta ya Umma
 3. Tutaimarisha mchango wa Wataalam wetu, wanawake na vijana katika kusimamia uchumi na kuwajengea mazingira stahiki ya kazi pamoja na mafao.
 4. Tutapiga vita rushwa na ubadhirifu katika sekta ya Umma na binafsi
 5. Tutadhibiti na kupunguza matumizi ya serikali ikiwa ni pamoja na kufuta safari za watumishi serikalini zisizokuwa muhimu pamoja na zile za Rais na kupiga marufuku matumizi ya mashangingi serikalini.
 6. Tutadhibiti deni la Taifa kwa kuanza na ukaguzi wa madeni ya serikali ili kuhakiki jinsi yalivyotumika
 7. Tutaimarisha uwazi na kuondoa usiri katika shughuli za serikali na kuweka bayana mikataba yote ya nchi ikiwa ni pamoja na ile ya mafuta, madini na gesi asilia

 KUKUZA PATO LA SERIKALI
 1. Tutadhibiti mapato kutokana na raslimali kwa kupitia upya viwango vya mirabaha kutokana na madini na gesi asilia ili kuhakikisha kuwa Tanzania inapata gawio stahiki.
 2. Serikali itaanzisha Wizara maalum itakayosimamia nishati ya gesi na mafuta.
 3. Tutaimarisha ofisi ya Msajili wa Hazina ili kusimamia vema uwekezaji wa Serikali katika mashirika na mapato yake.
 4. Tutahakikisha kuwa mashirika ya umma yanaendeshwa kwa misingi ya faida na uadilifu.
 5. Tutadhibiti ukwepaji kodi za ushuru wa forodha na kupiga marufuku misamaha ya kodi holela ili kuokoa mabilioni ya fedha yanayopotea kila wiki.
 6. Sambamba na hilo tutarahisisha utaratibu wa kulipa kodi ili kuondoa kero na mazingira ya rushwa. Kwa kudhibiti makusanyo ya kodi tutakusanya fedha za kugharimia huduma za msingi kama afya na elimu kikamilifu.

 KUIMARISHA MUUNGANO
 1. Tutaimarisha umoja, usalama na udugu wa Watanzania na Muungano kwa misingi ya haki na usawa
 WANAWAKE, WATOTO NA WAZEE
 1. Wanawake watapewa fursa na haki sawa katika elimu na uchumi ili waweze bila kuwezeshwa.
 2. Tutahakikisha wazazi wanapata fursa ya kuwa walezi na wafanyakazi kwa kuongeza urefu wa likizo ya uzazi
 3. Tutaimarisha elimu ya watoto hasa wasichana na kukuza fursa zao na kukomesha ndoa za watoto wadogo.
 4. Tutaongeza uwakilishi wa akina mama katika ngazi zote serikalini na mashirika yake kufikia asili mia hamsini ifikapo 2020.
 5. Wazee na wasiojiweza watapewa posho ya kujikimu inayokidhi mahitaji ya msingi itakayowawezesha kuishi kwa heshima na kulinda utu wao ndani ya familia na jamii zao.
 SANAA, UTAMADUNI NA MICHEZO
 1. Tutaendeleza na kuwezesha vipaji vya sanaa na michezo
 2. Tutarudisha viwanja vya michezo vilivyovamiwa
 3. Tutafuta kodi zote za vifaa vya michezo.
 4. Tutadhibiti viwango na maadili ya bidhaa za nje zinazoingizwa nchini na kuzitoza kodi halisia
 5. Tutajenga taasisi na vyuo vya kukuza michezo ili kuhakikisha kuwa ndani ya miaka mitano Tanzania inashiriki kwa ushindi katika mashindano ya kimataifa ya soka na riadha
 6. Tutalinda Hakimiliki za sanaa nchini
 7. Tutafuta kodi za sanaa kwa wasanii chipukizi ili kuwapa muda kwa kujijenga.
 SERA YA MAMBO YA NJE YENYE TIJA KWA TAIFA
 1. Tutakuza ushirikiano wa Kimataifa wenye tija na Ujirani mwema.
 2. Tutatetea haki za binadamu, usawa wa nchi na kuimarisha ushiriki wa Tanzania katika diplomasia ya kimataifa.
 3. Tutakuza umoja na ushirikiano wa Umoja wa Afrika, Jumuia ya Afrika Mashariki, SADC na Umoja wa Mataifa.
 4. Tutaimarisha Umoja wa Mataifa ikiwa ni pamoja na kudai mabadiliko ya mfumo ili kuleta usawa wa nchi shiriki.
 Ndugu Watanzania
 Naomba nimalizie kwa kusema yafuatayo
 1. Natambua kuwa uongozi ni dhamana. Mkinichagua nitaienzi dhamana hiyo kwa utendaji uliotukuka.
 2. Nawaahidi Watanzania kuwa kwa uwezo, akili, uzoefu na nguvu zangu zote nitawatumikia. Nawaomba nanyi mniahidi jasho lenu na uwezo wenu wote ili kwa pamoja tuvuke. Tutajikomboa toka utawala wa CCM unaodumaza uchumi na maendeleo. Tutaanza safari ya uhakika kuondoa umaskini.
 3. Mabadiliko pia ni kuthamini utu na kukataa hadaa ya hongo ili kuuza haki yako ya kuchagua. Msikubali rubuni za uchaguzi kwa kupewa pesa au vitu. Rushwa ya uchaguzi ndiyo sera ya CCM. Ukikubali basi umeuza pia haki na sauti yako ya kuwalalamikia walio madarakani. Imetosha. Tukatae. Tulinde utu na haki zetu. Tuchague mabadiliko.
 4. Mabadiliko ni fikra. Ni kufikiri na kutenda tofauti. Hatuwezi kuendelea kufikiri na kutenda kama kwamba hatuna dharura ya maendeleo. Kwanza tuanze kwa kufanya mabadiliko na tujiamini kuwa sisi kama Taifa tunaweza. Tunaweza kujitegemea na kuleta maendeleo yetu wenyewe bila kutegemea wafadhili. Hii si ndoto. Nchi nyingi zimefanikiwa kuondoa umaskini katika kizazi kimoja. Tujifunze kutoka kwao.
 5. Tuwe taifa linalotumia raslimali zake kujiendeleza na siyo kuwanufaisha wageni na kuwafanya Watanzania watwana katika nchi yao. Inabidi tuache kuwa taifa ombaomba. Tuache kuukubali na kuvaa umaskini kama joho la fahari.
 6. Mabadiliko ya kweli hayawezi kuletwa na CCM. Tusitegemee kuwa leo wana jipya. Ndiyo maana ahadi walizotoa miaka thelathini iliyopita ndizo wametoa juzi. Tukatae hadaa. Miaka hamsini ya CCM imetosha.
 7. Tunaamani kwamba tutashinda kwa sababu Watanzania mpo nyuma yetu. Watanzania mmeamua kuleta mabadiliko. Kura yako ndiyo itakayokuwa mkombozi wako. Hakikisha unapiga na kuilinda kura yako. Wakati wa mabadiliko ni sasa.
 Mungu ibariki Tanzania. Asanteni sana

November 22, 2014

Sakata la ESCROW: Ripoti inaonyesha Vigogo zaidi ya 50 watakumbwa na gharika.

Dar/Dodoma. Moto wa kashfa ya ufisadi katika akaunti ya Tegeta Escrow unaoendelea kuwaka bungeni, sasa unaonekana kugeuka gharika inayoweza kuwakumba vigogo wengi zaidi na kuiweka Serikali ya Rais Jakaya Kikwete katika hali ngumu.
Kashfa hiyo ya uchotaji wa Sh306 bilioni za akaunti ya Escrow, inahofiwa kuwakumba vigogo zaidi ya 50 ndani ya Serikali wakiwamo mawaziri, makatibu wakuu, wabunge, majaji na wakuu wa taasisi za Serikali waliohusika.
Habari zilizopatikana zinaeleza kuwa kutokana na kuwapo kwa idadi kubwa ya mawaziri na watendaji wa Serikali na mahakama, inatishia anguko la Serikali.
“Kuna waziri (anamtaja) ameniambia ameangalia ile orodha ya watu wanaodaiwa kuchukua fedha hizo ni zaidi ya 52. Hofu yangu hili jambo likiingia bungeni na kujadiliwa huenda likasababisha kuvunjwa kwa Baraza la Mawaziri kwa mara nyingine,” alisema mbunge mmoja kutoka Kanda ya Mashariki.
Wabunge wajipanga Mbunge mwingine kutoka Zanzibar (CCM), alisema kuwa anasubiri kwa hamu kuchangia katika mjadala huo ili waondoke wale wote ambao wamekwapua fedha hizo.
Juzi, Waziri Mkuu Mizengo Pinda aliitisha kikao cha mawaziri ambacho kilihudhuriwa na baadhi ya mawaziri na walifikia uamuzi kuwa suala hilo litajadiliwa ndani ya chama kabla ya kuingia ndani ya Bunge.
“Kinachosubiriwa ni ripoti ya Kamati ya Hesabu za Serikali (PAC) halafu tutakutana wabunge wa CCM kabla ya kwenda bungeni,” alisema mmoja wa wajumbe wa kikao hicho.
Pamoja na hali hiyo, wabunge katika makundi makundi kwa wiki nzima wamesikika wakijadili jambo hilo huku wakilihusisha na mbio za urais mwakani.
Mbunge mmoja (jina tunalo) alisema kuhusishwa kwa Waziri Mkuu Mizengo Pinda katika sakata hilo kunatokana na mtuhumiwa mmoja ambaye ni kiongozi katika Wizara ya Nishati na Madini, kuwa mmoja wa meneja wake wa kampeni.
“Hakuna mahali ambapo Pinda ameguswa moja kwa moja katika ripoti ya CAG (Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali) wala Takukuru (Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa), bali wanasema ni kwa sababu ya kampeni za urais na mhusika mmoja katika sakata hilo anatajwa kuwa kama Pinda akipata urais, yeye ndiye  atakayekuwa Katibu Mkuu Kiongozi,” alisema mbunge huyo kutoka upinzani.
Jana Mbunge wa Kilwa Kaskazini (CCM), Murtaza Mangungu akizungumza na gazeti hili, alisema sakata hilo linatakiwa liishe kwa kuwa linaumiza uchumi wa nchi kwa kuwa mtambo wa IPTL ni matatizo.
“Hili jambo kwa namna yoyote lazima liishe na kwamba mwisho wake ni bora tutaifishe ule mtambo na ufie mbali,” alisema Mangungu.
Alisema linatakiwa liishe kwa kuwa limekuwa ni jambo la kushutumiana kila upande kitu ambacho si kizuri, na kwamba Bunge linapaswa kusimama  kuonyesha makali yake.
“Ni mzigo kwa wananchi hivyo lifike mwisho. Ni heri shari yenye heri kuliko heri yenye shari,” alisema Mangungu.
Mbunge wa Ole (CUF), Rajabu Mohammed Mbarouk alisema sakata hilo limetokea juu na sasa limefika chini na kukwamisha mambo mengine yasifanyike.
“Bunge haliwezi kuisha kwa kuwa linagusa masilahi ya watu wengi, pia linagusa masilahi ya chama. Hili hata lijadiliwe bungeni haliwezi kuisha hivyo,” alisema Mbarouk.
Alisema ni jambo la ajabu kama alivyosema Zitto kwamba halikufaa kufanyika kwenye nchi ambayo ina dola, bali lingefanyika kwenye nchi ambazo hazina mhimili wa dola kama Somalia.
“Haya mambo yanaweza kumwangusha Waziri Mkuu na wengine, hivyo ni jambo zito,” alisema Mbarouk.
Mbunge wa Kasulu Mjini (NCCR-Mageuzi), Moses Machali akiwasilisha maoni ya kambi ya upinzani kuridhia Itifaki ya Uzuiaji wa Vitendo Haramu dhidi ya Miundombinu jana, alisema viongozi kama wabunge na mawaziri wametajwa kupiga dili katika akaunti ya Tegeta Escrow kwa kuwa viongozi wa Serikali hawaonyeshi dhamira njema katika kuheshimu misingi ya utawala bora na ndiyo maana wezi na mafisadi wanaotakatisha fedha kiharamu wameendelea kuachwa.
Alisema katika uchotwaji wa fedha hizo, Serikali imedhihirisha wazi kwamba ufisadi ni sehemu ya maisha ya baadhi ya mawaziri na watendaji wa Serikali.
“Ni aibu na majanga kwa Waziri Mkuu na mawaziri wengine kusema kwamba suala la Escrow haliwezi kuzungumzwa bungeni kwa sababu eti liko mahakamani, jambo linaloashiria Waziri Mkuu anakusudia kuwalinda wale wanaotajwa kuchota fedha hizo,” Machali alisema na kuongeza:
“Mbaya zaidi ni pale inapoonekana wazi mhimili wa Bunge unaingiliwa na mhimili mwingine unaotajwa  kuliandikia Bunge barua likitaka kutojadiliwa sakata la Escrow jambo ambalo ni dharau kwa Bunge.”
Kwa upande wake, Zitto ambaye kamati yake inapitia ripoti hiyo hakutaka kuzungumzia chochote kuhusu sakata hilo lakini juzi aliwataka wabunge wajiandae kupambana na taarifa atakazoziwasilisha mezani mara tu ripoti hiyo itakapokabidhiwa bungeni kwa ajili ya majadiliano.
Escrow yavuka mipaka ya nchi Sakata la utoroshwaji wa fedha katika akaunti ya Escrow ambalo linawaandama baadhi ya watendaji wakuu wa Serikali limejitokeza kwa sehemu kubwa katika baadhi ya magazeti ya nchi za Magharibi  yaliyohoji jinsi Serikali inavyoingiwa na kigugumizi cha kulipatia ufumbuzi sakata hilo.
Magazeti hayo likiwamo DailyMail  la Uingereza ambalo lililowahi kufichua kuwapo kwa vitendo vya ufisadi katika uwindaji wa wanyamapori kulikolisababishia taifa hasara kubwa, lilisema kuwa Tanzania inaendelea kuandamwa na jinamizi la ufujaji wa mali ya umma.
DailyMail limesema wabunge wameibana Serikali wakitaka kujadiliwa kwa ripoti ya Escrow ili kuliokoa taifa ambalo tayari limeanza kuonja machungu ya kusitishiwa misaada kutoka kwa wafadhili wa kigeni.
Katika ripoti yake hiyo ambayo imelinukuu Shirika la Habari la Reuters, DailyMail ilisema rushwa ni ugonjwa unaoendelea kuiandama Tanzania na kwamba vitendo hivyo sasa vimevuka mipaka na kuwakwaza wawekezaji wa kigeni.
Limesema kuwa Tanzania ambayo hivi karibuni ilitangaza kugundua hifadhi kubwa ya gesi iko katika njiapanda na bado haieleweki hatima yake hasa baada ya Serikali kuonyesha kuwa haiko tayari kuruhusu ripoti hiyo ijadiliwe hadharani.
Chanzo: Mwananchi

