Waandamanaji wamejipanga kisawasawa, Wanatembea na Maduka ya bidhaa mbalimbali na huduma muhimu.
Maandamano ya wananchi dhidi ya serikali yaUturuki, yamechukua
sura mpya na kuenea karibu katika maeneo yote ya nchi hiyo. Ilielezwa
mwanzoni mwa kadhia hiyo kwamba, ukandamizaji mkubwa wa polisi dhidi ya
waandamanaji, ndio uliopelekea kushtadi machafuko na maandamano hayo.
Ukandamizaji wa polisi umekuwa wa kupindukia mpaka ambapo mbali na
kukosolewa na mashirika mbalimbali ya haki za binaadamu kote duniani,
pia umemlazimu Waziri Mkuu wa Uturuki Recep Tayyip Erdoğan kusema kuwa
unafaa kufanyiwa uchunguzi. Pamoja na kwamba, polisi ya Uturuki
imelazimika kupunguza makabiliano dhidi ya waandamanaji, lakini
maandamano hayo yaliyoanzia mjini Istanbul, ambao ni kitivo cha uchumi
wa nchi hiyo, taratibu yameenea hata katika miji mingine ukiwemo mji
mkuu Ankara na miji mingine muhimu kama vile, Konya na Izmir.
Aidha maandamano hayo yamewafanya raia katika baadhi ya nchi za dunia
kufanya maandamano yenye lengo la kuyaunga mkono maandamano ya wananchi
wa Uturuki. Pamoja na hali hiyo, Recep Tayyip Erdoğan, amesisitizia
azma yake ya kuendelea na mpango wake wa kuharibu bustani ya Gezi mjini
Istanbul na kuweka mahala hapo kituo cha kibiashara. Kuhusiana na suala
hilo wapinzani wanasema kuwa jambo lililowafanya kumiminika barabarani
ni kiburi cha serikali ya Erdoğan cha kufumbia macho matakwa ya
wananchi. Erdoğan ambaye kwa miaka kadhaa sasa anatambulika na vyama vya
upinzani na fikra za waliowengi nchini Uturuki, kuwa mtu jeuri na
dikteta, hivi sasa anakabiliwa na upinzani mkali wa wananchi. Upinzani
huo unatajwa kuwa haujawahi kuonekana katika historia ya nchi hiyo. Hata
katika migogoro ya kiuchumi iliyowahi kutokea nchini Uturuki katika
muongo wa 90 Miladia, hakukushuhudiwa maandamano makubwa mithili ya yale
yanayoshuhudiwa sasa nchini humo.
Ni kwa ajili hiyo ndio maana duru mbalimbali za kisiasa nchini
Uturuki na ulimwenguni kwa ujumla zikajikita katika kuakisi radiamali na
hasira za wananchi wa nchi hiyo. Baadhi ya duru hizo zinaamini kuwa,
jamii ya Waturuki imekuwa ikikabiliwa na hali mbaya katika kipindi chote
cha utawala wa chama cha 'Uadilifu na Maendeleo' kinachoongozwa na
Recep Tayyip Erdoğan. Duru hizo zinaamini pia kwamba, katika kipindi cha
utawala wa kijeshi nchini humo, Uturuki haikushuhudia hali mbaya kama
ya sasa. Wakati huo huo, duru nyingine za kisiasa zinaamini kuwa, hasira
za wananchi wa nchi hiyo, zimetokana na hatua ya kupuuzwa upinzani wao
dhidi ya uingiliaji wa serikali ya Ankara katika mgogoro wa Syria.
Kwa upande wake Bülent esin, Mkuu wa chama cha Wafanyakazi nchini
Uturuki amesema kama ninavyomnukuu: "Kile kinachojiri nchini Uturuki ni
upinzani dhidi ya udikteta wa miaka 11 na siasa mbaya za chama cha
Uadilifu na Maendeleo hususan kuhusiana na Syria." Mwisho wa kunukuu.
Kwa mtazamo wa wapinzani, hatua ya serikali ya Ankara ya kuyaunga mkono
makundi ya kigaidi nchini Syria na kufuata siasa za kuzusha mifarakano
katika nchi hiyo na huko Iraq, ni sababu kuu iliyoibua vitendo vya
kigaidi na mifarakano ya kikabila na kimadhehebu katika nchi hizo.
Kupata habari zaidi juu ya sababu zilizopelekea maandamano hayo makubwa ambayo hayajawahi kutokea nchini Uturuki bofya link hii http://www.guardian.co.uk/world/blog/2013/jun/04/turkey-protests-whats-happening-open-thread
No comments:
Post a Comment