Baada ya mchakato wa muda mrefu wa upatikanaji wa vazi rasmi la Mtanzania kusuasua na kuonekana wazi kwamba upatikanaji wake umeshindikana na hakuna jitihada zozote kuntu zinazofanywa na seriakali kupelekea upatikanaji wa vazi hilo rasmi la taifa hatimaye Mbunifu ambaye hakutaka jina lake kutajwa mara moja ameibuka na vazi lake kama inavyoweza kuonekana pichani na kuishauri Serikali ilipitishe kuwa vazi rasmi la taifa kwasababu linakidhi vigezo na mahitaji ya vazi halisi la taifa.
Akiendelea kuongea na Maisha Times mbunifu huyo mchanga aliongeza kwamba imekuwa ni vigumu kupatikana kwa vazi la taifa kwasababu Watanzania walio wengi wameonekana kuvutiwa zaidi na mavazi ya kimagharibi kuliko mavazi yao ya kiasili jambo ambalo baada ya mbunifu huyo kulitafakari kwa kina ndipo alipoamua kuja na vazi hilo alilolipa jina na "nusu nusu" kwa namna muonekano wake ulivyo (Sura Mbili) ambapo upande mmoja umebeba utamaduni wa kimagharibi na upande mwingine umebeba utamaduni wa Kitanzania zaidi kama inavyoweza kuonekana pichani.
Je wewe una ushauri gani kuhusiana na vazi hili ambalo mbunifu amependekeza na kutaka Serikali ilipitishe kuwav vazi rasmi la taifa?
No comments:
Post a Comment