November 12, 2014

Samson Mwigamba atimuliwa uongozi ACT-Tanzania, Prof.Kitila, Mchange wapewa karipio kali!

Katibu Mkuu wa ACT- Tanzania Samson Mwigamba (Katikati)

Katibu Mkuu wa ACT- Tanzania Samson Mwigamba amesimamishwa uongozi ndani ya chama hicho kwa tuhuma za ukiukwaji wa maadili,kuvunja katiba na ubadhirifu ndani ya chama hicho.

Taarifa kutoka kwa waasisi wa chama hicho ambao ni Greyson Nyakarungu na Leopold Mahona zinasema mbali na Mwigamba pia chama hicho kimetoa karipio kali kwa viongozi waandamizi wa chama hicho Professor Kitila Mkumbo na Habib Mchange kwa tuhuma mbalimbali.

Ikumbukwe Samson Mwigamba,Prof Kitila Mkumbo na Zitto Kabwe walitimuliwa uongozi ndani ya CHADEMA mapema mwaka huu kwa tuhuma kama hizi na kusababisha kukimbilia chama cha ACT Tanzania.

Chanzo:Mtanzania Jumatano

Habari zaidi

 Habib Mchange

Kitila Mkumbo

Zitto Kabwe

Waasisi wa ACT Tanzania Greyson Nyakarungu na Leopold Mahona waliwaambia waandishi wa habari jana kuwa waliwakaribisha Kitila Mkumbo na Samson Mwigamba ndani ya chama hicho kwa nia njema kumbe ni wasaliti na walaghai wakubwa.


Alisema kwanza kina Mwigamba wanajivika uasisi wa ACT huku wakijua si kweli. Pia kina Mwigamba wanatuhumiwa kwenda ofisi ya Msajili kubadili nembo ya chama kinyume cha utaratibu. Pia wanatuhumiwa kusajili katiba nyingine kinyume na Katiba waliyoandaa waasisi na kupatia chama usajili.

Nyakarungu amesema tayari Waasisi halali wa ACT wameshamwandikia barua msajili wa vyama kumuelezea juu ya uasi unaofanywa na Mwigamba na Kitila.

November 5, 2014

UKAWA wanasa waraka wa siri wa ikulu kuingilia mchakato wa katiba!

Viongozi wa vyama vinavyounda umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA)

Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), umeibua maeneo yanayoongeza mgogoro kwenye mchakato wa Katiba inayopendekezwa, ukieleza kuwa serikali inaingilia zoezi hilo.

Aidha, umeibua shutuma nzito ukidai kuwa serikali imetenga Sh. bilioni 2.5, kwa ajili ya kutoa mada kwenye vyombo mbalimbali vya habari kutaka wananchi waipigie kura ya ndiyo wakati hairuhusiwi kisheria.

Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti Mwenza wa Ukawa, Prof. Ibrahim Lipumba, alisema sheria ya kura ya maoni inaielekeza Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Nec) kusimamia mchakato wa kura ya maoni kuanzia kuboresha daftari la wapigakura hadi kutangaza tarehe ya kupigakura ya maoni.

Alisema kinyume cha sheria hiyo, Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Frederick Werema, alikaririwa akitangaza kuwa kura ya maoni itafanyika Machi 30 wakati Rais Jakaya Kikwete naye alitangaza kuwa kura hiyo itapigwa Aprili, mwakani.

Alisema uboreshaji wa daftari haujafanyika, wala kazi ya kutoa elimu kwa umma inayopaswa kufanywa na Nec bado haijaanza, lakini katika hali ya kushangaza tayari serikali imetangaza tarehe ya kupiga kura.

“Lakini la kustaajabisha ni kwamba Ikulu imeandaa mpango ambao umeelekezwa na Rais Kikwete wa kufanya kampeni utakaogharimu Sh. bilioni 2.5 kwa kutumia vyombo vya habari ili kuwashawishi wananchi waipigie kura ya ndiyo Katiba inayopendekezwa kwa sababu ni ya serikali,” alisema.

Prof. Lipumba alisema sheria haijaviruhusu vyombo vya serikali wajibu wa kufanya kampeni badala yake ni Nec na asasi za kiraia zenye jukumu la kutoa elimu kwa raia na kuunda makundi mawili ya kufanya kampeni.

“Sasa serikali ambayo haimo ndani ya sheria imejisajili yenyewe na kuandaa mpango wa kufanya kampeni. Inasikitisha ambavyo Rais Kikwete haheshimu sheria za nchi…anaanzisha kikundi ndani ya Ikulu kitakachotumia fedha za wananchi kufanya kampeni hii,” alisema.

Kwa upande wake, Katibu wa Ukawa, Dk. Wilbrod Slaa, alisema umoja huo umepata waraka wa Ikulu unaoeleza namna fedha hizo zitakavyotumika ‘kunyonga’ mawazo ya wananchi kwenye kuamua hatma ya Katiba pendekezwa ambao utagharimu kiasi hicho cha fedha.

Alisema katika waraka huo, Rais Kikwete amemwelekeza Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo kuitangaza Katiba pendekezwa ili waipigie kura ya ndiyo ilhali Rais alipaswa kuelekeza wananchi waisome na kuielewa ndipo wapige kura ya ndiyo au hapana kwa utashi wao.

“Kifungu cha tatu cha waraka huu kinaeleza kuwa Rais Kikwete ametoa maelekezo ya kutaka wananchi waipigie Katiba pendekezwa kura ya ndiyo ili kuiepusha serikali na aibu na tahayari ambayo inaweza kutokea kama wananchi wataikataa Katiba,” alisema.

Dk. Slaa ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Chadema, alisema mpango huo unahusisha kampeni ya kuandaa vipindi kwenye televisheni, radio na makala kwenye magazeti ambazo zote zitalipiwa.

Naye Mwenyekiti Mwenza wa Ukawa, James Mbatia, alisema umoja huo haujachoka na hautakata tamaa katika kudai Katiba mpya na kwamba suala la Katiba linahitaji maridhiano na siyo mabavu. Alisema hakuna mtu mwenye haki ya kuamua kuhusu Katiba pendekezwa na kuhofia kwamba mpasuko mkubwa zaidi utaendelea kutokea nchini.

WAMPA POLE WARIOBAUmoja huo umempa pole aliyekuwa Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba, na kumtaka awe ‘ngangari’ kuendelea kudai Katiba.

Alisema asasi za kiraia ikiwamo Taasisi ya Mwalimu Nyerere zina haki kisheria ya kutoa elimu kwa umma na kwamba alichofanyiwa Jaji Warioba ni ukiukwaji wa sheria hiyo.
“Jaji Warioba ni mtu mwenye heshima kubwa nchini, kwa CCM kuratibu mbinu hizi ni wazi kuna mkakati wa kuzuia mawazo ya watu wenye mawazo tofauti kutoa maoni yao,” alisema Prof. Lipumba.

Alisema vurugu alizofanyiwa Jaji Warioba zimelenga kuwanyamazisha wajumbe wa iliyokuwa Tume ya Katiba kueleza kilichopo kwenye Katiba pendekezwa.

Mbatia amemtaka Jaji Warioba na wananchi wengine kutokata tamaa kuhusu Katiba kwa kuwa kufanya hivyo hakutaivusha nchi.

Wakati huo huo, Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Bawacha), Halima Mdee, ameituhumu Ikulu kwamba imeandaa mkakati wa kuwadanganya wananchi na kuwashawishi kuipigia kura ya ndiyo Katiba inayopendekezwa kupitia vipindi vya Radio na Televisheni pamoja na kuchapisha makala katika magazeti.

Kwa mujibu wa Mdee, mkakati huo unaojulikana kama ‘ijue Katiba inayopendekezwa’ unatarajia kutumia Sh. bilioni 2.5 ambao kwa vipindi vya radio na televisheni pekee vimetengewa milioni 700.

Mdee alisema hayo wakati akihutubia wananchi wa kijiji cha Mwandoya, wilayani Meatu mkoani Simiyu juzi jioni ikiwa ni sehemu ya ziara yake anayoifanya katika mikoa ya Kanda ya Ziwa Mashariki.

Alisema lengo la mkakati huo ni kuiepusha serikali na aibu na tahayari ambayo inaweza kutokea, endapo wananchi wataikataa katika kura ya maoni.
Pia alisema ni kukabiliana na upotoshaji ambao Ikulu imedai unafanywa na makundi yanayoipinga katiba hiyo.

Mdee alisema vipindi hivyo pia vitahusisha radio za jamii kwenye wilaya na mikoa mbalimbali na kuandika makala mbalimbali kwenye magazeti ambazo zitakuwa zinaandikwa vichwa vya habari vyenye kushawishi kuunga mkono kupigia kura ya ndiyo Katiba inayopendekezwa.

