Wakati
tunapofikiria juu ya faida na vikwazo vya kutatua matatizo ya uratibu wa jamii
kupitia taratibu za masoko, ni muhimu kuzitupilia mbali baadhi ya Hoja za Uongo
zilizozoeleka. Ninaposema Hoja za Uongo
ninamaanisha maneno ambayo kutokana na ukweli ulio dhahiri/ au usio na nguo hupita hivihivi bila
hata ya kuwa na haja ya kuhoji au kuhitaji uthibitisho. Ni mambo unayoweza kuyasikia redioni, kutoka
kwa marafiki, kutoka kwa wanasiasa yanayoelekea tu kuwa hewani. Yanarudiwarudiwa kana kwamba ndiyo aina
mojawapo ya maneno ya hekima. Hatari iliyoko ni kwamba, kwa sababu yameenea
sana, hayafanyiwi uchunguzi wa kina.
Hicho ndicho ninachopendekeza kukifanya hapa.
Mara nyingi,
lakini si mara zote, hoja za uongo hizo huenezwa na wale ambao wako kinyume na
Masoko Huria. Machache katika hayo
huenezwa na wale ambao labda wana hamu ya kupindukia kuhusu masoko huria.
Zifuatazo
ndizo hizo hoja za uongo ishirini zikiwa zimegawanywa katika makundi manne:
ü Ukosoaji
wa Kimaadili
ü Ukosoaji
wa Kiuchumi
ü Ukosoaji
Chotara wa Kimaadili Kiuchumi; na
ü Utetezi
Uliokithiri.
Ukosoaji
wa Kimaadili
1.
Masoko ni Potovu au kinyume na Maadili
Masoko
huwafanya watu wafikirie tu kuhusu kupata faida, safi na rahisi `kabisa. Hakuna suala la maadili katika ubadilishanaji
wa soko, hakuna jitihada za makusudi zinazoelekezwa katika kutambua utofauti
wetu kama wanadamu: Uwezo wetu wa kufikiri
si tu kitu kilicho na manufaa kwetu, bali kuhusu kilicho sahihi na kisicho
sahihi, kinachofaa kulingana na maadili
na kisichofaa kimaadili.
Madai yaliyo ya uwongo ndiyo magumu
hata kuyawaza. Ili
mabadilishano yaweze kufanyika lazima
pawepo na heshima ya haki. Watu
wanaojihusisha na biashara ya ubadilishanaji hutofautiana na wale ambao kazi yao ni kuchukua tu; wale
wanaoshughulika na ubadilishanaji huwa wanaheshimu madai ya kweli ya watu
wengine. Sababu inayowafanya watu
wajishughulishe na biashara ya ubadilishanaji ni kwamba kwanza wanataka kile
walicho nacho wengine lakini wanazuiliwa na sheria na maaadili ili wasikichukue hivihivi tu. Ubadilishanaji ni kitendo cha kuhamisha
raslimali kutoka sehemu moja kwenda sehemu nyingine; hii ina maana kwamba kila
ubadilishanaji hupimwa kwa kuzingatia msingi, kwa maana hiyo, kama
hakutafanyika ubadilishanaji, pande mbili zinazohusika zitabakia na kile
walichonacho. Mfumo wa ubadilishanaji
unahitaji misingi imara ya haki. Bila
kuwa na hiyo misingi imara ya kimaadili na kisheria haiwezekani kuwa na
ubadilishanaji.
Hata hivyo, Masoko hayajengwi tu juu
ya kuheshimu haki. Hujengwa pia juu ya
uwezo wa wanadamu wa kuzingatia sio tu matamanio yao, bali matamanio ya watu wengine, kujiweka
kwenye nafasi ya wengine. Mtu mwenye
mgahawa asiyejali wanachokitaka wateja wake biashara yake haiwezi kudumu. Kama wageni wataugua kutokana na chakula walichokula
hawawezi kurudi tena kula hapo. Kama chakula hakiwaridhishi, hawatarudi tena. Yeye mwenyewe atashindwa kuendelea na
biashara. Masoko hutoa vivutio kwa washiriki kujiweka kwenye nafasi ya wengine,
kuangalia mahitaji yao, na kujaribu kuyaona
mambo kama vile wayaonavyo wao.
Masoko ndiyo njia mbadala katika
kutumia nguvu.
2.
Masoko hukuza Uchoyo na Ubinafsi
Watu
walioko sokoni wanajaribu tu kutafuta bei iliyo ya chini kadiri iwezekanavyo au
kupata faida iliyo kubwa zaidi. Kwa
maana hiyo, wanachochewa zaidi na uchoyo na ubinafsi, na siyo kuwajali wengine.
Masoko hayakuzi wala hayapunguzi
uchoyo au ubinafsi. Badala yake
yanasababisha wale walio waungwana zaidi pamoja na walio wachoyo au wabinafsi
zaidi kuendeleza makusudi yao
katika hali ya amani. Wale ambao hutoa
maisha yao yote kwa ajili ya kuwasaidia wengine
hutumia utafutaji masoko kuendeleza makusudi yao,
kama walivyo wale ambao hulenga kujiongezea akiba ya mali nyingi. Baadhi ya hawa wanaolenga kujiongezea mali,
hufanya hivyo kusudi wawasaidie wengine baada ya kujiongezea uwezo. George Soros na Bill Gates ndiyo mfano mzuri
wa hao wanaojilimbikizia mali kwa faida yao na wengine vilevile; wao huchuma
fedha nyingi angalau kwa kiasi fulani ili waweza kujiongezea uwezo wa
kuwasaidia wengine kupitia kwenye mifuko yao mikubwa ya miradi ya hisani.
