Showing posts with label Lifestyle. Show all posts
Showing posts with label Lifestyle. Show all posts
September 4, 2014
Tatizo la Unene Uliopitiliza (Obesity) na kinga yake!
Tatizo hili la unene uliopitiliza kuliko inavyohitajika kiafya huwa linaletwa na kuongezeka kwa kiwango cha mafuta mwilini. Njia rahisi na inayokubalika ya kuweza kugundua kama mtu ni mnene kupita kiasi (obese) inafahamika kama kipimo cha Body Mass Index (BMI). Vipimo hivi vya BMI ndio vinaweza kukujulisha kama unene ulionao unastahili kulingana na umri, urefu na uzito wako.
Vipimo hivi ni kama ifuatavyo:
Jinsi ya kupima BMI yako
Kanuni ya BMI hutumia uzito wa mtu pamoja na urefu wake. Uzito wa mtu hupimwa katika kilograms (kg) na urefu wake katika mita (m) au sentimita (cm). Ikumbukwe pia kuwa mita moja ni sawa na sentimita 100 na mita² = mita x mita.
| Category | BMI range – kg/m2 |
| Emaciation | less than 14.9 |
| Underweight | from 15 to 18.4 |
| Normal | from 18.5 to 22.9 |
| Overweight | from 23 to 27.5 |
| Obese | from 27.6 to 40 |
| Morbidly Obese | greater than 40 |
- Vyakula vya mafuta - Ulaji wa vyakula venye mafuta mengi au calories nyingi.
- Kutofanya mazoezi - Wale wasiofanya mazoezi mara kwa mara huwa wanene tofauti na wale wanaofanya mazoezi.
- Kurithi viashiria vya asili (genes) - Viashiria hivi vinaweza kuwa moja ya vichocheo vya kuongeza uzito kwani ndivyo huamua wapi mafuta huhifadhiwa mwilini na kwa kiwango gani. Lakini haimanishi kuwa mtu akiwa navyo basi ndio atakumbwa na tatizo hili.
- Umri - Watu wengi huongezeka uzito au hunenepa kadri umri unavyoongezeka kwa sababu wanakuwa hawajishughulishi sana (less active) na huwa wanapungua maumbile ya miili yao (muscles mass)
- Matatizo ya kisaikolojia - Wakati mwengine watu wenye matatizo ya kisaikolojia au msongo wa mawazo (stress) huwa na tabia ya kula sana, matokeo yake ni kunenepa.
- Dawa - Baadhi ya dawa zenye madhara ya kuongeza unene ni kama corticosteroids, blood pressure medications, tricyclic medications na kadhalika.
- Matatizo ya afya - Baadhi ya magonjwa yanachangia kuongezeka kwa uzito au kenenepa kama cushings syndrome, hypothyroidism, osteoarthritis na kadhalika
- Kukua kwa uchumi wa nchi - Wananchi wengi wanaoishi kwenye nchi zilizoendelea au wenye kipato kikubwa ndio wanaopata tatizo hili kutokana na kuishi mfumo wa maisha ya kivivu na hali ya kutokufanya mazoezi (sedentary lifestyle).
- Historia ya kuongezeka uzito uliopitiliza kwenye familia nayo yaweza kuhatarisha mtu kupata tatizo hili. Aidha, si jambo la kushangaza kuona karibu familia nzima au wengi wa wanafamilia kuwa wanene kupitiliza.
- Kutojishughulisha na chochote (inactive).
- Kupenda kula sana kuliko kawaida (overeating).
- Kula vyakula vya mafuta mengi
- Kutumia dawa zenye madhara ya kuongeza uzito uliopitiliza.
- Kuwa na ugonjwa wa vichocheo mwilini (hormonal disorders) kama cushingsyndrome, hypothyroidism.
- Kuwa na msongo wa mawazo au kuathirika kisaikolojia.
- Kisukari
- Shinikizo la damu (hypertension)
- Kiharusi (Stroke)
- Magonjwa ya moyo
- Tatizo la kutopumua vizuri wakati mtu yupo usingizini (Sleep apnea)
- Vijiwe katika mfuko wa nyongo (Gallstones)
- Kiwango cha juu cha lijamu kwenye damu(cholesterol ikiwemo triglycerides)
- Ugonjwa wa mifupa kama yabisi (osteoarthritis).
- Saratani ya matiti
- Saratani ya tezi dume (prostate cancer)
- Saratani ya utumbo mpana pamoja na maeneo ya haja kubwa (Colorectal cancer)
- Matatizo ya mzunguko na mishipa ya damu kama vile kuvimba kwa vena za miguuni(varicose veins)
- Mabadiliko ya tabia - Hii inahusisha muhusika kupunguza kiwango cha chakula anachokula lakini kiwe chenye virutubisho vyote muhimu vya afya na kuongeza kiwango cha ufanyaji mazoezi.
- Mazoezi - Mazoezi husaidia kupunguza uzito hasa kipindi cha miezi sita ya mwanzo na hutunza uzito uliokusudiwa kwa muda mrefu. Pia hupunguza mafuta ya mwilini, huongeza ufanisi wa moyo, hupunguza tatizo la shinikizo la damu (hypertension), na kuweka sukari katika kiwango kinachohitajika mwilini.
