Advertise with Us

Advertise with Us

DHall

DHall

Pages

May 3, 2013

Breaking News: Serikali imefuta rasmi matokeo yote ya kidato cha nne mwaka 2012!

Serikali imetangaza kuanzia leo kufuta rasmi matokeo yote ya kidato cha nne mwaka 2012 na mitihani yote itasahihishwa upya kwa kutumia utaratibu ule uliotumika katika kusahihisha matokeo ya mwaka 2011.
Akisoma bungeni kwa niaba ya Waziri Mkuu ripoti ya awali ya Tume ya kuchunguza kushuka kwa matokeo Waziri wa Uratibu na Bunge William Lukuvi amesema hatua hiyo inatokana na uamuzi wa Baraza la Mawaziri ambao waliopokea taarifa ya tume hiyo ambayo imependekeza hatua hiyo.
Tanzania zaidi ya uijuavyo!

3 comments:

  1. Anonymous12:41 PM

    Kwa uamuzi wa serikali kuyafuta matokeo ya Kidato cha nne 2012 huu ni mtazamo wangu!

    1. Natumai uamuzi huu hauhusiani kabisa na kukwepa shinikizo la wananchi la kutaka waziri wa Elimu ajiuzulu.
    2. Kuyafuta matokeo hayo na kufanya usahihisaji upya hakufuti historia ya matokeo ya awali
    3. Matokeo yoyote yale ambayo yatakuwa kinyume au tofauti na yale ya awali yatasadifu uhalisia kwamba kulikuwa na uzembe mkubwa katika usahihishaji na hata utoaji wa matokeo ya awali na hivyo kuzidi kuweka msisitizo kuhusiana na suala la kujiuzulu kwa waziri wa wizara ya elimu na watendaji wake.
    4. Kutokana na yaliyojitokeza hapo awali sitarajii kama matokeo yajayo ya kidato cha nne yatakuwa yamelenga katika kumsafisha mtu yeyote awaye kwa cheo, wadhifa, nafasi yake au Serikali ya Tanzania..

    ReplyDelete
    Replies
    1. Anonymous2:08 PM

      Utaratibu uliotumika mwaka 2011 ni tofauti na wa mwaka 2012. Kwa hiyo matokeo tofauti yanaweza kutokea

      Delete
    2. Anonymous4:06 PM

      jifunze kusema kweli, ni tabia nzuri na faida kwa moyo wako. siku moja utayaacha haya yote kama walikutangulia walivyoyaacha. Utatoa hesabu ya utumishi wako kwa Mungu. Utavuna ilichopanda

      Delete