Mama Teresa hupenda kutumia mbinu
hizihizi za masoko kwa ajili ya kutumia mali
alizonazo kuwalisha, kuwavisha, na kuwafariji watu wengi sana.
Masoko huwasaidia hao kupata bei za chini kabisa za blanketi, chakula,
na madawa kwa ajili ya kuwahudumia wale wanaohitaji msaada wao. Masoko huwezesha utafutaji wa mali
ambayo huweza kutumiwa kwa ajili ya kuwasaidia wasiojiweza na kuwaunga mkono
wanaotoa misaada kujengewa uwezo zaidi wa kuwasaidia wengine. Masoko hutoa fursa kwa wahisani kufanya kazi yao kwa ufanisi zaidi.
Kosa la wengi ni pale tunapobainisha
makusudi ya watu na kuyaunganisha na matakwa yao “binafsi”. Makusudi ya watu walio wengi katika kutafuta
soko huwa ni kwa ajili yao
wenyewe; hata hivyo pamoja na hayo bado tunajishughulisha na matakwa ya wengine
– familia zetu, marafiki, majirani, hata wageni kabisa ambao kamwe hatuwezi
tukakutana nao tena. Na kama ilivyodokezwa hapo juu, ni kweli kwamba masoko
huwasaidia watu kujali mahitaji ya wengine, hii ikiwa ni pamoja na mahitaji ya
wageni tusiowajua kabisa.
Kama
ambavyo imekuwa ikisemwa mara nyingi, msingi mkubwa wa jamii ya wanadamu siyo
upendo wala urafiki. Upendo na urafiki
ni matunda ya kufaidiana unaotokana na ushirikiano, uwe katika kundi dogo au
makundi makubwa. Bila kuwa na tabia ya
kufaidika kila upande, jamii isingekuwepo.
Bila huko kusaidika kila upande kati ya mtu na mtu, basi kilicho kizuri
kwa Tomasi kitakuwa kibaya kwa Juni, ama kinyume na kamwe wasingeweza kuwa
washirika katika lolote, wasingeweza kuwa marafiki, wala kufanya shughuli
pamoja. Ushirikiano huboreshwa kwa kiasi
kikubwa na masoko, ambayo husababisha ushirikiano hata kati ya wale ambao
hawafahamiani sio wa dini wala lugha moja, na ambao hawawezi kukutana
kamwe. Ile hali ya kuwa na uhakika wa
faida kubwa kutokana na biashara na uwezeshaji wa kibiashara inayofanywa na
kuwepo kwa Haki ya kumiliki mali iliyo thabiti kisheria husababisha kupendana
miongoni mwa watu wasiofahamiana, upendo na urafiki hadi nje ya mipaka.
Ukosoaji wa
Kiuchumi
3. Kutegemea Masoko Husababisha Ukiritimba
Bila
serikali kuingilia kati, kutegemea soko huria kungesababisha makampuni makubwa
machache kuhodhi biashara ya kuuza bidhaa zote.
Kwa kawaida, masoko husababisha kuhodhi mali, wakati ambapo wazalishaji
wadogo wanabanwa wanasalimu amri kwa makampuni makubwa ambayo hulenga tu kupata
faida iliyo kubwa; na ndiyo maana serikali hulazimika kufuata matakwa ya walio
wengi kwa kuhakikisha inapambana na uhodhi wa mali.
Serikali zinaweza – na zimekuwa
zikifanya hivyo mara nyingi kuachia uhodhi kwa kuwapendelea watu binafsi au
makundi; yaani huwakataza wengine wasijiingize kwenye soko ili tu washindane kama ilivyo desturi ya wateja. Hiyo ndiyo maana ya uhodhi. Uhodhi unaweza ukaachiwa wakala wa serikali yenyewe (kama
ilivyo katika kuhodhi huduma za posta katika nchi nyingi), anaweza akapewa mwenye kampuni kwa upendeleo
maalumu, akapewa familia, au mtu fulani.
Je, masoko huria huendeleza mchakato
wa kuhodhi? Kuna sababu ndogo ama hakuna
sababu nzuri ya kufikiri hivyo na kuna sababu nyingi zaidi za kutokufikiri
hivyo kabisa. Masoko huria hujengwa
kwenye misingi ya uhuru wa watu kuingia sokoni, kujitoa sokoni kwa
uhuru, na kununua kutoka kwa ama kumuuzia yeyote wanayemtaka kama
wapendavyo. Kama
makampuni yaliyo katika biashara yenye uhuru wa kuingia wakipata faida iliyo
zaidi ya wastani, zile faida huwavutia washindani kuja kushindania hizo faida
ili nao waweze kuzichukua. Baadhi ya
vitabu vya kiuchumi vinatoa maelezo ya mazingira ya kinadharia tete ambapo hali
fulani za masoko husababisha “kodi isiyobadilikabadilika” hii ina maana kwamba
pato linakuwa kubwa kutokana na chaguo bora zaidi, kinachoelezwa kama kile ambacho raslimali hukizalisha katika matumizi
mengine. Lakini mifano halisi ni vigumu
kupatikana; licha ya mifano isiyoridhisha kama
vile umilikaji wa raslimali za kipekee (kwa mfano Mchoro uliochorwa na
Ralmbrandt). Kinyume chake, rekodi za
kihistoria zimejaa mifano kadha wa kadha ambapo serikali zimewapa upendeleo
maalumu kwa wale wanaowaunga mkono.