Mdee alisema tayari Ikulu imeagiza kuwapo na kamati ya kudumu ya habari ya kusimamia mpango wa kuelimisha umma hadi pale itakapofanyika kura ya maoni.
Mdee alisema jumla ya jopo la watu 20 wameandaliwa kushiriki katika vipindi hivyo na kila kwamba kila mshiriki atakuwa analipwa kati ya Sh. 500,000 na Sh. 200,000 kwa kila kipindi.

“Wamechakachua maoni ya wananchi ambayo waliyapendekeza, wameweka ya kwao na kuyapitisha kwa lazima, sasa wameona kwamba upepo umewakalia vibaya kutokana na uchakachuaji huo sasa Ikulu imeamua kuweka mkakati wa kuwalaghai na kuwashinikiza wananchi waipigie kura ya ndiyo katiba ambayo wamechakachua maoni yao ili kufanikisha mipango yao,” alisema Mdee.

MAJIBU YA IKULU Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu, Salva Rweyemamu, alipoulizwa kuhusiana na taarifa hiyo, alisema alichokisema Mdee ni Proposal (pendekezo) tu na siyo bajeti.
Alisema haoni tatizo kwa serikali kuandaa mpango huo kwa kuwa lengo lake ni kuelimisha umma juu ya Katiba inayopendekezwa.

“Mimi sioni ubaya serikali kuandaa kitu hicho kwa sababu lengo lake ni kutoa elimu kwa umma na kama yeye (Mdee) anavyozunguka nchi nzima kuipinga Katiba, vivyo hivyo kuna wengine watazunguka nchi nzima kuipigia kura ya ndiyo,” alisema Rweyemamu.


CHANZO: NIPASHE

September 18, 2014

Jeshi la Polisi laendeleza vipigo kwa Waandishi wa habari!

 Askari wa Jeshi la Polisi wa kuzuia ghasia wakiwazuia kwa mbwa Waandishi wa habari kufanya kazi yao.


Askari wa Jeshi la Polisi wa kuzuia ghasia wakimpa kipigo cha mbwa mwizi Mwandishi wa habari Bwn. Josephat Isango

Muendelezo wa Jeshi la Polisi nchini kuwanyanyasa, kuwatisha waandishi wa habari na kuwafanya wasitekeleze wajibu wao ipasavyo, ilijidhihirisha wazi jana makao makuu ya jeshi hilo, baada ya waandishi kupigwa, kukimbizwa na mbwa ili wasichukue taarifa za kuhojiwa kwa Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe.
Tukio la kupigwa na kudhalilishwa kwa waandishi wa habari lilitokea jana, limetokea ikiwa ni siku moja baada ya Makamu wa Rais, Dk. Mohamed Gharib Bilal, kuvitaka vyombo vya ulinzi na usalama nchini kushirikiana na waandishi wa habari katika kufanya kazi kwa ajili ya kulinda amani ya nchi.
Waandishi waliyopigwa na Polisi hiyo jana ni Josephat Isango anayeandikia gazeti la Tanzania Daima huku Yusuph Badi ambaye ni mpiga picha wa magazeti ya serikali, akipigwa na ‘kusakiziwa’ mbwa ili wamuume.
Dalili za waandishi wa habari kuzuiwa kufanya kazi yao zilianza kujionesha mapema jana wakati Mbowe alipowasili katika makao makuu ya Jeshi la Polisi, ambako waandishi walizuiwa wasiingie katika eneo hilo kwa ajili ya kuchukua picha na maelezo ya kiongozi huyo.
Akiwa anawaongoza askari wake katika amri ya kushambuliwa kwa waandishi wa habari hiyo jana, Kamishna wa Operesheni na Mafunzo, Paul Chagonja, alisikika mara kwa mara akiwaagiza vijana wake wawaondoe waandishi na hata kuwasakizia mbwa.
Chagonja, alisikika mara kadhaa akitoa amri kwa askari kuwa wawafungulie mbwa ili waweze kujeruhi angalau mtu mmoja kutoa funzo ili wafuasi wa CHADEMA waliokuwa kwenye lango kumsubiri Mbowe waondoke.
“Waondoeni wote msiwaruhusu hata hao waandishi kuingia humu, ninyi askari wa mbwa mnafanya nini hapo wakati watu wamejazana mlangoni wapelekeeni hao,” alisikika akisema Kamishna Chagonja.
Mara baada ya maelekezo hayo ya Kamishna Chagonja, askari waliokuwa na mbwa walianza kuwakimbiza wafuasi wa CHADEMA na waandishi wa habari.
Katika hali ya kustaajabisha, askari watatu kwa pamoja walimfuata Josephat Isango, aliyekuwa akitoka katika lango kuu na kuanza kumshambulia kwa rungu na mateke hali iliyowafanya waandishi wa habari kuingilia kati kwa ajili ya kumnusuru.
Baada ya waandishi kumnusuru Isango, kipigo kiligeukia kwa Mwandishi Yusuph Badi, ambaye wakati akishambuliwa alianguka chini huku askari wenye mbwa wakiwaachia kwa ajili ya kumshambulia.
Kilichomnusuru Badi asiumwe na mbwa hao ni kamera aliyoishika mkononi na kujikinga ili asidhurike, kitendo hicho cha kujikinga kilisababisha kuharibika kwa kifaa hicho.
Wakizungumza baada ya hali kutulia, Badi na Isango, walieleza kuwa kilichofanywa na jeshi la Polisi ni kuminya uhuru wa utendaji kazi wa waandishi katika kuuhabarisha umma wa watanzania juu ya mambo yaliyokuwa yakitokea.
“Ni jana tu wameambiwa namna ya kutoa ushirikiano na vyombo vya habari, lakini leo wanatupiga na kutusakizia mbwa hii si haki na viongozi wetu wanapaswa waangalie mara mbili mbili namna ya kushirikiana na jeshi hili,” alisema Badi.
Jeshi la Polisi limekuwa na kawaida ya kuwanyanyasa, kuwapiga na hata kuwaua waandishi wa habari pale wanapotekeleza wajibu wao wa kukusanya habari.


Tukio linalokumbukwa zaidi la ukatili wa askari wa jeshi hilo kwa waandishi wa habari ni mauaji ya Mwandishi wa kituo cha Televisheni ya Chanel ten mkoani Iringa, Daudi Mwangosi, mauaji yaliyotokea Septemba 2 mwaka juzi katika Kijiji cha Nyololo Mufindi mkoani Iringa wakati mwandishi huyo akiwajibika kukusanya habari.

August 19, 2014

Tetesi: Aliyekuwa Mwenyekiti wa CHADEMA wilaya/jimbo la TMK kukabidhiwa kadi ya CCM kwa mbwembwe!

Bwn. Patrick Yohana Joseph

Tetesi ambazo Blog ya Maisha Times imezipata muda mfupi uliopita zinarepoti kwamba aliyekuwa Mwenyekiti wa CHADEMA wilaya/jimbo Temeke, Mwenyekiti BAVICHA mkoa wa Temeke, Mjumbe wa Baraza Kuu la Chadema Taifa, Mjumbe wa mkutano mkuu wa Chadema Taifa ambaye alivuliwa na kufukuzwa uanachama wa chama hicho kutokana na usaliti na hujuma Bwn. Patrick Yohana Joseph anatarajia kujiunga na Chama Cha Mapinduzi hapo mnamo tarehe 28/08/2014 ambapo atakabidhiwa rasmi Kadi ya CCM na Kiongozi Mkubwa kitaifa wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa mbwembwe za kila namna kama ilivyokuwa kwa Mtela Mwampamba, Juliana Shonza na Madiwani wa Shinyanga ambao walifukuzwa CHADEMA na kuonekana ni almasi ndani ya CCM.

Tetesi zaidi zinadai kwamba mbwembwe na kila ambacho kitafanyika katika siku hiyo lengo kubwa likiwa ni kutumia kiasi kikubwa cha fedha kuwahamasisha wanachama wengi wa CHADEMA kujiunga na CCM ili kukidhoofisha chama hicho pendwa na wananchi walio wengi ambacho kwa miaka kadhaa kimekuwa kikikipa changamoto kubwa chama tawala CCM katika medani ya siasa!

August 8, 2014

Hii ndio Video ya mpango wa usaliti na hujuma kwa CHADEMA!

 Video ya mpango wa Usaliti na Hujuma kwa CHADEMA uliokuwa unapangwa na viongozi wa waandamizi wa CCM na ACT Tanzania umefichuliwa. 

Hakuna siri tena.

Kuangalia Video hiyo Bofya link hii


Waziri wa atajwa njama za kumuua Dk. Slaa na Mnyika!


 Naibu Waziri wa Nishati na Madini Mhe. Stephen Masele.

Hali ya kisiasa nchini imezidi kuwa tete baada ya Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Stephen Masele, kuhusishwa katika njama za kutaka kumuua Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willibrod Slaa na Mkurugenzi wa Habari na Mawasiliano wa chama hicho, John Mnyika.

Mbali na kutajwa katika njama hizo ambazo Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mjini, Anarose Nyamubi anadaiwa kukataa zisitekelezwe katika wialaya yake, Masele pia anahusishwa na kupanga kiasi cha fedha kilichotakiwa kutolewa kwa madiwani wawili wa CHADEMA kama wangeweza kufanikisha mkakati huo.
Tuhuma hizo nzito zilitolewa jana jijini Dar es Salaam na diwani wa Kata ya Ngokelo, Sebastian Peter kutoka mkoani Shinyanga wakati akizungumza na waandishi wa habari katika Makao Makuu ya CHADEMA.

Hata hivyo, wawili hao Masele na Nyamubi hawakuweza kupatikana kujibu tuhuma hizo, na alipoulizwa msemaji wa Jeshi la Polisi nchini, Advera Senso kama waliwahi kupokea malalamiko hayo, alisema hawana taarifa yoyote na kwamba hao waliotoa taarifa hizo wanapaswa kuziwasilisha polisi ili zifanyiwe kazi.
Peter maarufu kama Obama na diwani mwenzake wa kata ya Masekelo, Zakaria Mfukwa, alisema kuwa awali walihamia Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa ahadi ya kuboreshewa maisha ukiwa ni mkakati wa Waziri Masele.

Alifafanua kuwa mkakati huo wa kuwauwa viongozi hao wa CHADEMA ulikuwa utekelezwe mapema Februari mwaka huu, wakati viongozi hao walipofika mkoani Shinyanga kwa ajili ya kukusanya maoni ya wanancchi juu ya muundo wa serikali.

Alisema mara baada ya aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA, Zitto Kabwe kusimamishwa uongozi wa chama hicho, walifuatwa na Habibu Mchange na kuelezwa kuwa kuna mpango unaoweza kuwaondoa katika lindi la umasikini ikiwa wataweza kuufanikisha.

“Baada ya maongezi ya aina mbali mbali na Mchange tulishindwa kupata muafaka lakini tuliendelea kuwasiliana na aliporudi Shinyanga akatueleza kuwa kuna mpango mzuri wa fedha na kwamba utasimamiwa na Waziri Masele na kwamba tutapata sh. milioni 180 kila mmoja,”alisema.

Aliongeza kuwa alipigiwa simu na Masele na kisha kuelekezwa kazi ya kufanya kuwa ni kutoa taarifa ya helikopta iliyombeba Dk. Slaa na Mnyika ingetua eneo gani itakapofika Shinyanga Mjini na kwamba ni  nani wengine ambao wangekuwa katika msafara huo, huku wakielezwa kuwa jukumu lao lingeishia katika kutoa taarifa na mikakati ya ulipuaji ingesimamiwa na Masele.

