Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo
(Chadema) Wilfred Lwakatare
Dar es Salaaam. Jitihada za mawakili wa Mkurugenzi wa Ulinzi na
Usalama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Wilfred
Lwakatare, kumchomoa kutoka mahabusu leo zimegonga mwamba tena baada ya taarifa kutoka mahakamani kusema kwamba Hakimu mwenye jalada la Wilfred
Lwakatare bado yuko likizo hivyo atalazimika
kuendelea kusota mahabusu mpaka mwezi juni 10 mwaka huu.
Awali jitihada za mawakili hao kumtoa Lwakatare mahabusu kwa dhamana ziligonga mwamba kufuatia kitendo cha hakimu anayesikiliza kesi hiyo, Aloyce Katemana, kutokuwapo mahakamani kwa kile kilichosemwa kwamba yuko likizo na hivyo kusababisha kesi hiyo kuahirishwa mpaka leo Mei 27 ambapo hata hivyo bado hakimu huyo amedaiwa kuwa nje ya eneo la kazi kwa maana ya kuwa katika mapumziko ya likizo.

No comments:
Post a Comment