Uhuru wa kuingia sokoni na uhuru wa
kuchagua ununue kwa nani hukuza matakwa ya wateja kwa kuondoa zile faida za
muda ambazo huzifaidi wale wanaokuwa wa kwanza kununua bidhaa. Kinyume chake,
kuipa serikali nguvu ya kupanga nani anapaswa ama hapaswi kutoa bidhaa na
huduma husababisha uhodhi – halisi, hata uhodhi uliothibitika kihistoria ambao
una madhara kwa watumiaji wa mwisho ambao pia unaharibu nguvu za uzalishaji za
mwanadamu ulio msingi wa mafanikio ya binadamu. Kama
masoko mara zote yaliweza kupelekea kuwepo kwa uhodhi tusingetarajia kuona watu
wengi kiasi hicho wakiiendea serikali ili iwape uhodhi kwa hasara ya washindani
walio dhaifu na wateja wao. Badala yake
wangeweza tu kuwapata wahodhi wao kupitia sokoni.
Siku zote ni vizuri kukumbuka kwamba
serikali yenyewe, kama ilivyo, inatafuta fursa
ya kuendeleza uhodhi, ndiyo tafsiri ya kitaalamu kwa tabia ya serikali pale
inapotumia nguvu katika eneo fulani la kijiografia. Kwa nini tutarajie huo uhodhi kuwa wa
kupatana na ushindani kuliko soko lenyewe, ambao hutafsiriwa na uhuru wa
kushindana?
4.
Masoko Hutegemea Taarifa Iliyo Sahihi, Ikiitaka Kanuni ya
Serikali ihakikishe Taarifa Muhimu Inapatikana
Ili
masoko yaweza kuwa katika ushindani mzuri, wadau wote sokoni wanapaswa kuwa
wamepata taarifa sahihi kuhusu madhara yanayoweza kuwakumba kutokana na matendo
yao. Ikiwa baadhi watakuwa na taarifa sahihi zaidi
kuliko mengine, hizo tofauti zitapelekea kuwepo na matokeo mabaya. Serikali lazima iingilie kati kwa kutoa
taarifa ambazo masoko yanapaswa kuwa nazo, na kuweka mazingira bora zaidi yenye
mafanikio na haki.
Taarifa, kama
kilivyo kitu kingine chochote cha thamani tukitafutacho ni gharama kukipata,
lazima tutoe kitu cha thamani ili tupate taarifa iliyo sahihi na kwa wingi
zaidi. Taarifa yenyewe kama
ilivyo ni bidhaa inayopitia mchakato wa ubadilishanaji kuhusu masoko; kwa
mfano, tunanunua vitabu ambavyo vina taarifa kwa sababu tunathamini taarifa
iliyoko kitabuni kuliko tunavyothamini kile tunachokitoa badala yake. Ili yawe
katika ushindani ulio imara zaidi, masoko hayahitaji taarifa sahihi kama ambavyo Demokrasia zinavyohitaji. Dhana iliyozoeleka kwamba taarifa ni gharama
kwa wadau na masoko, lakini sio gharama kwa wanasiasa wale wanaojishughulisha
na siasa sio sahihi kwa namna inayoweza kuleta madhara makubwa sana. Sio wanasiasa wala wapiga kura walio na
taarifa iliyo sahihi zaidi. Ukweli ni
kwamba, wanasiasa pamoja na wapiga kura wana motisha ndogo ya kupata taarifa
iliyo sahihi kuliko wadau wa masoko kwa kuwa hawatumii fedha zao wenyewe. Kwa mfano, wanapotumia fedha kutoka kwenye
mfuko wa umma, wanasiasa hawana motisha ya kuwa makini au kutafuta taarifa
iliyo sahihi na kama wanavyotakiwa kufanya
watu ambao wanatumia fedha zao wenyewe.
Hoja ya watu wengi kwa serikali
kuingilia kati inatokana na mapungufu ya kitaarifa kati ya watumiaji na
watoa huduma za kitaaluma. Kwa kawaida, madaktari wanakuwa na maarifa
zaidi kuliko wagonjwa katika masuala ya madawa ya kidaktari; ndiyo maana
tunakwenda kwa madaktari badala ya kujitibu wenyewe. Ni kutokana na sababu hizo inadaiwa
kwamba watumiaji hawana namna ya kujua
ni madaktari gani wana ujuzi zaidi, au kama wanapata matibabu yaliyo sahihi, au
kama wanalipa gharama kubwa zaidi. Kupewa leseni na serikali kunaweza
kuchukuliwa kuwa ndiyo jibu; kwa kutoa leseni mara nyingine inasemekana kwamba
watu watahakikishiwa kwamba daktari huyu ana sifa zinazohitajika, anamudu kazi
yake, ni muadilifu. Uthibitisho
unaotokana na utafiti juu ya utoaji leseni ya udaktari na taaluma nyingine,
hata hivyo unaonyesha kinyume kabisa.
Wakati ambapo masoko huwa na kawaida ya kutoa madaraja ya uthibitisho;
kupewa leseni kuna matokeo pande zote mbili, hivyo kama
hujapewa itaeleweka tu. Vilevile ni
jambo la kawaida kwa mtu kunyang’anywa
ama kufutiwa leseni ikiwa mhusika atajihusisha na matendo yaliyo
“kinyume na maadili ya kitaaluma”. Ikiwa ni pamoja na matangazo! Lakini
matangazo ni njia mojawapo zinazotumiwa na masoko kutoa taarifa kuhusu
upatikanaji wa bidhaa na huduma, kuhusu viwango vya ubora, na kuhusu bei. Utoaji leseni si suluhisho la mapungufu ya taarifa; bali ndiyo chanzo
chake.
