Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo [Chadema], Freeman
Mbowe, akihutubia wakazi wa Katesh, wilayani Hanang, juzi, katika
mkutano wa hadhara, uliofanyika Kata ya Endasaki. Picha na Mussa Juma
Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe alisema hayo jana katika
kikao cha viongozi wa chama hicho na wadau wake kilichofanyika hapa.
Mbowe alisema pikipiki hizo zitakuwa na vipaza
sauti maalumu zitawasaidia viongozi wa chama hicho kufanya kazi kwa
ufanisi zaidi.
“Tumeanza mkakati wa kuhakikisha tunawafikia
wananchi kila mahali. Tunataka kusikiliza matatizo yao, na hata pale
ambako kuna shida ya usafiri, kwa pikipiki tutafika,” alisema.
Tayari chama hicho kimezindua kampeni yake ya Vuguvugu la Mabadiliko (M4C), ambayo lengo lake ni kuwaandaa wananchi kwa uchaguzi ujao.
Tayari chama hicho kimezindua kampeni yake ya Vuguvugu la Mabadiliko (M4C), ambayo lengo lake ni kuwaandaa wananchi kwa uchaguzi ujao.
Mbowe alisema upatikanaji wa pikipiki hizo
unatokana na fedha za ruzuku ambazo zinatolewa na Serikali kwa chama
hicho pia marafiki na wanachama wake walioko nje ya nchi.
No comments:
Post a Comment