- Dawa - Zipo dawa nyingi za kupunguza uzito lakini ikumbukwe ya kwamba hakuna tiba ya tatizo hili na dawa hizi zina madhara mengi kama kuongeza shinikizo la damu (hypertension), matatizo ya moyo, kuharisha,msongo wa mawazo (depression) na mengineyo.
- Chakula - Msingi wa kupunguza uzito au unene ni kujua ni kiwango gani cha calories mwili wako unahitaji kwa siku ili uwe unakula chakula ambacho hakitazidisha au kupunguza kiwango cha calories unazohitaji kwa siku. Mlo mzuri ni ule ulio na matunda kwa wingi, mboga za majani, nafaka ambazo hazijakobolewa, mafuta kidogo (less saturated fat). Vyakula vengine ni kama mayai, nyama isiokuwa ya mafuta (lean meat), samaki, kuku na vingineyo.
- Tiba ya upasuaji - Kuna aina nyingi za upasuaji ambao unasaidia kupunguza uzito aina hizi ni kama gastric banding, gastric bypass (Roux-en-Y-procedure), liposuction. Kabla ya kufanyiwa upasuaji, muhusika atahitaji kupimwa kisaikolojia (psychological testing) na kupewa ushauri nasaha kwani tiba hii pia ina madhara yake.
- Kisukari cha mimba (Gestatitional diabetes) - kisukari hiki kinatokea wakati wa ujauzito na hupotea baada ya kujifungua mtoto.
- Shinikizo la damu (hypertension)
- Shinikizo la damu wakati wa ujauzito pamoja na kifafa cha mimba (pre-eclampsia & eclampsia)
- Kuzaa kwa njia ya upasuaji (caesarean section)
- Tatizo la kiumbe kutopata hewa vizuri wakati wa ujauzito (fetal distress)
BMI (kg/m2) = Uzito katika kilograms/Urefu katika meters². Maana yake ni kwamba ili kuweza kupata BMI itakayokuwezesha kujifahamu kama u mnene ama la, chukua uzito wako gawa kwa kipeo cha pili cha urefu wako.
Tatizo la unene uliopitiliza husababishwa na nini ?
Kuna mambo kadhaa yanayoweza kusababisha unene uliopitiliza. Mambo hayo ni pamoja na
Vihatarishi vya tatizo la unene wa kupitiliza
Aidha yapo mambo kadhaa ambayo yanaweza kumuhatarisha mtu kupata unene wa kupitiliza. Mambo haya ni pamoja na
Magonjwa yanaoweza kuambatana na tatizo la unene uliopitiliza
Tiba ya kuongezeka unene kupita kiasi
Tiba ya tatizo hili ni mhusika kujitambua ya kwamba ana tatizo na kuwa tayari kupunguza uzito. Mabadiliko ya tabia ya mhusika ni muhimu sana, mabadiliko haya yawe ndio mfumo wa maisha yake ya kila siku.
Kupungua uzito na kujilinda au kutunza uzito ulionao baada ya kupunguza uzito ni jambo la msingi sana na inahusisha mazoezi, chakula na mabadiliko ya tabia ya mtu.
Kama hujazoea kufanya mazoezi ni vizuri uanze taratibu na ujiwekee lengo kwa kufanya mazoezi kwa muda wa nusu saa kila siku, siku tano kwa wiki,(dakika 30 kila siku kwa siku tano kwa wiki). Mazoezi mazuri ni kama kuogelea, kuendesha baiskeli, kutembea, kunyanyua vitu vizito (visiwe vyenye uzito mkubwa), mazoezi ya viungo na kadhalika. Kama mtu ni mnene sana basi ni bora kuzungumza na daktari wako kabla ya kuanza mazoezi mapya. Baada ya kuanza mazoezi kwa mara ya kwanza, mwili utakuwa na maumivu, hii ni kawaida lakini kama mtu atapata maumivu zaidi ya masaa 2 baada ya kufanya mazoezi ni vizuri kumuona daktari.
Wanawake ambao wana uzito wa kupitiliza (obese women) wakiwa wajawazito wako kwenye hatari ya kupata madhara yafuatayo;
Lebo:
Lifestyle
Kula Machungwa na Zabibu kunapunguza uwezekano wa kupata kiharusi (Stroke)
Utafiti huu umehusisha maelfu ya wanawake wanaoshiriki katika tafiti ya manesi Nurse’s Health Study lakini wataalamu wanaamini faida hizo za machungwa na zabibu pia zinapatikana kwa wanaume.
Timu ya watafiti katika chuo cha Norwich Medical School katika Chuo Kikuu cha East Anglia wamechunguza umuhimu wa kemikali aina yaflavonoids ambayo ni jamii ya antioxidant (kemikali zinauwa kemikali hatari za kwenye mwili) inayopatikana katika matunda, mboga za majani, chocolate nyeusi na wine nyekundu.
Utafiti huu ulifuatilia takwimu za miaka 14 za wanawake 69,222 ambao walikuwa wakishirki katika tafiti kwa kuandika kiwango chao cha kula matunda na mboga za majani kwa kila kipindi cha miaka 4. Timu hiyo ya utafiti iliangalia uhusiano wa aina sita yaflavonoids - flavanones, anthocyanins, flavan-3-ols, flavonoid polymers, flavonols naflavones na hatari ya aina mbalimbali za kiharusi kama Ischaemic, Hemorrhagic na Total Stroke. Ilionekna wanawake waliokula kiwango kikubwa cha flavanones kwenye matunda chachu walikuwa na asilimia 19 ya uwezekano wa kupunguza kiharusi kulinganisha na wanawake ambao walikula kiwango kidogo cha matunda hayo.