5. Masoko Huwa na Ushindani Madhubuti Pale tu Idadi
Kubwa ya Watu Wenye Taarifa Sahihi Wanapobadilishana Bidhaa Mchanganyiko
Masoko yaliyo imara ambayo matokeo huboreshwa na faida
kupunguzwa, yanaongozwa na kanuni kwamba hakuna mtu yeyote anayetakiwa kupanga
bei, hii ina maana kwamba, hakuna mnunuzi au mwuzaji kwa kuingia kwake au
kutoka kwake atakayeathiri bei. Katika
soko lililo imara sana kiushindani, hakuna mnunuzi mmoja anayeweza kubadilisha matokeo
ya bei zilizopo. Bidhaa zote zinafanana
na taarifa kuhusu bidhaa na bei haina gharama lakini masoko halisi sio ya
ushindani wenye manufaa, ndiyo maana serikali inapaswa kuingilia kati na
kurekebisha mambo.
Mifano ya
kidhahania ya maingiliano ya kiuchumi inaweza kutusaidia, lakini pale ambapo
maneno yaliyosanifiwa kiufundi kama “ubora” yakiwa yameongezwa kwenye
yanayofikirika kidhahania uharibifu mkubwa unaweza kufanyika. Pale ambapo hali fulani ya masoko imeelezwa
kuwa ushindano “bora” na kitu kingine chochote kitakuwa “sio bora” hivyo
kinahitaji kuboreshwa, labda na wakala fulani nje ya masoko. Kwa kweli, ushindani “bora” ni suala tu la
mfano wa kiakili, ambapo kutoka hapo tunaweza kupata taarifa fulani za kweli,
kama vile nafasi ya faida katika kutoa mwelekeo wa raslimali (ambapo ikiwa iko
juu ya wastani, washindani watahamisha raslimali ili waongeze bidhaa sokoni,
kupunguza bei, na kupunguza faida) na nafasi ya hali isiyotabirika katika kutoa
mwelekeo wa ulazima wa kushikilia fedha taslimu (kwa kuwa kama taarifa ingekuwa
haina gharama, kila mmoja angeweza kuwekeza fedha zake na kupanga iweze
kutolewa pale ambapo atahitaji kuwekeza, kutokana na hilo tunaweza kuhitimisha
kwamba kuwepo kwa fedha taslimu ni sura halisi ya kutokuwa na taarifa sahihi). Ushindani “bora” sio njia ya kutuongoza
kuelekea kwenye uboreshaji masoko; badala yake ni neno lililochaguliwa kidhaifu
kwa ajili ya mfano wa kiakili wa michakato ya masoko ambao hutokana na nadharia
za hali halisi za masoko kiushindani duniani.
Ili serikali
iweze kuwa wakala wa kusaidia masoko yaweze kufikia kwenye “ubora” unaotakiwa
tungetegemea kuona serikali pia ina sera “bora” za demokrasia makini ambapo
idadi kubwa ya wapiga kura na wagombea hawawezi kuathiri mwelekeo mzuri wa
kisera, kwa kuwa sera zote zinafanana, na kwa hiyo taarifa kuhusu gharama na
faida za sera hazina gharama. Hata
hivyo, bahati mbaya hali halisi sivyo ilivyo.
Njia za
kisayansi za kuchagua sera zinazofaa zaidi zinaelekeza kwamba uchaguzi wa sera
sahihi lazima utokane na zile sera zilizopo tayari. Kwa kuwa uchaguzi wa kisiasa na ule wa masoko
vyote kwa pamoja kama vilivyokuwa hapo havikuwa na “ubora”, uchaguzi mzuri
hauna budi uzingatie vigezo linganifu na michakato “bora” ya masoko na ya
michakato ya kisiasa.
Masoko
yanayozingatia hali halisi hubuni njia mbalimbali za kutoa taarifa na
ushirikiano wenye manufaa miongoni mwa wadau wa soko. Masoko hutoa mwongozo kwa ajili ya watu
kupata taarifa ikiwa ni pamoja na aina iliyo bora ya ushirikiano. Matangazo ya biashara, Taasisi za ukopeshaji
fedha, heshima ubadilishanaji bidhaa, Masoko ya Hisa, Bodi za Uidhinishaji na
taasisi mbalimbali hujitokeza ndani ya masoko ili tu kuwezesha ushirikiano wa
kibiashara kwa manufaa anuwai kati ya mnunuzi na mwuzaji. Badala ya kutupilia mbali masoko kwa sababu
tu hazina ubora unaohitajika, hatuna budi tukatafuta njia mbadala za kuboresha
hali ya maisha ya mwanadamu.
Hatimaye,
ushindani kwa tafsiri unaeleweka vizuri zaidi sio kama sifa ya soko, ila ni
mchakato wa tabia ya kutokuridhika na hali duni. Wakati wajasiriamali
wanapokuwa huru kuingia kwenye soko kushindana na wengine na wateja kuchagua
kutoka miongoni mwa wazalishaji, ushindani miongoni mwa wazalishaji kwa ajili
ya tabia ya wateja hupelekea kuboresha tabia ya ushindani kwa wateja husika.
