Kulingana na hali halisi ya kimaisha ilivyo kwa sasa labda kutokana na ugumu wa ajira nk. tabia ya baadhi ya waajiri katika mashirika na kampuni mbalimbali kuwatongoza au
kuwadai rushwa ya ngono wale wanaokwenda kuomba kazi haswa haswa wanawake imekuwa inatishia hata baadhi ya watu [wanawake] kwenda kuomba kazi katika mashirika na makampuni mbalimbali kutokana na kuogopa kukumbana na dhahma za aina hiyo. Tukiachilia mbali maofisini pia vyuoni nako
rushwa ya ngono imekuwa ni kama njia mojawapo inayotumiwa na wahadhiri [lectures] wa vyuo
wasio waadilifu ili kupata wanachuo wa kike wanaokuwa labda wamewatamani au kuvutiwa nao kimwili na hivyo kutumia kigezo cha kuwabana/kuwafelisha kwa makusudi au kwa bahati mbaya katika mitihani yao na hatimaye kuweka makubaliano ya kuwabeba katika masomo au mitihani yao kulingana na somo husika.
Kwa hakika rushwa ya ngono ni tatizo linaloendelea kukua na kushika
kasi kubwa sana karibu katika kila nyanja ya ajira nchini kwani karibu kila mwanamke ambaye nimebahatika kuzungumza naye kuhusiana na maswala ya ajira amekuwa
akilalamikia tabia hii, na papohapo bado kuna janga la gonjwa hatari wa ukimwi ambalo
kiuhalisia halimtambui wala kumbagua mtu yeyote awaye.
No comments:
Post a Comment