Kama ilivyokuwa kwa Mkuu wa Mkoa wa Mtwara jana kuongea na vyombo vya habari (Wapo Radio Fm) kwamba hali ni shwari Mtwara hali ni ileile kwa RPC ambaye naye anaongea na vyombo vya habari na kuwasihi wananchi waende makazini ilihali kiuhalisia hali sio shwari kabisa.
Taarifa zinasema kwamba tayari waziri wa mambo ya Ndani Emmanuel Nchimbi ameshaingia Mtwara akitokea Dodoma alipokuwepo kwaajili ya vikao vya Bunge.
Katika eneo la Mikindani inaripotiwa kwamba maaskari
wanaingia kwa nguvu majumbani mwa watu na kumsomba mtu yeyote ambaye ni mwanaume
awe amehusika au hajahusika na kumkamata. Maeneo ya Magomeni, Chikongola, Nkanaledi, Pia inaripotiwa uhalifu
unafanywa na maaskari hao jambo linaloamsha hisia na hasira kali kwa wananchi.
Mabasi 5 ya Champion yaliyobeba Wanajeshi yako njiani yakielekea eneo la matukio.
Serikali yatoa tamko yasema watu 91 wanashikiliwa na Jeshi la Polisi.
Mabomu na milio ya risasi inaendelea kusikika huku na huko tangu jana mpaka muda huu tunapoandika taarifa hii.
Raia wapatao 7 wameripotiwa kufariki (wengine walipelekwa hospitali ya Ndanda Ndogo na mmoja ameripotiwa kupokelewa Ligula.
Nyumba za viongozi zinaendelea kuchomwa moto.
Mpaka
sasa ni vita baina ya wananchi na Maaskari wa Jeshi la Polisi.
Jeshi la Polisi lalaumiwa kuhusika na Uvunjaji wa Nyumba, Maduka na kupora katika maeneo ya Magomeni Nkanaledi.
Vyanzo mbalimbali vyenye habari zinazoendana na hii bofya link hizi:
No comments:
Post a Comment