6. Masoko
Hayana Uwezekano wa Kuzalisha Bidhaa kwa Ajili ya Umma wote
Kama mimi nakula “tufaha”, na wewe huwezi kula; ulaji wa
“tufaha” ni hali ya ushindani. Kama
ninaonyesha mkanda wa video na sitaki watu wengine wauone, itanilazimu kutumia
fedha ili kujenga kuta ili kuwadhibiti wale wasiolipa wasiweze kuuona. Vivyo hivyo zipo bidhaa ambazo, ulaji wake
hauhitaji ushindani na hapohapo kula kwa kujitenga huhusisha gharama; haviwezi
kuzalishwa sokoni kwa kuwa kila mmoja
anayo shauku ya kuwangojea wengine wazalishe.
Kama utazalisha kiasi cha kutosha, mimi nitaweza kutumia tu; kwa hivyo
mimi sina shauku ya kukizalisha. Hali
hii ndiyo ilivyo hata kwako. Ile hali ya
kuzalisha kwa wingi ukilenga manufaa ya umma wote, lazima iwe ni serikali ndiyo
inaweza kuzalisha kama njia pekee ya kuhakikisha upatikanaji wake. Bidhaa hizi sio tu hujumuisha ulinzi na
usalama pamoja na mfumo wa kisheria, bali pia Elimu, Usafirishaji, Huduma za
Afya, na huduma nyinginezo za msingi.
Masoko hayapaswi kamwe kutegemewa kuwa ndio yanapaswa kuzalisha bidhaa
za aina hii, kwa sababu wale waliozoea bure wangekimbilia hapo na kuwazidi wale
wanaolipa, wasingekuwepo wanaotupa kabisa.
Ndiyo maana ni serikali pekee yenye dhamana ya kuzalisha bidhaa hizo.
Suala la
uhalali wa serikali kuwa mzalishaji bidhaa kwa ajili ya umma ni mojawapo ya
hoja za kiuchumi zisizozingatiwa kabisa.
Suala la kwamba bidhaa zina ushindani au la katika utumiaji wake
halitokani na aina ya bidhaa husika; ila hutegemea uwingi wa watu wanaotumia
bidhaa husika: Bwawa la kuogelea linaweza kuwa halina ushindani kwa watu
wawili, ila likawa na ushindani mkubwa kwa watu mia mbili. Na gharama za kuzuia wengine wasitumie bidhaa
husika ni zilezile kwa bidhaa zote ziwe kwa bidhaa za wote au za
binafsi,gharama ya umma au ya binafsi: kama nataka kukuzuia wewe usile tufaha
zangu, ni lazima nichukue hatua fulani ya kuzilinda kama kuzungushia
ukuta. Bidhaa nyingi zisizo na ushindani
katika kuzitumia, kama vile kuangalia mchezo wa soka (kama wewe unauangalia
mchezo huu haina maana kwamba mimi siwezi kuuangalia, vilevile), hutolewa kwa
sababu tu wajasiriamali wamewekeza kwa njia fulani za kuwatenga wale wasiopenda
kulipia huduma hiyo.
Licha ya
kutokuwa na sura halisi ya bidhaa, huduma nyingi zinazodaiwa kuwa za umma ni
taswira ya maamuzi ya kisiasa ambayo bidhaa zinapatikana katika misingi ya
kuwapatia wengi na pia pasipo gharama.
Kama serikali itaruhusu bidhaa kwa kufuata “misingi ya bure” si rahisi kwa wafanyabiashara kuruhusu hiyo
“Misingi ya bure” kwa maana ya usafirishaji wa “bure” ambao ungetegemea uwe
katika ushindani. Lakini tambua ya kwamba hiyo “misingi ya bure” si bure kabisa
kwa kuwa gharama zinalipwa kupitia kodi
(ambayo ina aina mbaya zaidi ya watu kufurahia matunda ya mfumo huu, ujulikanao
kama jela), na vilevile kukosekana kwa upangaji bei ndiyo sababu ya msingi ya
kuwa na mifumo duni ya miundombinu ikiwemo barabara nyembamba inayosababisha
foleni kubwa ya magari, ambayo ni kiashiro dhahiri cha njia zisizofaa za
mgawanyo wa raslimali haba (mfano barabara zenye upana wa kutosha) kwa ajili ya
matumizi yaliyo bora zaidi. Kwa kweli,
mwelekeo duniani umekuwa wa mpango wa kulipia miundombinu ya barabara
ulimwenguni kote, ndio uliopelekea kupunguwa kwa mijadala juu ya serikali kulipia
gharama za huduma za barabara.
Bidhaa
nyingi ambazo zinadaiwa kutowezekana kuuzwa kwa faida zimekuwa au kwa sasa,
zimeanza kulipiwa gharama kuanzia umeme, hadi elimu, polisi, hadi usafirishaji,
ambayo inadhihirisha kwamba madai ya kutumiwa kwa umma bila kulipia si halali. Hoja iliyopo kila mahali kwamba baadhi ya
huduma zinaweza tu kutolewa na serikali ni kuwa yapo masuala yaliyo “nje ya
mipaka” ambayo hayawezi kupangiwa bei.
Kwa hivyo, elimu inayotolewa kote – si tu hunufaisha umma wote kwa
ujumla licha ya watu wachache walio na elimu tayari, wanaodai kuhalalisha
utoaji wa serikali na ugharimiaji kupitia mapato ya kodi. Lakini licha ya manufaa kwa wengi, ambayo
yanaweza kuwa makubwa au madogo, manufaa kwa watu wenye elimu ni makubwa kwao
kiasi kwamba hushawishi uwekezaji wa kutosha katika elimu. Manufaa ya umma si lazima yaondoe dhana ya
wasiopenda kulipia gharama. Kwa kweli,
kama utafiti mwingi unavyoonyesha leo, ni kwamba ikiwa serikali itachukua
jukumu la kuhodhi na kutoa elimu kwa umma (bure), basi lazima itashindwa
kuwasaidia walio maskini, ambao nao wanaelewa umuhimu wa elimu, na wanawekeza
sehemu kubwa ya mapato yao katika kuwasomesha watoto wao.