Kiwango kikubwa cha flavanones kilikuwa 45mg kwa siku kulinganisha na kiwango kidogo cha 25mg kwa siku. Utafiti huu ulichapishwa katika jarida la Medical Journal Strokeumesema flavanones hupatikana kwa asilimia 82 kwenye machungwa na juisi ya machungwa na hupatikana kwa asilimia 14 kwenye zabibu na juisi ya zabibu. Hata hivyo watafiti hao wamesema kwa wale wenye kusudio la kuongeza kiwango kikubwa cha flavanones itawalazimu kula tunda la chungwa kwa wingi na si juisi za machungwa zinazotengenezwa kiwandani kutokana na kiwango kikubwa cha sukari kinachopatikana katika juisi hizo za viwandani.
Professa Aedin Cassidy wa masuala ya lishe bora (nutrition) na ambaye alikuwa kiongozi wa utafiti huo amesema “kula kwa wingi kwa matunda, mboga za majani, na hasa Vitamin C uhusishwa na kupunguza uwezekano wa kupata kiharusi”. Flavanones hutoa kinga dhidhi ya kiharusi kutokana na kuongeza ufanisi wa mishipa ya damu kwenye ubongo na kutokana na kuwa na uwezo wa kuzuia maambukizi mwilini (Anti-inflammatory effect).
Utafiti uliofanyika hapo awali ulionyesha ya kwamba ulaji wa matunda chachu na juisi yake na si matunda ya aina nyingine yoyote hupunguza uwezekano wa kupata kiharusi aina yaIschaemic Stroke na kuvuja damu kwenye ubongo (Intracerebral Haemorrhage).
Utafiti mwingine uliofanyika kipindi cha nyuma ulionyesha hakuna uhusiano wowote wa matunda ya njano na machungwa katika kupunguza uwezekano wa kupata kiharusi lakini ulionyesha ya kwamba kuna uhusiano wa zabibu na mapeasi wa kupunguza uwezekano wa kupata kiharusi.
Katika utafiti mwingine uliofanyika nchini Sweden umeonyesha ya kwamba wanawake ambao walikula kiwango kikubwa cha antioxidant karibia asilimia 50 kutoka kwenye matunda na mboga za majani, ni wachache tu kati yao waliopata kiharusi ikilinganishwa na wanawake ambao walikuwa na kiwango kidogo cha antioxidant.
Matokeo ya utafiti huu yasiwafanye watu kuacha kula matunda ya aina nyingine pamoja na mboga za majani kwani nayo yana faida kubwa katika mwili wa binadamu.
Kupunguza uwezekano wa kupata kiharusi inawezekana kama mtu atakula lishe bora iliyo na virutubisho vyote muhimu, kula matunda na mboga za majani kwa wingi, kufanya mazoezi mara kwa mara, kupunguza kiwango cha ulaji chumvi (kwani watu wenye asili ya Kiafrika wana kiashiria cha asili kinachojulikana kama salt retention gene ambacho hufanya kiwango kidogo cha matumizi ya chumvi mwilini kuonekana kama kiwango kikubwa na hivyo kuongeza hatari ya kupata kiharusi), kupunguza uzito (kuwa kwenye uzito unaotakikana kiafya kulingana na umri na urefu wako), kupunguza kiwango cha matumizi ya mafuta katika chakula, kulala masaa ya kutosha na kupunguza msongo wa mawazo.
Lebo:
Lifestyle
July 29, 2014
July 26, 2014
Mke wa Mbunge Dr Cyril Chami adaiwa kumuua "Housegirl"
Mfanyakazi wa ndani wa mbunge wa Jimbo la Moshi vijijini Cyril Chami (CCM) aitwaye Mariam Said (16) amefariki dunia mapema alfajiri ya leo ikiaminika kwabmba kifo chake kimesababishwa na kipigo toka kwa mke wa Mbunge huyo.
Sababu kubwa ikielezwa kuwa binti huyo ambaye ni muislamu alikataa kwenda kuhudhuria misa kanisani siku ya jumapili na amekua na tabia ya kupinga kwenda kanisani kila mara tangu aajiriwe na mbunge huyo kwa madai kuwa ni kinyume na imani yake (Uislamu).
Msimamo wa binti huyo ulimpelekea kipigo kikali usiku wa siku hiyo (jumapili) ambapo inadaiwa alivunjika mbavu baada ya mke wa mbunge kumpiga na stuli ubavuni.
Majirani wa mbunge huyo wanasema licha ya binti huyo kuvunjika mbavu hakupewa matibabu yoyote badala yake alifungiwa ndani huku akiendelea kulazimishwa kufanya kazi.
Mbaya zaidi mke wa Mbunge huyo alimnyang'anya simu binti huyo ili asiweze kuwasiliana na familia yake na kuwaeleza yaliyompata. Hata majirani walipomuuliza juu ya hali ya mtoto huyo aliwajibu kwa lugha ya kejeli na kuwaambia hakuna mtu anaweza kumfanya chochote, kwani serikali ya Chama Cha mapinduzi (CCM) ni yao.