Alisema katika mkakati huo, mkuu wa Wilaya ya Shinyanga mjini, Anarose Nyamubi ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya wilaya alikataa mpango huo kutekelezwa katika wilaya yake hali iliyowafanya wao wajiulize kama wana sababu ya kuendelea na jambo hilo.
“Nilipofikiria Taifa na nikafikiria namna msiba wa Dk. Slaa na Mnyika utakavyopokewa nikaona siwezi kutekeleza jambo hilo nilichoweza kuwashauri ni kwamba waandae mabango ya kumzomea Dk. Slaa,”alisema Peter.

Akizungumzia mikakati hiyo, Mwanasheria wa CHADEMA, Tundu Lissu, alisema siku zote wamekuwa wakiueleza umma juu ya njama zinazofanywa na CCM kupitia kwa watu waliofukuzwa ndani ya CHADEMA kama Habibu Mchange aliyetajwa kuwa nyuma ya uratibu wa mkakati huo kwa kushirikiana na CCM.

Alisema kitendo cha kutaka kulipua helikopta makosa yake yanaelekezwa katika sheria ya kukabiliana na ugaidi na kwamba jeshi la polisi linapaswa kuchukua hatua zinazostahili.

July 10, 2014

Huyu ndiye waziri jangili!!


Apachikwa majina ya utani, buibui au pweza..

Ni kwa umahiri wake kuunganisha majangili..


WAZIRI aliyeukwaa wadhifa huo katika mabadiliko ya mwisho ya Baraza la Mawaziri yaliyofanyika mapema mwaka huu, akiongoza wizara nyeti, amebainika kuratibu mtandao wa ujangili wenye mizizi yake wilayani Manyoni na maeneo mengine mkoani Singida, vyanzo vya uhakika vya habari vimeeleza.
Waziri huyo (jina linahifadhiwa kwa sasa) amekuwa na mawakala maalumu katika maeneo ya karibu na mapori kunakoendeshwa ujangili na mara kwa mara, hufika wilayani Manyoni kuhakiki ufanisi wa mtandao wake huo wa ujangili, huku gazeti hili likielezwa kwamba, taarifa zake ziko ‘mikononi’ mwa vyombo muhimu vya dola nchini.
Kutoka wilayani Manyoni, mkoani Singida, taarifa za ‘kiintelijensia’ zinafichua kwamba mtandao wa waziri huyo unaongozwa na mfanyabiashara (jina linahifadhiwa) wa maduka ya vifaa. Mfanyabiashara huyo ni mkazi wa kitongoji cha Mnyang’ombe mjini Manyoni na kazi zake hizo ndani ya mtandao wa ujangili huzifanya hadi mkoani Tabora.
Inadaiwa kwamba ukaribu kati ya mfanyabiashara huyo na waziri husika umejijengea nguvu zaidi kutokana na umakini wake katika kufanikisha matukio ya ujangili.
Taarifa zinabainisha kwamba mfanyabiashara huyo amekuwa na vijana maalumu ambao kazi yao ni kukusanya pembe za ndovu kutoka katika maeneo ya Itigi, Ilangali lakini katika kituo cha Manyoni, mfanyabiashara huyo hufanya kazi hiyo yeye binafsi.
Vijana hao (majina yanahifadhiwa pamoja namba zao za simu), mmoja anaishi Manyoni akimiliki namba tatu za mtandao wa aina mmoja wa simu za mkononi, mwenzake mwingine ni mwenyeji katika vijiji vinavyopakana na Pori la Akiba Rungwa, maeneo ya Kizigo. Kijana huyo wa Kizigo ndiye mnunuzi wa meno yote ya tembo yanayopatikana maeneo hayo kwa niaba ya mtandao huo.
Mbali na vijana hao wawili, yupo kijana mwingine (jina linahifadhiwa kwa sasa), huyu ni mkazi wa kijiji cha Ilangali, naye akiwa anamiliki namba tatu tofauti za simu za mtandao mmoja wa mawasiliano ya simu za mkononi. Kazi kubwa ya kijana huyu katika mgawanyo wa majukumu ya kijangili ni kuhifadhi silaha sambamba na kununua meno ya tembo kwa ‘wadau’ hapo kijiji cha Ilangali na baada ya kununua meno hayo, mfanyabiashara wa Manyoni hufika kuyachukua.
Mbinu za usafirishaji
Baada ya kazi ya ununuzi na ukusanyaji kukamilika, meno ya tembo yaliyopatikana, husafirishwa kwa njia ya reli ya kati chini ya usimamizi wa mfanyakazi mmoja wa Shirika la Reli Tanzania (jina linahifadhiwa) mwenye makazi yake mjini Morogoro.
Mfanyakazi huyo husimamia usafirishaji wa meno hayo kutoka Tabora hadi Itigi ambako hapo hupokelewa na mfanyabiashara (wa Manyoni) ambaye huyahifadhi hapo Manyoni.
Yakiwa hapo Manyoni, meno hayo huhifadhiwa kwa mmiliki wa mojawapo ya hoteli kubwa na maarufu mjini Manyoni, mwenye asili ya mikoa ya kanda ya kaskazini, ambaye yeye huwasiliana na waziri kwa ajili ya maelekezo zaidi juu ya namna ya kusafirisha meno hayo.
Taarifa za kiuchunguzi zinazidi kubainisha kwamba mara nyingi, waziri husika hufika hapo Manyoni kwa ajili ya kuchukua “mzigo” na kila anapokwenda huongozana na mwanamke mmoja, mwenye lafudhi ya watu kutoka mikoa ya kanda ya kaskazini (jina linahifadhiwa).
Mwanamke huyo ndiye hutumiwa kusafirisha meno hayo yaliyokusanywa yakiwamo ya kutoka ‘kituo’ chao cha Puma, mkoani Singida, ili hatimaye kuyafikisha wanakokubaliana yafike.
Waziri huyo anapokuwa Manyoni amekuwa na kawaida ya kuwakusanya washirika wake katika mtandao huo na wote hupata malazi yao katika moja ya hoteli kubwa na maarufu hapo Manyoni.
Wakiwa hapo Manyoni na bosi (waziri) genge hilo la kijangili hujiimarisha kiulinzi kwa kuweka watu wa kulinda hoteli husika na hata kudadisi wageni wengine wanaofika hotelini hapo.
Katika maeneo ya Singinda, mjini Puma, yupo kijana maalumu anayetumiwa na waziri huyo ambaye anatajwa kuwa na undugu wa namna fulani na mteule huyo wa Rais Kikwete. Kijana huyu hutumia namba za mitandao miwili tofauti ya simu za mkononi.
Huyu kazi yake kubwa ni kuwaunganisha wawindaji (wenyewe majangili huita wapigaji) na wakati mwingine hutokea waziri ndiye anayekusanya mzigo. Wakati uchunguzi huu ulipokuwa ukifanyika, kijana huyo alikuwa na meno ya tembo yaliyokuwa yamehifadhiwa eneo la Tinde, mkoani Shinyanga. Hata hivyo, uaminifu wa kijana huyo si mkubwa kwa sababu uchunguzi wetu umebaini wakati mwingine ‘huchota’ mzigo kiasi fulani na kuuza kinyemela bila mtandao kujua.
Kijana huyo, kati ya kazi alizowahi kufanya ni kuwaunganisha baadhi ya vijana na mwindaji kutoka Wilaya ya Igunga (jina na mawasiliano yake yanahifadhiwa). Mwindaji huyo wa Igunga anamiliki bunduki aina ya Rifle (namba inahifadhiwa) na wakati uchunguzi wa gazeti hili ukifanyika, alikuwa na vipande sita vya meno ya tembo ambavyo ni sawa na meno matatu.
Kwa wakati huo tukifanya uchunguzi, waziri husika alitoa maelekezo vijana wake wasimamishe shughuli zao kwa muda.
Huko wilayani Kahama, mkoani Shinyanga, Waziri husika anashirikiana na mtu (jina linahifadhiwa) ambaye anafanya biashara ya ng’ombe kama kinga ya kuficha shughuli zake za ujangili. Mtu huyu ni mnunuzi wa meno ya tembo na hukusanya meno yanayotoka katika mapori ya Moyowosi, Kigosi, Burigi, Biharamulo na Kimisi.
Hivi karibuni, mtu huyo amekuwa akikusanya meno ya tembo yanayotoka Moyowosi na amekuwa na wadau wake ambao ni watumishi wa serikali katika mapori ya Burigi na Biharamulo. Mtu huyo amenunuliwa na waziri husika gari aina ya Rav4, kwa ajili ya kukusanya meno ya tembo maeneo ya vijiji vinavyozunguka mapori hayo.
Katika maeneo ya Ilongelo na Ngamo, mkoani Singida, huko waziri husika anaendesha mtandao wake wa ujangili kwa kushirikiana na tajiri mmoja, mwenye asili ya Mkoa wa Simiyu ambaye naye anao mtandao mkubwa unaowahusisha vigogo kadhaa, akiwamo mmoja wa wabunge aliyepata kupigia kelele kuhusu ufisadi bungeni, zikiwamo fedha za akaunti za Uswisi, mbunge huyu ni mwenyeji wa kanda ya ziwa na ni kijana kwa umri.
Taarifa za kiuchunguzi zinabainisha kwamba meno ya tembo yanayokusanywa maeneo ya Singida, Kahama na Meatu hufikishwa katika kijiji cha Ngamo ambako waziri husika akiwa na mwanamke mmoja mkazi wa moja ya mikoa ya kaskazini ambaye ndiye mwenye jukumu la kusafirisha meno hayo.
Mtandao wa waziri huyo umejipanua zaidi katika operesheni za kijangili, ukihusisha Wilaya ya Babati, mkoani Manyara. Huko Babati, katika kijiji cha Mayoka, kuna tawi la ujangili la waziri huyo.
Msimamizi wa shughuli za kijangili eneo hilo ni mtu (jina linahifadhiwa) ambaye mara kwa mara huwapo Dodoma kila waziri husika anapokuwa huko kwa shughuli za Bunge. Huyu mtu ndiye husimamia ukusanyaji meno ya tembo kutoka maeneo ya Magugu na Mayoka, wakipata meno hayo kutoka katika Hifadhi ya Taifa Tarangire na ushoroba wa Tarangire – Manyara.
Kutokana na umahiri wa kuunganisha mitandao wa kijangili nchi nzima, waziri huyo kwa baadhi ya watu analinganishwa na pweza au buibui kutokana na kunasa na kuunda mtandao mpana. 

Chanzo Gazeti la Raia Mwema


April 12, 2014

Hotuba ya Tundu Lissu iliyokatishwa kwa makusudi na TBC- Sehemu ya Nne!

Mjumbe wa Bunge maalum la Katiba Mhe. Tundu Lissu alipokuwa akitoa Hotuba ya Maoni ya walio wachache kutoka katika Kamati Na. 4 kabla ya Kukatiwa matangazo na Kituo cha matangazo cha TBC 

<<<<<<<<<<<<Sehemu ya nne>>>>>>>>>

IBARA YA 8

Mheshimiwa Mwenyekiti,

Ibara ya 8 ya Rasimu inahusu ‘Ukuu na utii wa Katiba’ na ilizua mjadala mkali sana katika Kamati Namba Nne. Wajumbe walio wengi kwenye Kamati hawakupendekeza marekebisho yoyote katika ibara hiyo. Hata hivyo, wajumbe hao walipiga kura kupinga marekebisho yaliyopendekezwa na wajumbe walio wachache.

Mapendekezo hayo ni kwamba ibara ya 8(1) iongezewe maneno ‘kwa kadri yatakavyohusika na utekelezaji wa mambo ya Muungano.’ Lengo la marekebisho haya ni kuhakikisha kwamba Katiba ya Shirikisho la Jamhuri inakuwa na ukuu katika mambo yote yanayohusu Shirikisho, na Katiba za Nchi Washirika zinakuwa na ukuu katika masuala yote yanayohusu Nchi Washirika ambayo sio mambo ya Shirikisho. Mapendekezo haya yatalinda u-shirikisho wa nchi yetu na mamlaka ya Nchi Washirika katika masuala yasiyo ya Shirikisho.