Mwishoni, ni
vizuri ikakumbukwa kwamba karibu kila hoja inayodai kutokuwezekana kwa
uzalishaji wa madhubuti wa bidhaa za umma kupitia masoko hutumika sawa kwa
nguvu kabisa angalau – na mara nyingi kwa nguvu zaidi katika uwezekano wa kuwa
serikali itazalisha bidhaa za umma. Kule
tu kuwepo kwa uendeshaji wa serikali kwa njia ya haki na kufuata utawala wa
sheria tayari yenyewe ni huduma ya umma; hii ina maana kwamba, kutumiwa kwa
manufaa yake hakuhitaji ushindani (angalau miongoni mwa wananchi) na ingekuwa
gharama zaidi kuwabagua wale wasiochangia huduma katika kuiendeleza huduma hiyo
kwa mfano – (wapiga kura makini) huwezi ukawazuia wasinufaike na huduma
zilizopo. Vivutio vilivyopo kati ya wanasiasa na wapiga kura kuunda serikali
yenye haki na inayofaa si vikubwa sana, hasa pale vinapolinganishwa na
vilivyopo kati ya wajasiriamali na watumiaji wanaopaswa kununua bidhaa kwa
ushirikiano katika soko. Hii haina maana kwamba serikali isijihusishe kabisa na
jukumu la uzalishaji wa bidhaa za umma, bali ihakikishe wananchi hawaibebeshi serikali mizigo mizito
ya kuwajibika na uzalishaji bidhaa na huduma.
Ukweli ni kwamba, kadiri serikali inavyobebeshwa majukumu mengi zaidi,
ndivyo inavyoshindwa kuzalisha hizo bidhaa za umma, kama vile suala la ulinzi
wa haki za raia wake dhidi ya uvamizi, jambo ambalo lingeiletea manufaa
makubwa.
7. Masoko Hayafanyi Vizuri
(au Hayana Ufanisi) Pale Kunapokuwa
na Mazingira Hasi au Chanya
Masoko hufanikiwa zaidi pale ambapo hatua za utekelezaji
hubebwa na wale wanaohusika na kutoa maamuzi.
Ikiwa watu watanufaika tu bila kuchangia katika mchakato wa jinsi ya
kuyafikia hayo manufaa, basi masoko yatashindwa kufanya kazi yake vizuri katika
viwango vilivyokusudiwa. Vilevile, kama
watu watapokea “manufaa hasi”, yaani, kama watapata madhara, na hizo gharama
kutokuzingatiwa katika maamuzi ya kuzalisha bidhaa masoko yatawanufaisha wengine na wengine huishia
kubeba gharama kubwa, kwa kuwa mwingine ataishia kulipia gharama tu.
Kule kuwepo
tu kwa mazingira hatarishi hakutoshi kuipa uhalali serikali kubeba baadhi ya
shughuli ama kutupilia mbali maamuzi binafsi.
Nguo zinazoendana na wakati au malezi mazuri huleta mazingira nufaishi
mengi, kwa kuwa wengi hupenda kuwaona watu wanavaa vizuri au watu waliolelewa
katika maadili mazuri, lakini hiyo haitoshi bado kuwa sababu ya kuigeuzia
serikali wajibu wa kutoa huduma ya kutengeneza nguo au malezi mazuri. Kuwa na bustani nzuri, uchoraji ramani
nzuri za nyumba, na shughuli nyingi
mbalimbali huleta mazingira nufaishi kwa baadhi ya watu, lakini watu huchukua
jukumu la kupendezesha bustani na majengo yao kwa namna inayofanana. Katika mifano yote hiyo, faida inayowaangukia
wazalishaji peke yao – ukiwemo msukumo wa wale ambao yale mazingira nufaishi
yamewagusa moja kwa moja – inatosha kuwahamasisha wazalishe bidhaa hizo. Katika
mifano mingine kama vile utoaji wa huduma ya utangazaji wa televisheni na
radio, huduma ya umma “imeunganishiwa”
kwenye utoaji wa huduma nyinginezo kama vile matangazo ya biashara kwa ajili ya
makampuni; njia mbalimbali za kuzalisha huduma za Umma ni kubwa kama vile
walivyo wajasiriamali wengi wanaozalisha huduma/ bidhaa husika.
Kwa kawaida,
hata hivyo ni kule kuwepo kwa uzalishaji holela
unaoathiri jamii moja kwa moja, ndio husababisha watu wahoji umuhimu au uhalali
wa taratibu huru za masoko. Uchafuzi wa
mazingira ndio mfano unaotolewa mara nyingi.