Kutokana na maumivu makali pamoja na kukosa matibabu hatimaye binti huyo amefariki dunia leo asubuhi.
Source: Radio Moshi Fm
Lebo:
Lifestyle
Matokeo ya usaili Uhamiaji: 90% ni Watoto na Ndugu wa wafanyakazi wa Uhamiaji!
1. Abdulhaq Amin Mandemla – Mtoto wa afisa Uhamiaji Amin Mandemla
2. Alphonce Kishe – Mtoto wa Afisa Uhamiaji Aleluya Kishe
3. Asha Burhani Idd – Ndugu ya Afisa Uhamiaji Tatu Burhani Idd
4. Beatrice Temba – Ndugu wa Afisa Uhamiaji Joseph Kasike
5. Geofrey Justine Mhagama – Ndugu ya Afisa Uhamiaji Rose Mhagama
6. Iginga Daniel Mgendi – Mtoto wa Afisa Uhamiaji Daniel Mgendi
7. Issack Michael Makwinya – mtoto wa aliyekuwa Afisa Uhamiaji Makwinya
8. John Alfred Mungulu – mtoto wa Afisa Uhamiaji Alfred Mungulu
9. Joseph A. Milambo - mtoto wa Karani wa Uhamiaji Milambo
10. Michael J. Choma – mtoto wa Afisa Uhamiaji John Choma
11. Shimba H Zakayo – mtoto wa Afisa Uhamiaji Zakayo Mchele
12. Upendo E. Mgonja - mtoto wa Afisa Uhamiaji Mgonja
13. Vaileth A. Kidesu – mtoto wa Afisa Uhamiaji Adam Kidesu
14. Elizabeth Edward – Ndugu wa Afisa Uhamiaji Edward Martin
15. Ester Mahirane – Ndugu wa Afisa Uhamiaji Mahirane
16. Basil Lucian John – Ndugu wa Afisa Uhamiaji Dismas Lucian
17. Frank E Kajura- Ndugu wa Afisa Uhamiaji Kajura
18. Jacob P. Ulungi – Ndugu wa Afisa Uhamiaji Magnus Ulungi
19. Janeth John Milinga – Ndugu wa aliyekuwa Afisa Uhamiaji Milinga
20. Janeth R Lukuwi – Ndugu wa Afisa Uhamiaji Eliza Lukuwi
21. Joseph N. Yondani – Mtoto wa Afisa Uhamiaji Mary Yondani
22. Leila khatib Irovya - Mtoto wa Afisa Uhamiaji Abbas Irovya
23. Lucian F. Mlula – ndugu wa Afisa Uhamiaji Dismas Mlula
24. Neema Kasian Lukosi- Ndugu wa Afisa Uhamiaji Zubeda Abbas
25. Pendo D. Gambadu – ndugu wa Afisa Uhamiaji Gambadu
26. Paschalia E. Mwenda – ndugu wa Martin Edward mwenda
27. Theresia Ernest Kalunde – Mtoto wa Ernest Kalunde
28. Veronica G Vitalis – Mtoto wa aliyekuwa Afisa Uhamiaji Vitalis Mlay
29. Victor G. Mlay- Mtoto wa aliyekuwa Afisa Uhamiaji Vitalis Mlay
30. Catherine J. Mapunda- mtoto wa Afisa Lucy Mapunda
2. Alphonce Kishe – Mtoto wa Afisa Uhamiaji Aleluya Kishe
3. Asha Burhani Idd – Ndugu ya Afisa Uhamiaji Tatu Burhani Idd
4. Beatrice Temba – Ndugu wa Afisa Uhamiaji Joseph Kasike
5. Geofrey Justine Mhagama – Ndugu ya Afisa Uhamiaji Rose Mhagama
6. Iginga Daniel Mgendi – Mtoto wa Afisa Uhamiaji Daniel Mgendi
7. Issack Michael Makwinya – mtoto wa aliyekuwa Afisa Uhamiaji Makwinya
8. John Alfred Mungulu – mtoto wa Afisa Uhamiaji Alfred Mungulu
9. Joseph A. Milambo - mtoto wa Karani wa Uhamiaji Milambo
10. Michael J. Choma – mtoto wa Afisa Uhamiaji John Choma
11. Shimba H Zakayo – mtoto wa Afisa Uhamiaji Zakayo Mchele
12. Upendo E. Mgonja - mtoto wa Afisa Uhamiaji Mgonja
13. Vaileth A. Kidesu – mtoto wa Afisa Uhamiaji Adam Kidesu
14. Elizabeth Edward – Ndugu wa Afisa Uhamiaji Edward Martin
15. Ester Mahirane – Ndugu wa Afisa Uhamiaji Mahirane
16. Basil Lucian John – Ndugu wa Afisa Uhamiaji Dismas Lucian
17. Frank E Kajura- Ndugu wa Afisa Uhamiaji Kajura
18. Jacob P. Ulungi – Ndugu wa Afisa Uhamiaji Magnus Ulungi
19. Janeth John Milinga – Ndugu wa aliyekuwa Afisa Uhamiaji Milinga
20. Janeth R Lukuwi – Ndugu wa Afisa Uhamiaji Eliza Lukuwi
21. Joseph N. Yondani – Mtoto wa Afisa Uhamiaji Mary Yondani
22. Leila khatib Irovya - Mtoto wa Afisa Uhamiaji Abbas Irovya
23. Lucian F. Mlula – ndugu wa Afisa Uhamiaji Dismas Mlula
24. Neema Kasian Lukosi- Ndugu wa Afisa Uhamiaji Zubeda Abbas
25. Pendo D. Gambadu – ndugu wa Afisa Uhamiaji Gambadu
26. Paschalia E. Mwenda – ndugu wa Martin Edward mwenda
27. Theresia Ernest Kalunde – Mtoto wa Ernest Kalunde
28. Veronica G Vitalis – Mtoto wa aliyekuwa Afisa Uhamiaji Vitalis Mlay
29. Victor G. Mlay- Mtoto wa aliyekuwa Afisa Uhamiaji Vitalis Mlay
30. Catherine J. Mapunda- mtoto wa Afisa Lucy Mapunda
Hawa ni wachache tu kati ya wale walioajiriwa Uhamiaji ila zaidi ya asilimia tisini ni watoto na ndugu wa Maafisa Uhamiaji.
