Advertise with Us

Advertise with Us

DHall

DHall

Pages

June 30, 2014

Ulokole umekuja kuuimarisha au kuuvuruga ukristo??!!


Pichani ni walokole ambao kwa Imani yao waliambiwa na Mchungaji wao kwamba wakila majani watakuwa karibu na Mungu.

Nakumbuka wakati nikiwa na miaka 7 na kuendelea kulikuwa na madhebebu kama manne makubwa ya Kikristo ambayo niliyafahamu kwa mf:

1. Catholic
2. Lutheran
3. Anglican
4. Advent. Sabath 

ambapo kila dhehebu liliisimamia vyema imani ya kikristo sambamba na nidhamu ya viongozi na waumini wake inavyotakikana,. Lakini tangu kuingia kwa hili wimbi la madhehebu ya "Kilokole" katika nchi mbalimbali barani Afrika hususani nchini Tanzania ambapo hapo awali madhebebu hayo hayakuwepo hali imebadilika na vitendo vinavyoidhalilisha dini ya Kikristo vimeonekana kuongezeka kwa kiasi kikubwa kutokana na mambo mbalimbali kwa mf. Vitendo vinavyofanywa na Viongozi wa madhehebu hayo au Waumini wa madhehebu hayo.

Swali ni langu ni je: Tatizo ni nini?

1. Madhehebu hayo.
2. Wamiliki/Viongozi wa madhehebu hayo.
3. Waumini wa madhehebu hayo.
4. Mabadiliko ya hali ya kimaisha.
5. Imani mbadala zinazoupinga Ukristo?

Au tatizo ni nini haswa?¿

Naipenda sana dini yangu ya Kikristo pasipo kujali dhebebu lolote lakini nachukizwa sana na vitendo vinavyofanywa na baadhi ya wamiliki/viongozi na waumini wa madhehebu ambavyo vinaudhalilisha na kuupaka matope Ukristo.

No comments:

Post a Comment