Ikiwa mzalishaji anaweza akazalisha bidhaa kwa faida naye anafanya hivyo
kwa sababu anawabebesha wengine gharama za uzalishaji ambao hawakuridhia kuwa
sehemu ya mchakato huo wa uzalishaji, kwa mfano, kwa kutupa moshi mzito hewani
ama kemikali kwenye mto, anaweza kabisa akafanya hivyo. Wale watu wanaovuta hiyo hewa iliyochafuliwa
au wale wanaokunywa maji yenye uchafu wa kemikali ndio wanaobeba gharama
zitokanazo na ule uzalishaji wakati ambapo mzalishaji yule anapata faida ya
kuuza zile bidhaa alizozalisha. Tatizo
lililopo katika mifano hii, siyo kwamba masoko yameshindwa kazi yake, bali ni
kwamba hayapo kabisa. Masoko huweka misingi yake kwenye raslimali kwa hivyo
hayawezi kufanya kazi yake vizuri kama haifanyi kazi wakati sheria ya
hakimiliki haijatekelezwa. Masuala ya
uchafuzi wa mazingira au uchafuzi wa hewa si masuala ya kushindwa kwa masoko,
bali kushindwa kwa serikali kufafanua na kutetea hakimiliki ya watu wengine
kama vile wale watu wanaovuta hewa chafu au maji yenye kemikali. Watu wanapoamua kuondoa huo uchafuzi – wana
haki ya kutetea haki yao, wanatetea haki zao kwa kuwazuia wachafuzi hao
wasichafue (mazingira, hewa na maji.
Mzalishaji anaweza akaweka kwa gharama zake mwenyewe mtambo ama
teknolojia inayozuia uchafuzi wa hewa, maji au kupunguza kwa viwango ambavyo havitaleta
madhara), au akaamua kuwalipa watu ili waweze kuondokana na madhara zaidi,
(labda kwa kuwapa sehemu nyingine nzuri ya kuishi), au aache kabisa kuendelea
kuzalisha bidhaa hiyo kwa sababu anaingilia haki za watu wengine ambao
wasingekubali haki zao kuingiliwa, kwa kuonyesha kwamba gharama zote kwa ujumla
ni kubwa kuliko faida. Ni hakimiliki
ndiyo inayofanya hayo mahesabu yafanyike; na hiyo ndiyo inawahimiza watu
wazingatie athari za matendo kwa wengine.
Ni masoko hayohayo, yaani, ni fursa ya kushiriki katika ubadilishanaji
huria wa haki, ambazo zinaruhusu pande zote mbalimbali kukokotoa gharama za
utekelezaji.
Masuala
yenye madhara kwa mwanadamu kama vile uchafuzi wa hewa au maji si dalili za
masoko kushindwa kufanya kazi yake bali ni kushindwa kwa serikali kutafsiri na kulinda sheria ya Hakimiliki
ambayo ndiyo msingi ambapo masoko huegemea ili kufanya kazi yake vizuri.
8. Kadiri Mfumo wa Maisha ya Jamii
Ulivyo Mbovu, Ndivyo Utakavyotegemea Masoko kwa Kiasi Kidogo Zaidi na Ndivyo
Utakavyohitaji Mwongozo wa Serikali
Kutegemea masoko kulikuwa kuzuri pale jamii ilipokuwa
haina utata, lakini kutokana na ukuaji wa haraka wa uchumi na mitandao ya
kijamii, serikali haina budi iiongoze jamii na kuratibu shughuli za watu kwa
wingi wao.
Kama kuna
ukweli wowote, kinyume chake ndiyo sahihi.
Kunapokuwa na mfumo rahisi wa maisha ya jamii kama vile kundi la
wawindaji au waokotaji, wanaweza kuongozwa kwa urahisi na kiongozi mwenye uwezo
wa kuhimiza utii lakini kadiri mahusiano ya kijamii yanavyozidi kuwa magumu
ndivyo kutegemea zaidi ubadilishanaji katika masoko huria kunavyokuwa umuhimu –
sio mdogo – zaidi. Mfumo uliochanganyika
wa maisha ya jamii unahitaji uratibu wa taarifa zaidi kuliko mtu yeyote mwenye
akili au kundi la watu wenye akili ambavyo wangeweza kuwamudu. Masoko yamebuni njia mbalimbali za kusambaza
taarifa kwa gharama zilizo nafuu; bei zimeunganisha taarifa kuhusu upatikanaji
wa bidhaa na huduma na soko la hizo bidhaa na huduma katika viwango ambavyo ni
vilinganifu kwa bidhaa na huduma mbalimbali, kwa namna iliyo rahisi zaidi
kuliko jinsi ambavyo urasimu wa serikali usingeweza kufanya. Hali kadhalika, bei hutafsiriwa
tofautitofauti kulingana na lugha, mila na desturi za jamii, makabila, dini na
kuruhusu watu kutumia fursa hiyo kwa manufaa ya maarifa waliyonayo watu
wasiofahamika walioko maili kadha wa kadha mbali na watu ambao kamwe hawawezi
kuwa na mahusiano yoyote nao. Kadiri
uchumi na jamii vinavyokuwa changamani ndivyo umuhimu wa kutegemea mifumu bora
ya masoko huria unavyoongezeka.
9. Masoko Hayafanyi Kazi
Vizuri katika Nchi Zinazoendelea
Masoko hufanya kazi vizuri zaidi katika nchi zilizo na
miundombinu iliyo bora na mifumo mizuri ya kisheria, lakini kunapokuwa hakuna,
basi nchi zinazoendelea haziwezi kumudu mbio za masoko. Katika hali hiyo, ni lazima serikali
isimamie, angalau mpaka pale miundombinu
madhubuti itakapokuwepo na mfumo mzuri wa kisheria ambao kwa pamoja huruhusu
masoko kufanyakazi yake vizuri zaidi.