Nadhani ingekuwa vyema kama wahusika wasingekuwa wanatangaza nafasi hizi bali wawe wanagawiana ndani kwa ndani.
Nadhani ingekuwa vyema kama wahusika wasingekuwa wanatangaza nafasi hizi bali wawe wanagawiana ndani kwa ndani.
Lebo:
Lifestyle
July 22, 2014
Inatisha: Mabaki ya miili ya binadamu yakutwa Kichakani Dar!
Mabaki ya miili ya watu zaidi ya 100 imekutwa katika msitu mdogo uliopo eneo la Mpiji, kata ya Mbweni, wilaya ya Kinondoni, jijini Dar es Salaam, ikiwa imetelekezwa.
Mabaki hayo ya miili yalionekana jana katika eneo hilo majira ya jioni na kuvuta mamia ya wananchi waliokwenda kushuhudia tukio hilo.Mmoja wa mashuhuda wa tukio hilo alisema: mabaki yalikuwa yamehifadhiwa katika mifuko ya plastiki ikiwa imefungwa juu.
Alisema mabaki hayo ambayo yamekaushwa na kuhifadhiwa katika mifuko ya ujazo wa kilo 25 ni pamoja na miguu, mikono, mbavu na mafuvu ya vichwa.
Alisema waliobaini kuwapo kwa mabaki hayo ni majirani wa eneo hilo ambao walitoa taarifa polisi.
Polisi walifika eneo la tukio na kuanza kupakia mabaki hayo katika gari lao lenye namba za usajili MS 54 UKH na kuipeleka hospitali kwa ajili ya uchunguzi zaidi.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Kinondoni, Camilius Wambura, alipoulizwa alisema wakati huo alikuwa eneo la tukio na kwamba angetoa taarifa baadaye.
Mabaki hayo ya miili yalionekana jana katika eneo hilo majira ya jioni na kuvuta mamia ya wananchi waliokwenda kushuhudia tukio hilo.Mmoja wa mashuhuda wa tukio hilo alisema: mabaki yalikuwa yamehifadhiwa katika mifuko ya plastiki ikiwa imefungwa juu.
Alisema mabaki hayo ambayo yamekaushwa na kuhifadhiwa katika mifuko ya ujazo wa kilo 25 ni pamoja na miguu, mikono, mbavu na mafuvu ya vichwa.
Alisema waliobaini kuwapo kwa mabaki hayo ni majirani wa eneo hilo ambao walitoa taarifa polisi.
Polisi walifika eneo la tukio na kuanza kupakia mabaki hayo katika gari lao lenye namba za usajili MS 54 UKH na kuipeleka hospitali kwa ajili ya uchunguzi zaidi.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Kinondoni, Camilius Wambura, alipoulizwa alisema wakati huo alikuwa eneo la tukio na kwamba angetoa taarifa baadaye.
Lebo:
Lifestyle
July 10, 2014
Huyu ndiye waziri jangili!!
Ni kwa umahiri wake kuunganisha majangili..
WAZIRI aliyeukwaa wadhifa huo katika mabadiliko ya mwisho ya Baraza la Mawaziri yaliyofanyika mapema mwaka huu, akiongoza wizara nyeti, amebainika kuratibu mtandao wa ujangili wenye mizizi yake wilayani Manyoni na maeneo mengine mkoani Singida, vyanzo vya uhakika vya habari vimeeleza.
Waziri huyo (jina linahifadhiwa kwa sasa) amekuwa na mawakala maalumu katika maeneo ya karibu na mapori kunakoendeshwa ujangili na mara kwa mara, hufika wilayani Manyoni kuhakiki ufanisi wa mtandao wake huo wa ujangili, huku gazeti hili likielezwa kwamba, taarifa zake ziko ‘mikononi’ mwa vyombo muhimu vya dola nchini.
Kutoka wilayani Manyoni, mkoani Singida, taarifa za ‘kiintelijensia’ zinafichua kwamba mtandao wa waziri huyo unaongozwa na mfanyabiashara (jina linahifadhiwa) wa maduka ya vifaa. Mfanyabiashara huyo ni mkazi wa kitongoji cha Mnyang’ombe mjini Manyoni na kazi zake hizo ndani ya mtandao wa ujangili huzifanya hadi mkoani Tabora.