Mheshimiwa Mwenyekiti,

Mapendekezo haya hayaongezi kitu chochote kipya katika kamusi ya kikatiba ya nchi yetu. Hii ni kwa sababu, hata ibara ya 64(5) ya Katiba ya sasa ya Muungano inayohusu ukuu wa Katiba ya Muungano imeweka wazi kwamba ukuu huo unahusu mambo ya Muungano tu: “Bila ya kuathiri kutumika kwa Katiba ya Zanzibar ... kuhusu mambo yote ya Tanzania Zanzibar yasiyo mambo ya Muungano, Katiba hii itakuwa na nguvu ya sheria katika Jamhuri nzima ya Muungano na endapo sheria nyingine yoyote itakiuka masharti yaliyomo katika Katiba hii, Katiba ndiyo itakuwa na nguvu, na sheria hiyo nyingine, kwa kiasi inachokiuka Katiba, itakuwa batili.”

Ukuu huu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano katika mambo ya Muungano pekee unathibitishwa pia na ibara ya 4 ya Katiba ya Zanzibar inayohusu ukuu wa Katiba ya Zanzibar: “Katiba hii ni Katiba ya Zanzibar na itakuwa na nguvu za kisheria nchini kote na isipokuwa kutokana na kifungu cha 80 ikiwa sheria yoyote inatofautiana na Katiba hii, basi Katiba hii ndiyo itayokuwa na nguvu na sheria hiyo itakuwa batili kwa kiwango kile ambacho kinahitilafiana.”

Mheshimiwa Mwenyekiti,

Kama ambavyo tumeeleza kwa kirefu kuhusu ibara ya 1 ya Rasimu, kwa miaka hamsini ya Muungano wetu, Serikali ya Jamhuri ya Muungano imenyakua mamlaka ya Zanzibar kwa mambo ambayo hayakuwa mambo ya Muungano kwa mujibu wa Hati ya Makubaliano ya Muungano. Hilo limefanyika kwa njia mbali mbali lakini kwa kiasi kikubwa kwa kuongeza orodha ya mambo ya Muungano kwenye Katiba au kwa kutunga sheria za kawaida na kuzifanya kuwa sheria za Muungano.

Endapo mapendekezo ya ibara ya 8 ya Rasimu yataachwa yalivyo bila kurekebishwa, athari yake kubwa itakuwa ni kufuta kabisa haiba ya u-shirikisho (federalism) ambayo imekuwa sehemu ya mfumo wetu wa kikatiba kwa nusu karne. Hakutakuwa tena na tofauti kati ya mambo ya shirikisho na mambo yasiyo ya shirikisho yaliyoko chini ya mamlaka ya Nchi Washirika.

Aidha, itakuwa ni halali kwa mamlaka za shirikisho kuingilia mambo yasiyo ya shirikisho ya Nchi Washirika kwa kisingizio cha ukuu wa Katiba ya Shirikisho. Pendekezo hili litakuwa na madhara makubwa sana kikatiba na kisiasa na litapelekea migogoro isiyoisha baina ya Nchi Washirika na Shirikisho la Jamhuri. Wajumbe walio wachache wa Kamati Namba Nne wanaliomba Bunge lako tukufu kukubali mapendekezo ya marekebisho ya ibara ya 8 ili kulinda federal character ya nchi yetu.

SURA YA SITA

IBARA YA 60

Mheshimiwa Mwenyekiti,

Rasimu ya Katiba Mpya inapendekeza mabadiliko makubwa katika muundo wa Jamhuri ya Muungano katika maeneo mawili. Kwanza, ibara ya 60(1) ya Rasimu inapendekeza “... muundo wa shirikisho lenye serikali tatu ambazo ni Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania; Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar; na Serikali ya Tanzania Bara.”

Pili, Rasimu inapendekeza mabadiliko makubwa katika orodha ya Mambo ya Muungano. Kwa mujibu wa aya za 62(1) na 63 za Rasimu, Serikali ya Jamhuri ya Muungano itakuwa na mamlaka ya utekelezaji kwa mambo yote yaliyoorodheshwa katika Nyongeza ya Katiba kuwa Mambo ya Muungano. Mambo ya Muungano yaliyoorodheshwa katika Nyongeza hiyo ni Katiba na mamlaka ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ulinzi na usalama, uraia na uhamiaji na sarafu na Benki Kuu. Mambo mengine ya Muungano ni mambo ya nje, usajili wa vyama vya siasa na ushuru wa bidhaa na mapato yasiyo ya kodi yatokanayo na mambo ya Muungano. Kwa ujumla, Rasimu inapendekeza kuwa na Mambo ya Muungano saba.

Kama ambavyo tumeonyesha katika Sura ya Kwanza, suala la Mambo ya Muungano limekuwa na utata mkubwa katika miaka hamsini ya Muungano. Sasa Rasimu inapendekeza Mambo ya Muungano kuwa saba, na kati ya hayo ni Mambo matano tu – Katiba na mamlaka ya Jamhuri ya Muungano, ulinzi na usalama, uraia, uhamiaji na mambo ya nje - ambayo yalikuwepo kwenye orodha ya mwanzo ya Mambo ya Muungano. Na katika Mambo 11 yaliyoongezwa baada ya Muungano, ni mambo mawili tu – sarafu na Benki Kuu na usajili wa vyama vya siasa – ambayo yamebaki katika Rasimu. Kwa ujumla, Rasimu inapendekeza kuondoa Mambo 16 yaliyopo katika orodha ya sasa ya Mambo ya Muungano na kuongeza jambo moja jipya – ushuru wa bidhaa na mapato yasiyo ya kodi yatokanayo na mambo ya Muungano – katika orodha hiyo.

Mapendekezo ya Rasimu kuhusu Mambo ya Muungano yanaashiria mabadiliko makubwa katika muundo wa sasa wa Muungano, na katika Hati za Makubaliano ya Muungano zilizosainiwa mwaka 1964. Kama tulivyoonesha kuhusu ibara ya 1 ya Rasimu, mapendekezo haya ya ibara ya 60 Rasimu hayawezi kuitwa ‘Mwendelezo wa Hati ya Makubaliano ya Muungano.’

SHIRIKISHO LA SERIKALI TATU

Mapendekezo ya muundo wa shirikisho lenye serikali tatu na Mambo ya Muungano yamezua mjadala mkubwa wa kisiasa na kitaaluma. Katika mhadhara wake juu ya Rasimu ya Kwanza, Profesa Shivji alihoji madai ya aya ya 1(3) ya Rasimu. Kwa mujibu wa Profesa Shivji, “... Hati (ya Makubaliano ya Muungano) iliweka serikali mbili; sasa iweje rasimu inayozungumzia serikali tatu iwe na msingi ambao ulijengeka kwenye serikali mbili?... Katiba iliyojikita kwenye serikali tatu haiwezi, kwa vyovyote vile, ikawa mwendelezo wa Hati (za Makubaliano ya Muungano).”

Kama lilivyo jina la mhadhara wake, hoja hii ya Profesa Shivji ina ‘utatanishi’ mkubwa, kwani kumekuwa na mabishano makubwa na ya kihistoria kuhusu tafsiri halisi ya Makubaliano ya Muungano juu ya muundo wa Muungano. Katika kitabu chake Pan Africanism or Pragmatism?, Profesa Shivji mwenyewe amedai kwamba Rais wa pili wa Zanzibar Aboud Jumbe Mwinyi na wasaidizi wake wa karibu waling’olewa madarakani mwaka 1984 kwa sababu ya kuhoji, pamoja na mambo mengine, muundo wa Muungano wa Serikali Mbili kwa madai kwamba Hati za Makubaliano ya Muungano zilikuwa zimeweka utaratibu wa muundo wa shirikisho lenye Serikali Tatu.

Mheshimiwa Mwenyekiti,

Miaka kumi na saba kabla ya kuchapishwa kitabu hicho, Tume ya Nyalali iliyoteuliwa na Rais Ali Hassan Mwinyi kuchunguza kama Tanzania iendelee kuwa na chama kimoja cha siasa au vyama vingi ilipendekeza muundo wa Shirikisho lenye Serikali tatu. Mwaka mmoja baadaye, mwasisi wa Muungano na Rais wake wa kwanza, Mwalimu Nyerere aliandika yafuatayo kuhusu madai ya Rais Jumbe yaliyopelekea ‘kuchafuka kwa hali ya hewa ya kisiasa’ Zanzibar: “Huko nyuma baadhi ya viongozi wa Zanzibar wapinzani wa Muungano wamewahi kudai tufanye referendum kwa Zanzibar kuhusu Muungano. Tukakataa kwa sababu safi kabisa.”

Katika kitabu hicho hicho, Mwalimu Nyerere alisema yafuatayo juu ya kilichotokea kwenye Bunge la Jamhuri ya Muungano mwaka 1993:

“Tarehe 30 Julai, 1993 wakati mkutano wa bunge la bajeti ukiendelea, zaidi ya wabunge 50 kwa pamoja walitoa taarifa ya kusudio la kuwasilisha hoja Bungeni ambayo inadai (kwamba) kuendelea na mfumo huu wa Muungano usiowaridhisha wananchi wengi wa upande mmoja ni kuhatarisha kuendelea kudumu kwa Muungano.... Hivyo basi wabunge hawa wanaliomba Bunge ... liazimie kwamba Serikali ... ilete Muswada Bungeni kabla ya Februari 1994, kurekebisha katiba ya Jamhuri ya Muungano ili kuwezesha uundaji wa ‘Serikali ya Tanganyika’ ndani ya Muungano....

Tarehe 20 Agosti, 1993 wabunge wahusika waliwasilisha taarifa nyingine ... iliyokuwa inalitaka Bunge ... liazimie kwamba Serikali ... iandae kura ya maoni ambayo itafanyika kabla ya 31 Desemba, 1994 ili kupata maoni ya wananchi wa Tanzania juu ya kuundwa kwa “Serikali ya Tanganyika” ndani ya Muundo wa Muungano....”

Aidha, miaka kumi na moja kabla ya kuchapishwa kwa kitabu cha Profesa Shivji, Tume ya Kissanga iliyoteuliwa na Rais Benjamin Mkapa kuchunguza masuala mbali mbali ya kikatiba, nayo ilipendekeza muundo wa Shirikisho lenye Serikali tatu.

MUUNDO WA SERIKALI MBILI UMESHINDWA!!!

Mapendekezo ya kubadili muundo wa Muungano yaliyotolewa na Tume mbali mbali za kikatiba pamoja na Rasimu yanathibitisha mambo mawili. Kwanza, Muungano umekuwa na migogoro isiyoisha na ambayo haijapatiwa ufumbuzi hadi sasa. Jambo la pili ni kwamba, baada ya karibu nusu karne ya maisha yake, muundo wa Muungano wenye Serikali mbili umeshindwa na hauwezi tena kutatua migogoro ya Muungano.

Sehemu kubwa ya migogoro hiyo inatokana na historia ya kuanzishwa kwake. Kama ambavyo wasomi wa historia ya Muungano wameonyesha, Muungano huu ulianzishwa kwa sababu ya shinikizo la mataifa makubwa ya Magharibi yaliyokuwa na hofu kwamba Mapinduzi ya Zanzibar yangeleta siasa za kijamaa katika pwani ya Afrika Mashariki kwa sababu, mara tu baada ya Mapinduzi hayo, Jamhuri ya Watu wa Zanzibar ilitambuliwa na nchi za kijamaa za wakati huo. Aidha, watawala wa nchi za Afrika Mashariki, na hasa waasisi wa Muungano Mwalimu Nyerere na Sheikh Abeid Amani Karume, walikuwa na hofu ya tawala zao kupinduliwa kutokana na mfano wa Mapinduzi ya Zanzibar.

