Imekuwa ni jambo la kawaida kwa TFDA na TBS kukagua bidhaa mbalimbali zitokapo ughaibuni kama madawa/vyakula nk. lakini pindi tu inapotokea wakigundua kwamba bidhaa hizo hazina ubora kwa haraka huchukua hatua/maamuzi ya kuziteketeza kwa moto tena kwenye ardhi ya Tanzania. Kwa kitendo hicho cha TBS na TFDA kutekeza bidhaa hizo batiili/zisizo na ubora tena kwa majigambo makubwa huku wakijua au kutokujua kwamba wanachafua hali ya hewa na kuharibu mazingira kwa ujumla maswali ya kujiuliza ni:
1. Kwanini bidhaa hizi zisirudishwe katika nchi zilipotoka kwa gharama za wale waliozileta na kuteketezwa huko?!
2. Hivi Tanzania ni dampo la uteketezaji wa takataka za ughaibuni?!
3. Nani atawafidia watanzania madhara (extenalities) yatakayotokana na uchafuzi wa hali ya hewa/uharibifu wa mazingira?!
4. NEMC mko wapi?! Mnatambua au hamtambui wajibu wenu?! Au kazi yenu ni fitna, kutalii, kuzurura sehemu mbalimbali nchini huku mkitafuna bure kodi za watanzania wavuja jasho?!
Maswali na maneno haya makali yalitolewa na Mwananchi mmoja aliyekerwa na hali hiyo.
Angalia Video bofya hapa http://www.youtube.com/watch?v=5pBhbiNfy4o&feature=youtu.be
No comments:
Post a Comment