Inadaiwa kwamba ukaribu kati ya mfanyabiashara huyo na waziri husika umejijengea nguvu zaidi kutokana na umakini wake katika kufanikisha matukio ya ujangili.
Taarifa zinabainisha kwamba mfanyabiashara huyo amekuwa na vijana maalumu ambao kazi yao ni kukusanya pembe za ndovu kutoka katika maeneo ya Itigi, Ilangali lakini katika kituo cha Manyoni, mfanyabiashara huyo hufanya kazi hiyo yeye binafsi.
Vijana hao (majina yanahifadhiwa pamoja namba zao za simu), mmoja anaishi Manyoni akimiliki namba tatu za mtandao wa aina mmoja wa simu za mkononi, mwenzake mwingine ni mwenyeji katika vijiji vinavyopakana na Pori la Akiba Rungwa, maeneo ya Kizigo. Kijana huyo wa Kizigo ndiye mnunuzi wa meno yote ya tembo yanayopatikana maeneo hayo kwa niaba ya mtandao huo.
Mbali na vijana hao wawili, yupo kijana mwingine (jina linahifadhiwa kwa sasa), huyu ni mkazi wa kijiji cha Ilangali, naye akiwa anamiliki namba tatu tofauti za simu za mtandao mmoja wa mawasiliano ya simu za mkononi. Kazi kubwa ya kijana huyu katika mgawanyo wa majukumu ya kijangili ni kuhifadhi silaha sambamba na kununua meno ya tembo kwa ‘wadau’ hapo kijiji cha Ilangali na baada ya kununua meno hayo, mfanyabiashara wa Manyoni hufika kuyachukua.
Mbinu za usafirishaji
Baada ya kazi ya ununuzi na ukusanyaji kukamilika, meno ya tembo yaliyopatikana, husafirishwa kwa njia ya reli ya kati chini ya usimamizi wa mfanyakazi mmoja wa Shirika la Reli Tanzania (jina linahifadhiwa) mwenye makazi yake mjini Morogoro.
Mfanyakazi huyo husimamia usafirishaji wa meno hayo kutoka Tabora hadi Itigi ambako hapo hupokelewa na mfanyabiashara (wa Manyoni) ambaye huyahifadhi hapo Manyoni.
Yakiwa hapo Manyoni, meno hayo huhifadhiwa kwa mmiliki wa mojawapo ya hoteli kubwa na maarufu mjini Manyoni, mwenye asili ya mikoa ya kanda ya kaskazini, ambaye yeye huwasiliana na waziri kwa ajili ya maelekezo zaidi juu ya namna ya kusafirisha meno hayo.
Taarifa za kiuchunguzi zinazidi kubainisha kwamba mara nyingi, waziri husika hufika hapo Manyoni kwa ajili ya kuchukua “mzigo” na kila anapokwenda huongozana na mwanamke mmoja, mwenye lafudhi ya watu kutoka mikoa ya kanda ya kaskazini (jina linahifadhiwa).
Mwanamke huyo ndiye hutumiwa kusafirisha meno hayo yaliyokusanywa yakiwamo ya kutoka ‘kituo’ chao cha Puma, mkoani Singida, ili hatimaye kuyafikisha wanakokubaliana yafike.
Waziri huyo anapokuwa Manyoni amekuwa na kawaida ya kuwakusanya washirika wake katika mtandao huo na wote hupata malazi yao katika moja ya hoteli kubwa na maarufu hapo Manyoni.
Wakiwa hapo Manyoni na bosi (waziri) genge hilo la kijangili hujiimarisha kiulinzi kwa kuweka watu wa kulinda hoteli husika na hata kudadisi wageni wengine wanaofika hotelini hapo.
Katika maeneo ya Singinda, mjini Puma, yupo kijana maalumu anayetumiwa na waziri huyo ambaye anatajwa kuwa na undugu wa namna fulani na mteule huyo wa Rais Kikwete. Kijana huyu hutumia namba za mitandao miwili tofauti ya simu za mkononi.
Huyu kazi yake kubwa ni kuwaunganisha wawindaji (wenyewe majangili huita wapigaji) na wakati mwingine hutokea waziri ndiye anayekusanya mzigo. Wakati uchunguzi huu ulipokuwa ukifanyika, kijana huyo alikuwa na meno ya tembo yaliyokuwa yamehifadhiwa eneo la Tinde, mkoani Shinyanga. Hata hivyo, uaminifu wa kijana huyo si mkubwa kwa sababu uchunguzi wetu umebaini wakati mwingine ‘huchota’ mzigo kiasi fulani na kuuza kinyemela bila mtandao kujua.
Kijana huyo, kati ya kazi alizowahi kufanya ni kuwaunganisha baadhi ya vijana na mwindaji kutoka Wilaya ya Igunga (jina na mawasiliano yake yanahifadhiwa). Mwindaji huyo wa Igunga anamiliki bunduki aina ya Rifle (namba inahifadhiwa) na wakati uchunguzi wa gazeti hili ukifanyika, alikuwa na vipande sita vya meno ya tembo ambavyo ni sawa na meno matatu.
Kwa wakati huo tukifanya uchunguzi, waziri husika alitoa maelekezo vijana wake wasimamishe shughuli zao kwa muda.