Sababu zote hizi zilipelekea Muungano kufanywa kwa siri kubwa, na kwa vyovyote vile, bila kupata ridhaa ya wananchi wa Tanganyika au Zanzibar au ya vyombo vyao vya uwakilishi. Kama ambavyo tumekwishaonesha katika maoni haya, sio tu kwamba Baraza la Mapinduzi lililokuwa linatawala Zanzibar wakati huo lilikataa pendekezo la Muungano, bali pia halikutunga sheria ya kuridhia Hati za Makubaliano ya Muungano baada ya Sheikh Karume kuamua kuunganisha Zanzibar na Tanganyika bila ridhaa ya Baraza la Mapinduzi!

Kwa upande wake, Bunge la Tanganyika liliitishwa kwa dharura siku tatu baada ya kusainiwa kwa Hati za Makubaliano ya Muungano na kutakiwa kupitisha Sheria ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar siku hiyo hiyo kwa kutumia hati ya dharura! Sheria hiyo ilipitishwa bila mjadala wowote wa maana na kesho yake, tarehe 26 Aprili, 1964, Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ukazaliwa rasmi! Kwa hiyo, kama ambavyo Profesa Shivji na wasomi wengine wa Muungano wameonyesha, Muungano ulizaliwa bila uhalali wa kisheria wala baraka za kisiasa za wananchi wa nchi hizi mbili.

Sehemu nyingine kubwa ya migogoro ya Muungano imetokana sio kwa sababu ya namna ulivyozaliwa, bali na utekelezaji wa masharti ya Hati za Makubaliano ya Muungano. Hii ni kwa sababu, wakati Muungano umetukuzwa katika majukwaa ya kisiasa, umekuwa ukikiukwa kwa vitendo - hasa hasa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano - wakati wote wa historia yake ya karibu miaka hamsini. Kama tulivyoonesha, mbinu kubwa iliyotumiwa kukiuka masharti ya Hati ya Makubaliano ya Muungano ilikuwa kuongeza Mambo ya Muungano kwenye orodha ya Mambo ya Muungano yaliyokuwa kwenye Hati za Makubaliano ya Muungano zilizosainiwa mwaka 1964.

‘KERO ZA MUUNGANO’ AU ‘MUUNGANO WA KERO’?

Mheshimiwa Mwenyekiti,

Mfano mwingine unaoonyesha kwamba muundo wa Muungano wa Serikali Mbili umeshindwa kutatua matatizo ya Muungano ni kile kinachojulikana katika kamusi ya kisiasa ya nchi yetu kama ‘Kero za Muungano.’ Tangu kung’olewa madarakani kwa Rais Jumbe mwaka 1984, mjadala wowote juu ya ‘Hati ya Kuzaliwa’ ya Muungano – kama Jumbe alivyoziita Hati za Makubaliano ya Muungano wakati akijitetea mbele ya Kikao Maalum cha Halmashauri Kuu ya CCM – imekuwa, kwa maneno ya Jumbe, ‘dhambi.’ Na tangu wakati huo, migogoro inayohusu Mambo ya Muungano imeacha kutaja ‘Hati za Makubaliano ya Muungano’, badala yake migogoro hiyo imefichwa ndani ya lugha ya ‘Kero za Muungano.’

Kinachoitwa ‘kero za Muungano’ kiuhalisia ni migogoro juu ya Mambo mbali mbali ya Muungano kati ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar. Hii inadhihirishwa na ‘Hoja za Muungano’ zilizojadiliwa katika vikao mbali mbali vilivyofanywa kati ya Serikali zote mbili kati ya Oktoba 2012 na Machi 2013: hisa za Serikali ya Mapinduzi Zanzibar zilizokuwa katika Bodi ya Sarafu ya Afrika Mashariki; usajili wa vyombo vya moto; malalamiko ya wafanya biashara wa Zanzibar kutozwa kodi mara mbili; mapendekezo ya Tume ya Pamoja ya Fedha; mgawanyo wa mapato; ushiriki wa Zanzibar katika taasisi za nje; utafutaji na uchimbaji mafuta na gesi asili; ajira kwa watumishi wa Zanzibar katika taasisi za Muungano; uvuvi kwenye ukanda wa uchumi wa bahari kuu; ongezeko la gharama za umeme kutoka TANESCO kwenda ZECO; na ushiriki wa Zanzibar katika Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Katika ‘hoja’ hizi ni ongezeko la gharama za umeme kati ya TANESCO na ZECO pekee ambayo haina uhusiano wowote na masuala ya Muungano. Kwa upande mwingine, hisa za Serikali ya Mapinduzi Zanzibar katika Bodi ya Sarafu ya Afrika Mashariki, wafanya biashara wa Zanzibar kutozwa kodi mara mbili; mapendekezo ya Tume ya Pamoja ya Fedha na mgawanyo wa mapato yana uhusiano wa moja kwa moja na ‘mikopo na biashara za nchi za nje’, ‘kodi ya mapato na ushuru wa forodha’, mambo yanayohusiana na ‘sarafu na fedha’ yaliyoko katika orodha ya Mambo ya Muungano ambayo ni Nyongeza ya Kwanza ya Katiba ya Muungano.

Aidha, ushiriki wa Zanzibar katika taasisi za nje na katika Jumuiya ya Afrika Mashariki ni masuala yenye uhusiano wa moja kwa moja na ‘mambo ya nchi za nje’ kwenye orodha ya Mambo ya Muungano. Vile vile, utafutaji na uchimbaji wa mafuta na gesi asili yanahusiana na ‘maliasili ya mafuta ... na gesi asilia’ katika orodha ya Mambo ya Muungano; wakati uvuvi katika Ukanda wa Uchumi wa Bahari Kuu yanahusiana moja kwa moja na ‘Katiba ya Tanzania’ inayotangaza sehemu ya bahari inayopakana na Tanzania kuwa ni sehemu ya eneo la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Mwisho, ‘hoja’ ya ajira kwa watumishi wa Zanzibar katika taasisi za Muungano iko katika ‘utumishi katika Serikali ya Jamhuri ya Muungano’ kwenye orodha ya Mambo ya Muungano.

UTARATIBU WA KUTATUA MIGOGORO YA MUUNGANO UMESHINDWA!!!

Mheshimiwa Mwenyekiti,

Tumeonyesha jinsi ambavyo ‘Kero za Muungano’ zimekuwa sehemu ya historia yote ya Muungano. Kwa mujibu wa Katiba ya Muungano, kero hizi zinazohusu tafsiri ya masuala ya Muungano zilitakiwa kuamuliwa na Mahakama Maalum ya Katiba iliyoundwa chini ya ibara ya 125 ya Katiba. Idadi ya wajumbe wa Mahakama hiyo haijatajwa lakini ibara ya 127(1) inatamka kwamba wajumbe wake ni “... nusu ya jumla ya wajumbe wote watakaoteuliwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano na nusu nyingine ... watateuliwa na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.” Kwa mujibu wa ibara ya 128(2) ya Katiba, akidi ya kikao cha Mahakama hiyo ni wajumbe wote; na “kila suala linalohitaji uamuzi ... litaamuliwa kwa kufuata kauli ya theluthi mbili ya wajumbe kutoka Tanzania Bara na theluthi mbili ya wajumbe kutoka Tanzania Zanzibar.” (ibara ya 128(3) Na kwa mujibu wa ibara ya 126(3), uamuzi wa Mahakama Maalum ya Katiba “... utakuwa ndio wa mwisho (na) hakutakuwa na haki ya kukata rufaa popote.”

Licha ya Katiba ya Muungano kuweka utaratibu huu wa kutatua migogoro ya tafsiri ya Katiba kuhusu masuala ya Muungano, Mahakama Maalum ya Katiba haijawahi kuitishwa kusikiliza migogoro mingi kuhusu tafsiri ya Katiba kuhusu masuala ya Muungano. Jaribio pekee la kukiitisha chombo hiki cha kikatiba kutatua migogoro hiyo lilizimwa mwaka 1984 wakati aliyekuwa Rais wa Zanzibar Aboud Jumbe, Waziri Kiongozi Ramadhani Haji Faki na Mwanasheria Mkuu Bashir Kwaw Swanzy walipong’olewa madarakani kwa kile kilichoitwa ‘kuchafuka kwa hali ya hewa ya kisiasa’ Zanzibar. Profesa Shivji yupo sahihi anaposema - katika Pan Africanism or Pragmatism? – kwamba ‘pengine Mahakama hiyo haikupaswa kufanya kazi’!

Badala ya kutatua matatizo ya Muungano kwa njia zilizowekwa kikatiba, Serikali ya Muungano na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar zimeanzisha taratibu za kirasimu zilizoko nje kabisa ya mfumo wa kikatiba wa Muungano. Ndio maana Taarifa ya Utekelezaji Bajeti Mwaka wa Fedha 2012/13: Kipindi cha 01 Julai hadi 31 Desemba, 2012, iliyowasilishwa Bungeni tarehe 23 Januari mwaka huu inaelezea uratibu wa vikao vitatu vya Sekretarieti ya Kamati ya Pamoja ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, iliyoundwa mwaka 2006 ili “... kushughulikia changamoto zinazojitokeza katika utekelezaji wa Mambo ya Muungano....”

Vile vile, kwa mujibu wa Taarifa hiyo, vikao vya Kamati ya Makatibu Wakuu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano na wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na mawaziri wa Serikali hizo vilivyokaa kati ya tareje 20 Desemba 2012 na 13 Januari 2013 vilikutana kujadili ‘Hoja za Muungano.’ Haihitaji msisitizo kusema kwamba vikao hivyo vyote havitambuliwi kikatiba. Katika mazingira haya, ni halali kuuliza swali kama pande zote mbili za Muungano zinataka kuendelea na Muungano kabla hata ya kujadili muundo wake.

MUUNGANO AU UHURU???

Mheshimiwa Mwenyekiti,

Katika mhadhara wake wa kuaga Kigoda cha Mwalimu, Profesa Shivji amehitimisha uchambuzi wake wa Rasimu kwa kusema kwamba muundo wa Muungano unaopendekezwa “... ni tegemezi na ... ni dhaifu kwa sababu umejengwa juu ya mchanga wa dhamira na nia nzuri badala ya msingi wa mawe ya nguvu za kikatiba zilizowekwa na wananchi wenyewe. Ni kama kwamba suala la Muungano ni (la) ujirani mwema badala ya umoja wa nchi.” Kwingineko katika mhadhara huo, mwanazuoni huyu maarufu ‘amediriki kusema’ kwamba “muundo wenyewe wa serikali tatu uliopendekezwa (na Rasimu) ni compromise kati ya wale waliosimamia serikali mbili na wale waliopigania muungano wa mkataba, kwa maneno sahihi, kuuvunja muungano.”

Ijapokuwa hajasema wazi wazi, Profesa Shivji anaonyesha kupendelea kwamba muundo wa sasa wa Muungano wa serikali mbili ni bora zaidi na hauna budi kuendelea. Kwa maneno yake, “... compromise inazaa uamuzi legelege. Compromise juu ya muundo ... imezaa muundo wa muungano legelege. Kuna maeneo mengi ... yatazaa migogoro ambayo hatimaye inaweza kuuvunja Muungano. Kero za Muungano zitaendelea, safari hii kutoka pande zote mbili.”

Si sahihi kupuuza hoja na kauli za mwanazuoni huyu maarufu. Hata hivyo, ni muhimu kuhoji uhalali wake kwa kuangalia historia halisi ya Muungano wetu. Kwanza kabisa, kama ambavyo Profesa Shivji mwenyewe amedhihirisha katika maandishi yake ya zaidi ya miaka ishirini, Muungano huu haujawahi kuwa Muungano wa watu wa Tanganyika na Zanzibar, bali ulikuwa na umeendelea kuwa Muungano wa watawala kwa maslahi ya watawala wa ndani ya nchi yetu na wa nchi za kibeberu!

