Marehemu George Tyson alipokuwa akiongea na kituo cha EATV enzi za uhai wake.
Ni pigo tena kwa tasnia ya Bongo Muvi, mwongozi filamu Bongo na aliyekuwa mume wa staa wa filamu za Kibongo, Yvonny Cherry 'Monalisa', George Tyson amefariki dunia baada ya kupata ajali mbaya ya gari maeneo ya Gairo, Morogoro akitokea mkoani Dodoma. Tyson alikuwa ameambatana na watu kadhaa katika safari hiyo ambao wanadaiwa kuumia vibaya.
Mwili wa marehemu Tyson pamoja na majeruhi wa ajali hiyo wamepelekwa Hospitali ya Mkoa wa Morogoro.
Tyson enzi za penzi lake na Monalisa walifanikiwa kupata mtoto aitwaye Sonia.
Maisha Times Blog inatoa pole kwa familia, ndugu, jamaa na wasanii wote wa tasnia ya Bongo Movie kwa msiba mzito wa kuondokewa na kaka mpendwa George Tyson.
No comments:
Post a Comment