Huko wilayani Kahama, mkoani Shinyanga, Waziri husika anashirikiana na mtu (jina linahifadhiwa) ambaye anafanya biashara ya ng’ombe kama kinga ya kuficha shughuli zake za ujangili. Mtu huyu ni mnunuzi wa meno ya tembo na hukusanya meno yanayotoka katika mapori ya Moyowosi, Kigosi, Burigi, Biharamulo na Kimisi.
Hivi karibuni, mtu huyo amekuwa akikusanya meno ya tembo yanayotoka Moyowosi na amekuwa na wadau wake ambao ni watumishi wa serikali katika mapori ya Burigi na Biharamulo. Mtu huyo amenunuliwa na waziri husika gari aina ya Rav4, kwa ajili ya kukusanya meno ya tembo maeneo ya vijiji vinavyozunguka mapori hayo.
Katika maeneo ya Ilongelo na Ngamo, mkoani Singida, huko waziri husika anaendesha mtandao wake wa ujangili kwa kushirikiana na tajiri mmoja, mwenye asili ya Mkoa wa Simiyu ambaye naye anao mtandao mkubwa unaowahusisha vigogo kadhaa, akiwamo mmoja wa wabunge aliyepata kupigia kelele kuhusu ufisadi bungeni, zikiwamo fedha za akaunti za Uswisi, mbunge huyu ni mwenyeji wa kanda ya ziwa na ni kijana kwa umri.
Taarifa za kiuchunguzi zinabainisha kwamba meno ya tembo yanayokusanywa maeneo ya Singida, Kahama na Meatu hufikishwa katika kijiji cha Ngamo ambako waziri husika akiwa na mwanamke mmoja mkazi wa moja ya mikoa ya kaskazini ambaye ndiye mwenye jukumu la kusafirisha meno hayo.
Mtandao wa waziri huyo umejipanua zaidi katika operesheni za kijangili, ukihusisha Wilaya ya Babati, mkoani Manyara. Huko Babati, katika kijiji cha Mayoka, kuna tawi la ujangili la waziri huyo.
Msimamizi wa shughuli za kijangili eneo hilo ni mtu (jina linahifadhiwa) ambaye mara kwa mara huwapo Dodoma kila waziri husika anapokuwa huko kwa shughuli za Bunge. Huyu mtu ndiye husimamia ukusanyaji meno ya tembo kutoka maeneo ya Magugu na Mayoka, wakipata meno hayo kutoka katika Hifadhi ya Taifa Tarangire na ushoroba wa Tarangire – Manyara.
Kutokana na umahiri wa kuunganisha mitandao wa kijangili nchi nzima, waziri huyo kwa baadhi ya watu analinganishwa na pweza au buibui kutokana na kunasa na kuunda mtandao mpana.
Chanzo Gazeti la Raia Mwema
July 8, 2014
Mabomu Arusha hali ni tete!
•Ni katika mgahawa wa kihindi ujulikanao kama Vama Restaurant uliopo maeneo ya Gymkhana.
•Bomu jingine lakutwa limetegwa nyumbani kwa mkuu wa mkoa Arusha Bw.Magesa Mulongo.
Jeshi la Polisi bado halijatoa tamko lolote na linaendelea kufanya uchunguzi juu ya tukio hili la mlipuko wa Bomu ambao ni tukio la sita kutukia jijini Arusha.
1. Olasiti Kanisani
2. Soweto Chadema
3. USA River mkesha wa mwaka mpya
4. Matako Bar wakati wa UEFA
5. Majengo kwa Sheikh
6. Mgahawa wa kihindi ujulikanao kama Vama Restaurant (sasa)
Lebo:
Lifestyle
July 7, 2014
Vazi la taifa la Tanzania, yapi maoni yako?!
Baada ya mchakato wa muda mrefu wa upatikanaji wa vazi rasmi la Mtanzania kusuasua na kuonekana wazi kwamba upatikanaji wake umeshindikana na hakuna jitihada zozote kuntu zinazofanywa na seriakali kupelekea upatikanaji wa vazi hilo rasmi la taifa hatimaye Mbunifu ambaye hakutaka jina lake kutajwa mara moja ameibuka na vazi lake kama inavyoweza kuonekana pichani na kuishauri Serikali ilipitishe kuwa vazi rasmi la taifa kwasababu linakidhi vigezo na mahitaji ya vazi halisi la taifa.
Akiendelea kuongea na Maisha Times mbunifu huyo mchanga aliongeza kwamba imekuwa ni vigumu kupatikana kwa vazi la taifa kwasababu Watanzania walio wengi wameonekana kuvutiwa zaidi na mavazi ya kimagharibi kuliko mavazi yao ya kiasili jambo ambalo baada ya mbunifu huyo kulitafakari kwa kina ndipo alipoamua kuja na vazi hilo alilolipa jina na "nusu nusu" kwa namna muonekano wake ulivyo (Sura Mbili) ambapo upande mmoja umebeba utamaduni wa kimagharibi na upande mwingine umebeba utamaduni wa Kitanzania zaidi kama inavyoweza kuonekana pichani.
Je wewe una ushauri gani kuhusiana na vazi hili ambalo mbunifu amependekeza na kutaka Serikali ilipitishe kuwav vazi rasmi la taifa?
Lebo:
Lifestyle
June 30, 2014
Ulokole umekuja kuuimarisha au kuuvuruga ukristo??!!
Pichani ni walokole ambao kwa Imani yao waliambiwa na Mchungaji wao kwamba wakila majani watakuwa karibu na Mungu.