Pili, Muungano huu wa watawala haujawahi kuheshimiwa na watawala wenyewe kwa miaka yote ya uwepo wake, kama ambavyo historia ya Mambo ya Muungano na utaratibu wa kutatua migogoro yake inavyothibitisha.

Tatu, kwa kuangalia mwelekeo wa siasa za sasa za kikatiba za Zanzibar, ni wazi kwamba wananchi wa Zanzibar wanapendelea uhuru kuliko kuendelea na Muungano huu. Profesa Shivji anathibitisha hili kwa kauli yake kwamba “Wazanzibari kwa muda mrefu tu wamedai haki yao ya kujiamulia mambo yao wenyewe.” Nne, kwa sababu ya kuwa Muungano wa watawala badala ya kuwa Muungano wa wananchi; kwa sababu ya kutoheshimiwa na watawala hao; na kwa sababu ya mwelekeo wa siasa za Zanzibar za sasa, ‘Kero za Muungano’ haziwezi kutatuliwa kwa kutumia muundo wa sasa wa Serikali mbili. Compromise ya serikali tatu, katika mazingira haya, ni njia pekee iliyobaki ya kuwa na Muungano, hata kama ni muundo dhaifu na legelege kama anavyolalamika Profesa Shivji! Nje ya serikali tatu ni uhuru kamili wa ‘Washirika wa Muungano’ na kuzaliwa upya kwa Jamhuri ya Tanganyika na Jamhuri ya Watu wa Zanzibar.

BILA MUUNGANO KUWEPO NI VITA???

Katika hitimisho la mhadhara wake, Profesa Shivji ametoa ‘picha ya kiama’ (doomsday scenario) endapo Muungano utavunjika kwa sababu ya kukubaliwa muundo wa shirikisho lenye serikali tatu: “Muungano ukivunjika hakuna mwananchi atakayenusurika, awe wa Tanganyika au wa Zanzibar.”

Kwingineko katika hitimisho la mhadhara huo, msomi huyu maarufu anaendeleza dhana yake ya ‘serikali tatu ni kiama’: “Suala la Muungano sio letu tu. Kuna nchi za kibeberu zina maslahi makubwa ya rasilmali pamoja na ya kijeshi katika eneo letu, hasa Bahari ya Hindi. Tukibeza mambo haya nyeti kwa sababu tu ya uchu wa madaraka ya viongozi wachache, tutawapeleka watu wetu kwenye hali mbaya.” Ili kutilia nguvu hoja yake kwamba kuvunjika kwa Muungano kutaleta vita, Profesa Shivji ametumia mifano ya vita na migogoro ya mipaka iliyotokea baada Urusi ya Kisovieti, Shirikisho la Yugoslavia na, katika Afrika, Sudan kuvunjika.

Hoja hii ya Profesa Shivji na mifano yake inastahili majibu. Kwanza, mifano aliyoitumia ni ya upande mmoja na ya kiitikadi zaidi. Hii ni kwa sababu kuna mifano ya nchi zilizovunja muungano wao bila kuwepo vita au migogoro ya mipaka. Jamhuri za Czech na Slovakia zilizotokana na kuvunjika kwa Jamhuri ya zamani ya Czechoslovakia ni mfano mzuri. Haiyumkini kwamba Profesa Shivji anaufahamu mfano huu vizuri.

Pili, kuna nchi nyingi ambazo zimepigana vita ya wenyewe kwa wenyewe kwa muda mrefu kwa sababu ya kulazimisha muungano usiokubaliwa na upande mmoja au mwingine katika umoja huo. Ethiopia na Eritrea ni mfano mmojawapo. Mwaka 1952 Ethiopia ilisaini makubaliano kati yake na Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa yaliyoifanya Eritrea sehemu ya Shirikisho la Ethiopia na hivyo kumaliza utawala wa Uingereza katika koloni hilo la zamani la Italia.

Hata hivyo, tarehe 14 Novemba, 1962, Mfalme Haile Selassie I wa Ethiopia alivunja makubaliano hayo kwa nguvu na kuifanya Eritrea kuwa sehemu ya Himaya yake. Vita vya ukombozi vilivyosababishwa na kitendo hicho vilichukua karibu miaka thelathini hadi Ethiopia iliposhindwa mwaka 1991 na Eritrea kujipatia uhuru kamili. Vile vile Profesa Shivji anaufahamu mfano huu vizuri sana, kwa sababu alikuwa mmoja wa wanazuoni wengi waliounga mkono wa Chama cha Ukombozi wa Watu wa Eritrea (Eritrean People’s Liberation Front - EPLF), kilichoongoza mapambano ya uhuru wa nchi hiyo.

Sudan ya zamani ni mfano mwingine wa vita vilivyosababishwa na kulazimisha muungano usiotakiwa na upande mmoja. Mnamo Februari, 1953, Uingereza na Misri zilizokuwa zinatawala Sudan ya Kusini na ya Kaskazini kama maeneo tofauti kwa utaratibu wa Condominium zilikubaliana kukabidhi uhuru kwa shirikisho la Sudan ifikapo tarehe 1 Januari, 1956. Hata hivyo, kabla ya tarehe hiyo kufika, viongozi wa Sudan Kaskazini walikiuka makubaliano ya kuunda serikali ya shirikisho. Matokeo yake ni kwamba wananchi wa Sudan Kusini waliasi na kuanzisha kile kinachojulikana katika historia kama Vita ya Kwanza ya Wenyewe kwa Wenyewe ya Sudan (First Sudanese Civil War au Anyanya I Rebellion). Vita hiyo ilianza Agosti, 1955 na ilimalizika kwa kusainiwa kwa Makubaliano ya Amani ya Addis Ababa ya mwaka 1972. Makubaliano hayo yalirudisha mfumo wa Shirikisho ulioipa Sudan Kusini mamlaka makubwa ya utawala wa ndani. Makubaliano ya Addis Ababa hayakudumu muda mrefu kwa sababu Serikali Kuu ya Sudan iliyahujumu. Matokeo yake, mwaka 1978 Maasi ya Anyanya II yalianza tena. Makubaliano ya Addis Ababa yalivunjika kabisa mwaka 1983 na Vita ya Pili ya Wenyewe kwa Wenyewe ya Sudan (Second Sudanese Civil War) ilianza mwaka 1983 hadi ilipoisha baada ya kusainiwa kwa Mkataba wa Amani wa Nairobi wa tarehe 9 Januari, 2005.

Chini ya Mkataba wa Amani wa Nairobi, Sudan Kusini ilijitawala kwa masuala ya ndani kwa miaka sita hadi 2011 wananchi wa Sudan Kusini walipopiga kura ya maoni na kuamua kujitenga na Sudan ya Kaskazini. Tarehe 9 Julai, 2011, Jamhuri ya Sudan Kusini ilizaliwa kama nchi huru. Ni kweli kwamba bado kuna mgogoro wa mpaka kati ya Jamhuri hiyo mpya na Sudan Kaskazini. Hata hivyo, mgogoro huo hauwezi kulinganishwa na vita vya wenyewe kwa wenyewe iliyochukua miaka hamsini kuanzia 1955 hadi 2005! Hapana shaka kwamba Profesa Shivji anaifahamu historia hii vema, kwani zama za ujana wake alisoma katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam pamoja na Dk. John Garang, mwasisi wa Chama/Jeshi la Ukombozi wa Watu wa Sudan (Sudanese People’s Liberation Movement/Army – SPLM/A).

Tatu, zipo nchi ambazo zinaendelea kuwa na vita kwa sababu ya kulazimisha umoja ambao upande mmoja unaukataa. India (mgogoro wa Jimbo la Kashmir), Hispania (Jimbo la Basque) na Angola (Jimbo la Cabinda) ni mifano mizuri. Ni vigumu kuamini kwamba Profesa Shivji hafahamu mifano ya nchi hizi pia. Ni wazi, kwa hiyo, kwamba hoja serikali tatu = kuvunja Muungano = vita na maangamizi ni hoja yenye lengo la kutisha wananchi ili wasiweze kujadili masuala yote yanayohusu Muungano ikiwamo kuachana nao.

Na nne, hoja ya Profesa Shivji kwamba wanaodai kuwe na Muungano wa shirikisho lenye serikali tatu ni ‘viongozi wachache’ wenye ‘uchu wa madaraka’ ni ya kusikitisha sana. Hii ni sawa sawa na kuwaita Rais Aboud Jumbe na wasaidizi wake, au wajumbe wa Tume ya Nyalali, au ya Kissanga au hata ya sasa ya Warioba, au Wabunge wa G55, waroho wa madaraka kwa sababu tu hawakukubaliana na mfumo wa serikali mbili ambao Shivji mwenyewe amekiri mara nyingi umeshindwa kutatua matatizo na ‘Kero za Muungano’!

SERIKALI TATU NI GHARAMA KUBWA!!!

Mheshimiwa Mwenyekiti,

Tangu kuchapishwa kwa Rasimu, kumejitokeza kauli kwamba kuwa na muundo wa Muungano wenye serikali tatu itakuwa ni gharama kubwa kwa nchi maskini kama ya kwetu. Viongozi na makada wa CCM wameidaka hoja hii ya gharama za Muungano kama ndio turufu yao ya kuendelea na muundo wa sasa wa Muungano wa Serikali mbili. Katika Ufafanuzi wake, CCM imedai kwamba “gharama za uendeshaji wa Serikali zilizopo hivi sasa ni kubwa. Kuwepo kwa Serikali ya tatu kutakuwa ni gharama ya ziada na hivyo kuwa mzigo mkubwa kwa wananchi.”

Kwa upande wake, Profesa Shivji amezungumzia suala hili kama ifuatavyo: “Kwa upande wa gharama, ni wazi kwamba kuendesha serikali ya muungano kutakuwa na gharama kubwa. Kazi inayofanywa na taasisi moja au idara moja katika muundo uliopo sasa itahitaji taasisi mbili. Kwa mfano, badala ya kuwa na Tume moja ya uchaguzi, sasa kutakuwa na tume mbili, moja ya Muungano na nyingine ya Bara. (Ukiongeza ya Zanzibar kutakuwa na Tume tatu za uchaguzi. Na hivyo hivyo kuhusu tume nyingine. Ukiangalia juu juu tu, licha ya taasisi na idara za kawaida katika serikali, kuna tume karibu nane na mabaraza mawili yenye wajumbe wazito ambao bila shaka watakuwa na mishahara minono na marupurupu poa. Wananchi wamekwishaanza kuonyesha wasiwasi wao kwa kuwaongezea mzigo wa kubeba serikali kamili nyingine, zaidi ya hizi mbili tulizonazo.”

Mheshimiwa Mwenyekiti,

Hoja hii ya gharama za kuendesha serikali tatu ni red herring, yaani ina lengo la kuwatoa wananchi kwenye mjadala wa msingi juu ya kushindwa kwa muundo wa sasa wa Muungano kutatua ‘Kero za Muungano’, kwa kuwaaminisha kwamba muundo wa sasa una gharama nafuu zaidi kuliko muundo wa serikali tatu. Kwanza, kwa kadri ya ufahamu wetu, hadi sasa hakuna mtu yeyote aliyefanya uchambuzi wa ulinganifu wa gharama za kuendesha serikali – iwe moja, mbili au tatu – katika nchi yetu. Hata Ufafanuzi wa CCM uko kimya juu ya jambo hili. Kwa sababu hiyo, hakuna ushahidi wowote wa kuthibitisha kwamba kuendesha serikali tatu ni ghali zaidi kuliko kuendesha serikali mbili. Kwa vyovyote vile, kama suala la gharama za kuendeshea serikali ndio jambo muhimu zaidi katika kuamua muundo wa Muungano, kwa nini tusiwe na serikali moja tu, kuliko mbili za sasa au tatu zinazopendekezwa na Rasimu?

