Foleni ya magari kama inavyoweza kuonekana katika picha 1-3
Moja ya barabara katika mitaa ya jiji la Dar es Salaam
Imekuwa ni jambo la kawaida sana kuona foleni kubwa katika sehemu mbalimbali jijini Dar es salaam zinazotokana na karabati mbalimbali zinazofanywa ili kuboresha miundombinu mbalimbali jiji kwa maendeleo ya jiji na taifa kwa ujumla, Swali ni je, kuna ulazima wowote wa matengenezo hayo ya miundombinu mbalimbali haswa barabara, mabomba na mitaro ya maji machafu kufanyika nyakati za mchana na kusababisha adha kubwa ya foleni kwa raia badala ya matengenezo hayo kufanyika zaidi nyakati za usiku ambapo foleni na pilika mbalimbali zinakuwa zimepungua au hazipo kabisa?
Kwa upande mwingine naonelea kwamba iwapo serikali itaboresha kwa mpangilio barabara katika mitaa mbalimbali ya jiji la Dar es salaam hii itachangia sana kupunguza ulazima wa idadi kubwa ya magari na vyombo vinginevyo vya usafiri kulazimika kupita katika barabara kuu pekee kwa kule kuepuka kukwama au uharibifu wa vyombo vyao vya usafiri kutokana tu na ubovu wa barabara za mitaani ambazo sambamba na miundo mbinu yake kama mitaro ya kupitishia maji machafu kiuhalisia ni mbovu sana na kwa ujumla ni kama zimesahaulika.
No comments:
Post a Comment