Wajumbe wa mkutano mkuu wa UWT, wakiwasili mjini Dodoma tayari kwa uchaguzi unaofanyika Jumamosi Oktoba 20, 2012.
Mwenyekiti
wa Jumuiya ya Wanawake ya CCM, (UWT), ambaye anamaliza muda wake,
Sophia Simba, akiingia ukumbi wa Mipango tayari kwa uchaguzi mkuu wa
Jumuiya hiyo mjini Dodoma, Jumamosi Oktoba 20, 2012
Makamu
wa Rais, Dkt. Ali Mohammed Shein, (Kulia), Makamu wa Mwenyekiti wa
CCM, (Bara), Pius Mekwa, (Kushoto), na Mwenyekiti wa Jumuiya ya
Wanawake, UWT, Sophia Simba, mwanzoni mwa kikao cha uchaguzi cha Jumuiya
hiyo, mjini Dodoma, Jumamosi Oktoba 20, 2012.
Shy-Rose
Bhanji, (Kulia), akionyesha uso wa hasira huku akitulizwa na mjumbe
mwenzake, kufuatia tafrani kati yake na mwenyekiti wa Jumuiya ya
Wanawake Tanzania UWT), Sophia Simba
Mbunge
wa bunge la Afrika Mashariki, Shy-Rose Bhanji, (Aliyekaa), akitulizwa
hasira na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Uwkezaji na Uwezeshaji,
Dkt. Mary Nagu, wakati wa kikao cha uchaguzi mkuu wa Jumuiya ya Wanawake
ya CCM, UWT, kwenye ukumbi wa chuo cha Mipango Dodoma Jumamosi Oktoba
20, 2012.
Kimsingi swali hili lilikuwa ni swali makini, lililoulizwa wakati muafaka na kwa mtu sahihi kabisa anayetaka kupewa tena fursa ya uongozi.
Badala ya kujibu swali la Shyrose, Sophia Simba akajiuliza swali lake mwenyewe na kuja na majibu haya “Inaonekana aliyeuliza swali hajakomaa katika siasa za nchi, ndio maana ameambulia kuzomewa na wajumbe wa mkutano huu. Habwatuki bungeni au majukwaani kwa vile yeye ni serikali, na hata mbunge wa CCM hapaswi kukikosoa chama chake. Mimi si mithili ya upinzania kukaa na kukiosoa chama napaswa kukitetea. Anayesema Sofia Simba hajafanya kitu anajidanganya kwani wapiga kura wako kwenye matawi, kata, wilaya na mikoa, hao ndio wapiga kura wa chama na mimi kama mwenyekiti wa UWT nilijiimarisha katika ngazi za chini.”
Sophia
Simba ambaye ni Waziri wa Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto,
anakabiliwa na upinzani mkali kutoka kwa mbunge wa Same Mashariki, Anne
Kilango Malecela.
No comments:
Post a Comment