Pili, na muhimu zaidi, kama tukichukua mapendekezo ya Mambo ya Muungano kama kigezo cha kupima ukubwa wa serikali – na kwa hiyo gharama za kuiendeshea – basi gharama za serikali ya Muungano zinaweza kuwa ndogo sana. Hii ni kwa sababu, haiwezekani – kwa mambo saba ya Muungano yanayopendekezwa na Rasimu – kuwa na serikali kubwa ya Muungano. Kwa Mambo hayo ya Muungano, hakutakuwa na zaidi ya wizara nne za Serikali ya Muungano. Hivyo, kwa mfano, kutakuwa na wizara ya katiba na sheria itakayoshughulikia masuala ya Katiba na mamlaka ya Jamhuri ya Muungano; wizara ya ulinzi itakayokuwa na majukumu ya ulinzi na usalama wa Jamhuri ya Muungano; wizara ya fedha itakayoshughulikia masuala ya sarafu na benki kuu, na ushuru wa bidhaa na mapato yasiyo ya kodi yatokanayo na Mambo ya Muungano; na wizara ya mambo ya nje. Masuala yaliyobaki, yaani uraia na uhamiaji na usajili wa vyama vya siasa hayastahili kuwa na wizara zinazojitegemea kwa hiyo yanaweza kuwekwa chini ya mojawapo ya wizara zilizotajwa hapo juu.

Ibara ya 98(2) ya Rasimu inapendekeza ukomo wa ukubwa wa Baraza la Mawaziri la Jamhuri ya Muungano kuwa mawaziri wasiozidi kumi na tano. Kwa upande mwingine, ibara ya 98(3) inaelekeza kwamba “Serikali ya Jamhuri ya Muungano itakuwa na Wizara kwa kuzingatia mamlaka ya Serikali kwa mujibu wa Katiba hii.” Sasa kama mamlaka ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano yako kwenye mambo saba ya Muungano kwa mujibu wa Rasimu hii, je, hao mawaziri wasiozidi kumi na tano watatoka wapi na watatimiza majukumu gani? Ni wazi kabisa kwamba mapendekezo ya ibara ya 98(2) yanakinzana na matakwa ya ibara za 62(1) na 63 zinazohusu mamlaka ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano juu ya Mambo ya Muungano.

Kwa mtazamo huo huo wa ibara ya 98(3) na orodha ya Mambo ya Muungano kama kipimo cha ukubwa wa Serikali ya Muungano, taasisi nyingine zinazopendekezwa na Rasimu haziwezi kuwa kubwa sana na nyingine hazitakuwepo kabisa. Kwa mfano, Katibu Mkuu Kiongozi na Makatibu Wakuu wanaopendekezwa katika ibara za 105 na 106 za Rasimu hawawezi kuzidi idadi ya Wizara nne zilizotajwa hapo juu zitakazoshughulikia Mambo ya Muungano. Kwa maana hiyo, kwa kuzingatia idadi ya Makatibu Wakuu wenyewe, Kamati Maalumu ya Makatibu Wakuu inayoelezwa katika ibara ya 107; na Sekretarieti ya Baraza la Mawaziri inayotajwa katika ibara ya 108, hazina maana wala umuhimu wowote kikatiba.

Au tuchukue mapendekezo yanayohusu Bunge la Jamhuri ya Muungano. Kwa mujibu wa ibara ya 105(4) ya Rasimu, kila Jimbo la Uchaguzi litawakilishwa na wabunge wawili kwa kuzingatia jinsia zao. Ibara ya 113(2)(a) inabainisha ‘Jimbo la Uchaguzi’ kuwa ni kila mkoa kwa upande wa Tanzania Bara na wilaya kwa upande wa Zanzibar. Aidha, kwa mujibu wa ibara ya 113(2)(b), kutakuwa na wabunge watano wa kuteuliwa na Rais kuwakilisha watu wenye ulemavu. Tukichukua idadi ya mikoa ishirini na tano ya Tanzania Bara na wilaya 10 za Zanzibar kwa sasa, Bunge la Jamhuri ya Muungano litakuwa na wabunge 75.

Kwa mapendekezo ya muundo wa serikali tatu, Bunge la Zanzibar litakuwa na Wabunge hamsini wa majimbo ya sasa ya uchaguzi; wakati bunge la Tanganyika litakuwa na wabunge 189 wa majimbo ya uchaguzi ya sasa. Kwa maana hiyo, muundo wa Muungano wa serikali tatu utakuwa na mabunge matatu yenye jumla ya wabunge 314.

Kwa kulinganisha, Bunge la Jamhuri ya Muungano la sasa lina idadi ya wabunge 239 wa majimbo ya uchaguzi – 189 wa majimbo ya uchaguzi ya Tanzania Bara na hamsini ya Zanzibar. Vile vile, kuna wabunge 102 wa Viti Maalumu, 10 wa kuteuliwa na Rais na watano wanaowakilisha Baraza la wawakilishi Zanzibar na Mwanasheria Mkuu, kwa idadi ya jumla ya wabunge 357.

Kwa upande wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar, kuna wawakilishi hamsini wanaowakilisha majimbo ya uchaguzi, kumi wa kuteuliwa na Rais wa Zanzibar, ishirini wa Viti Maalum na Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar, kufanya jumla ya wawakilishi themanini na moja. Kwa maana hiyo, kwa muundo wa sasa wa Muungano, mabunge mawili tuliyonayo yana idadi ya wabunge 438. Idadi hiyo ni kubwa kuliko idadi ya wabunge wa mabunge matatu yatakayokuwepo chini ya muundo wa serikali tatu kwa wabunge 124!

Na sio Bunge ambalo linaweza kuwa na gharama ndogo kuliko gharama za sasa. Taasisi za Muungano zinazopendekezwa kama vile Tume ya Uhusiano na Uratibu wa Serikali (ibara ya 109); Tume ya Utumishi wa Mahakama (ibara ya 180); na Tume ya Utumishi wa Umma (ibara ya 186) haziwezi kuwa kubwa sana kwa kuzingatia ukubwa wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano kwa mujibu wa Rasimu.

Aidha, uwepo wa taasisi nyingine kama vile Tume ya Maadili ya Uongozi na Uwajibikaji (ibara ya 200) na Tume ya Haki za Binadamu (ibara ya 208) unakinzana na matakwa ya aya za 62(1) na 63 za Rasimu na kwa hiyo haziwezi kugharimiwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano!

Vile vile, majukumu ya utekelezaji wa Mambo mengine ya Muungano kama uchaguzi na usajili wa vyama vya siasa yanaweza kutekelezwa na taasisi husika za Washirika wa Muungano kwa makubaliano na masharti maalumu chini ya aya ya 59(3) ya Rasimu. Hii nayo itapunguza gharama za kuendesha Serikali ya Jamhuri ya Muungano.

Ni wazi – kwa mtazamo huu – kwamba gharama za kuendeshea muundo wa shirikisho lenye serikali tatu zinaweza kuwa hata ndogo kuliko gharama za kuendeshea muundo wa Muungano wa serikali mbili za sasa.

FAIDA ZA MUUNGANO NI KWA WAZANZIBARI PEKE YAO?

Mheshimiwa Mwenyekiti,

Pendekezo la Rasimu kuhusu muundo wa Serikali tatu limeleta hoja juu ya faida za Muungano kwa kila upande wa Washirika wa Muungano. Hivyo, kwa mfano, katika Ufafanuzi wake CCM imedai kwamba pendekezo hili litaleta “... urasimu na utata wa kisheria katika umiliki na uendeshaji wa shughuli za kiuchumi na kijamii.” CCM inafafanua zaidi juu ya jambo hili: “Urasimu wa kibiashara na umilikaji ardhi utaongezeka kwa sababu biashara, ardhi na umilikaji wa mali wa aina nyingine si mambo ya Muungano.”

Kwingineko katika Ufafanuzi wake, CCM inadhihirisha kwamba msimamo wake juu ya muundo wa Serikali tatu unatokana na hofu ya athari za muundo huo kwa maslahi ya kiuchumi ya Wazanzibari walioko, au wenye vitega uchumi, Tanzania Bara. Hivyo basi, “muundo wa Serikali mbili una urasimu mdogo wa kisheria na hivyo kutoa fursa nyingi za kiuchumi na kijamii hususan kwa Wazanzibari ambao eneo lao la ardhi ni dogo wakati idadi ya wakaazi inaongezeka mwaka hadi mwaka.” Aidha, kwa mujibu wa CCM, “muundo uliopo unawawezesha Wazanzibari kumiliki ardhi na rasilmali nyingine zilizoko Tanzania Bara kama raia wa Tanzania, ingawaje ardhi na rasilmali nyingine za kiuchumi si masuala ya Muungano.”

Mheshimiwa Mwenyekiti,

Inajulikana kwamba, kwa mujibu wa sheria za Zanzibar, Watanzania Bara hawana haki ya kumiliki ardhi Zanzibar, licha ya kuwa raia wa Tanzania. Aidha, licha ya kuwa raia wa Tanzania, Watanzania Bara wanaoajiriwa katika sekta binafsi Zanzibar wanatakiwa kutimiza masharti ya vibali vya ajira sawa na raia yeyote wa nchi za kigeni. Yote haya ni nje ya ukweli kwamba Watanzania Bara hawawezi kuajiriwa katika taasisi yoyote ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, tofauti na Wazanzibari ambao wanaajiriwa na taasisi za Serikali ya Jamhuri ya Muungano hata kwa mambo yasiyokuwa ya Muungano.

Vile vile, yote haya ni nje ya ukweli kwamba wakati Wazanzibari wanaweza kikatiba kushiriki shughuli za kisiasa na kiutawala Tanzania Bara hata kwa mambo yasiyokuwa ya Muungano, Watanzania Bara hawana uwezo huo. Hivyo basi, kwa utaratibu huu, Wabunge wa Zanzibar katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wanashiriki katika mijadala ya mambo yasiyo ya Muungano ya Tanzania Bara, Wazanzibari wanashikilia nafasi za juu za kisiasa kama vile uwaziri katika wizara zisizokuwa za Muungano na Baraza la Wawakilishi Zanzibar lina uwakilishi maalum katika Bunge la Jamhuri ya Muungano. Wananchi wa Tanzania Bara hawana haki ya kushiriki katika mambo haya kwa upande wa Zanzibar.

Mheshimiwa Mwenyekiti,

Upinzani wa CCM dhidi ya pendekezo la Rasimu juu ya muundo wa Serikali tatu unadhihirisha ushawishi mkubwa wa Zanzibar katika siasa za ndani ya CCM, hasa hasa katika zama hizi za vyama vingi na vita za makundi mbali mbali ndani ya chama hicho. Katika mazingira haya, mtu yeyote anayetaka kupitishwa kuwa mgombea urais kwa kupitia CCM anakuwa anahitaji kura za CCM Zanzibar ili kushinda katika kinyang’anyiro hicho.

Kwa kauli ya Mwalimu Nyerere katika kitabu chake Uongozi Wetu na Hatima ya Tanzania: “Sababu moja kubwa iliyofanya viongozi wetu wasitake kuwaudhi ‘Wazanzibari’ ... ni umuhimu wa kura za Zanzibar katika kumteua mwanachama wa CCM kuwa Mgombea wa Urais wa Jamhuri ya Muungano. Kwa kiongozi yeyote anayeliona jambo hilo kuwa ni muhimu kupita mengine yote, kuwaudhi ‘Wazanzibari’ ni dhambi ambayo haina budi iepukwe kwa kila njia.” Hofu hii ya ‘kuwaudhi’ Wazanzibari ndio imepelekea CCM kutaka kulinda maslahi ya kiuchumi ya Wazanzibari kwa kukataa muundo wa Serikali tatu.