Advertise with Us

Advertise with Us

DHall

DHall

Pages

May 13, 2013

TIGO YAZINDUA INTERNET YA HARAKA ZAIDI TANZANIA!

Pichani ni Meneja mkuu wa kampuni ya Tigo , Diego Gutierrez ( kushoto) akizindua INTANETI YA HARAKA ZAIDI TANZANIA, huduma ya internet yenye kasi ya 4G, ambayo ni huduma yenye nguvu zaidi ya vipimo vya hadi 42Mbps itakayowawezesha wateja hao kuperuzi, kupakua na kupakia taarifa mbalimbali kwenye mtandao na kucheza gem kwa haraka zaidi kuliko ilivyokuwa siku za nyuma.Kulia Deon Geyser, mfanyakazi kutoka Tigo MAKAO MAKUU.


 Wanafunzi wa chuo kikuu cha Dar es Salaam wakicheza na wanafunzi kutoka chuo kikuu cha Dodoma kwenye Playstation 3 kupitia kasi mpya ya intanet ya Tigo.
 
Waandishi wa habari waliokuwa chuo kikuu cha Dar es Salaam wakicheza michezo kwenye Playstation 3 na Waandishi wa habari waliokua Dodoma kupitia internet yenye kasi zaidi kutoka Tigo.
 Mwakilishi kutoka kampuni ya Tigo, John Sicilima, kulia, akimkabidhi Yusuph Richard, Mshindi wa Samsung S3 kupitia 'raffle droo' iliyo fanyika katika chuo kikuu cha Dar es Salam.

Meneja mkuu wa kampuni ya Tigo, Diego Gutierrez alizindua INTERNET YENYE KASI ZAIDI TANZANIA, huduma hiyo yenye kasi ya 4G, ambayo kasi yake ni hadi 42Mbps itawawezesha wateja wa Tigo kuperuzi, kupakua na kupakia taarifa mbalimbali kwenye mtandao na kucheza gemu kwa haraka zaidi kuliko ilivyokuwa siku za nyuma.

Uzinduzi huo ulifanyika Ijumaa iliyopita kupitia teknologia ya mikutano kwa njia ya mtandao yaani ‘video conference’ iliyounganisha mikoa minne (4) kwa hotuba maalum iliyokuwa ikitolewa na Ndg. Gutierrez kutoka ofisini kwake makao makuu ya kampuni ya tigo Dar Es Salaam. Mikoa iliyoshiriki katika uzindizi huo ni pamoja na Dar es Salaam, Dodoma, Arusha na Morogoro

No comments:

Post a Comment