Nakumbuka wakati nikiwa na miaka 7 na kuendelea kulikuwa na madhebebu kama manne makubwa ya Kikristo ambayo niliyafahamu kwa mf:
1. Catholic
2. Lutheran
3. Anglican
4. Advent. Sabath
ambapo kila dhehebu liliisimamia vyema imani ya kikristo sambamba na nidhamu ya viongozi na waumini wake inavyotakikana,. Lakini tangu kuingia kwa hili wimbi la madhehebu ya "Kilokole" katika nchi mbalimbali barani Afrika hususani nchini Tanzania ambapo hapo awali madhebebu hayo hayakuwepo hali imebadilika na vitendo vinavyoidhalilisha dini ya Kikristo vimeonekana kuongezeka kwa kiasi kikubwa kutokana na mambo mbalimbali kwa mf. Vitendo vinavyofanywa na Viongozi wa madhehebu hayo au Waumini wa madhehebu hayo.
Swali ni langu ni je: Tatizo ni nini?
1. Madhehebu hayo.
2. Wamiliki/Viongozi wa madhehebu hayo.
3. Waumini wa madhehebu hayo.
4. Mabadiliko ya hali ya kimaisha.
5. Imani mbadala zinazoupinga Ukristo?
Au tatizo ni nini haswa?¿
Naipenda sana dini yangu ya Kikristo pasipo kujali dhebebu lolote lakini nachukizwa sana na vitendo vinavyofanywa na baadhi ya wamiliki/viongozi na waumini wa madhehebu ambavyo vinaudhalilisha na kuupaka matope Ukristo.
Lebo:
Lifestyle
May 30, 2014
Pigo tena katika tasnia ya Bongo Movie: George Tyson afariki!
Marehemu George Tyson alipokuwa akiongea na kituo cha EATV enzi za uhai wake.
Ni pigo tena kwa tasnia ya Bongo Muvi, mwongozi filamu Bongo na aliyekuwa mume wa staa wa filamu za Kibongo, Yvonny Cherry 'Monalisa', George Tyson amefariki dunia baada ya kupata ajali mbaya ya gari maeneo ya Gairo, Morogoro akitokea mkoani Dodoma. Tyson alikuwa ameambatana na watu kadhaa katika safari hiyo ambao wanadaiwa kuumia vibaya.
Mwili wa marehemu Tyson pamoja na majeruhi wa ajali hiyo wamepelekwa Hospitali ya Mkoa wa Morogoro.
Tyson enzi za penzi lake na Monalisa walifanikiwa kupata mtoto aitwaye Sonia.
Maisha Times Blog inatoa pole kwa familia, ndugu, jamaa na wasanii wote wa tasnia ya Bongo Movie kwa msiba mzito wa kuondokewa na kaka mpendwa George Tyson.
Lebo:
Lifestyle
May 29, 2014
It's a shame that these posts can't be filled by Tanzanians!
A program is about to start in Tanzania, funded by Bill Merinda Gate Foundation, for transformation of the agricultural industry. However, the Senior Program Officer / Senior Regional Advisor -East Africa, who is Kenyan and based in Seattle, has told me that they have failed to find qualified Tanzanians to fill the positions indicated below. I did not believe her because I know we have a lot of talent in the different agricultural sciences. Please help to look for the right people so we do not loose these opportunities to foreign experts. This is very URGENT.
Though it may seem closed, UNDP will still welcome good candidates. Ask them to write to Ernest Salla at ernest.salla@undp.org
Director of Agricultural Productivity: http://jobs.undp.org/cj_view_job.cfm?cur_job_id=45669
Director of Performance Analytics and Evaluation: http://jobs.undp.org/cj_view_job.cfm?cur_job_id=45659
Manager of Market Efficiencies: http://jobs.undp.org/cj_view_job.cfm?cur_job_id=45670
Manager of Planning and Budget: http://jobs.undp.org/cj_view_job.cfm?cur_job_id=45673
Manager of Production Monitoring: http://jobs.undp.org/cj_view_job.cfm?cur_job_id=45672
Senior Analyst: http://jobs.undp.org/cj_view_job.cfm?cur_job_id=45674
Communications Analyst: http://jobs.undp.org/cj_view_job.cfm?cur_job_id=41731
Analyst: http://jobs.undp.org/cj_view_job.cfm?cur_job_id=45675
Best regards
Juliana
Dr. Juliana Rwelamira
Managing Director
Sasakawa Africa Association
P O Box 24135 Code 1000
Addis Ababa
ETHIOPIA
E-mail: jrwelamira@saa-safe.org
Tel: +251-11 647-7670/7667
Mobile: +251 911 512 555
Tafadhali sambaza ujumbe forward to your contacts please...
Lebo:
Lifestyle
April 19, 2014
March 29, 2014
Jiji la Dsm Kero tupu- Mafuriko+Uchafu+Foleni=??!!
Kutokana na mvua kubwa zilizonyesha na zinazoendelea kunyesha katika maeneo mbalimbali nchini, hivi ndivyo hali ilivyokuwa katika baadhi ya maeneo mengi ya jiji la Dar es salaam kama unavyoweza kujionea katika Picha hapo juu.
Lebo:
Lifestyle
Subscribe to:
Posts (Atom)