Kwa ujumla,
maendeleo ya miundombinu ni taswira halisi ya utajiri uliolimbikizwa kupitia
kwenye fursa za masoko, siyo sharti la kuwepo kwa masoko, na kushindwa kufanya
kazi kwa mfumo wa kisheria ndiyo sababu iliyopelekea kuwa na masoko dhaifu,
lakini kushindwa huko kwa mfumo wa masoko ndiko kutasababisha kufanya
marekebisho katika mfumo wa kisheria ili uweze kuwa ndio msingi wa uendelezaji
wa mfumo bora wa masoko, sambamba na uimarishaji miundombinu na uboreshaji wa
mfumo mzuri wa kisheria. Njia pekee ya
kupata utajiri katika nchi zilizoendelea ni kwa kuunda misingi imara ya mfumo
wa kisheria na wa kitaasisi kwa ajili ya masoko huria ili kwamba wajasiriamali,
watumiaji, wawekezaji na wafanyakazi waweze kushirikiana vizuri na kwa uhuru
zaidi kuleta utajiri.
Nchi zote
zilizo tajiri kwa sasa, hapo mwanzoni zilikuwa masikini sana, baadhi hata
kumbukumbu zake bado hazijafutika.
Kinachohitaji ufafanuzi si umaskini, ambao ni hali ya asili ya
mwanadamu, ila ni utajiri. Utajiri hauna
budi ujengwe, na njia bora ya kuhakikisha fursa za utajiri zinajengwa ni kwa
kuwapa watu vivutio vya kufanya
hivyo. Hakuna mfumo ulio bora kuliko
masoko huria, uliojengwa juu ya misingi imara ya mfumo wa kisheria na
Hakimiliki, taasisi za kisheria zinazorahisisha ubadilishanaji bidhaa/huduma,
uliofanikiwa sana kama huu, ndio uliogundulika kuwa bora zaidi kwa utoaji
vivutio kwa ajili ya kuleta utajiri.
Kuna njia moja kubwa ya kuukimbia umaskini, nayo ndiyo hii njia ya
kuvuta utajiri kwa kupitia masoko huria.
Neno “nchi
inayoendelea” mara nyingi hutumiwa vibaya pale yanapozungumziwa mataifa ambayo
serikali zao zimekataa masoko kwa kuweka mbele kila kitu mikononi mwa
serikali. Mipango, kumiliki mali, njia
kuu za uchumi na biashara, kulinda mali za wananchi, pamoja na upendeleo
maalumu. Mataifa haya, kwa kweli hayaendelei
chochote.
Nchi
zinazoendelea ni zile ambazo, ama zinaanza kwenye mazingira tajiri au masikini,
zimeunda taasisi zinazotoa haki za kisheria, zinazozingatia Hakimiliki na
mikataba halali, masoko huria, na zilizopunguza mamlaka ya serikali kuingilia
bajeti, na nguvu za mamlaka ya serikali zilizowekewa mipaka.
10. Masoko
Hupelekea Mizunguko Yenye Madhara Makubwa kiuchumi kama “Anguko kubwa la uchumi
Kutegemea upepo wa masoko kupindukia husababisha
mizunguko ya “Kukua sana kiuchumi pamoja na kufilisika”, pale ambapo
mwekezaji hujiamini kupita kiasi, hali
hiyo hupelekea Ustawi mkubwa katika uwekezaji ambayo lazima ifuatiwe na
kupungua kwa uzalishaji, kukosekana kwa ajira, na hali mbaya ya uchumi hutokea.
Mara
nyingine tabia za uchumi za “kukua kwa haraka” na “kushuka” hulaumiwa kwa
kutegemea zaidi masoko. Ushahidi, hata
hivyo ni kwamba kuzalisha zaidi ya kiwango kinachotakiwa si tabia mojawapo ya
masoko, wakati bidhaa na huduma nyingi zinapozalishwa, bei hujipanga vizuri na
matokeo yake ndiyo kuongezeka kwa ubora wa maisha ya watu katika nyanja zote,
na siyo kwa “maisha kuwa duni”. Wakati
kiwanda hiki au kile kikipanua uzalishaji wake zaidi ya uwezo wa masoko
kuhimili uendelevu wa faida, ndipo faida hupelekea raslimali kuelekezwa kwenye
maeneo mengine ya shughuli zilizopo.
Hakuna sababu za asili katika masoko kwa kujisahihisha huko kutokea
kwenye viwanda vyote; kwa kweli, huku ni kujichanganya (kwa kuwa kama uwekezaji
utachukuliwa) kutoka kwa wote na kuelekezwa tena kwa wote, hii haina maana
kwamba umeondolewa kutoka kwa wote).
Hata hivyo,
vipindi virefu vya kukosekana kwa ajira vinawezekana pale ambapo serikali
zinapotosha mifumo ya upangaji bei kupitia kwenye tabia chafu ya kuvuruga
mifumo ya fedha, kosa la kisera ambalo
mara nyingi linachanganywa na ruzuku kwa ajili ya viwanda ambavyo vinaelekea
kushindwa uzalishaji, na mishahara pamoja na udhibiti wa bei ambavyo huzuia
masoko yasijipanue hivyo kurefusha kipindi cha ukosefu wa ajira. Hayo ndiyo yaliyotokea wakati Uchumi wa Dunia
Uliposhuka sana kuanzia mwaka 1929 hadi mwishoni mwa Vita vya Pili vya Dunia,
jambo ambalo wachumi (kama vile mshindi wa Tuzo ya Nobeli, Milton Friedman)
walionya kuwa ndio ulisababishwa na kusinyaa kulikoambatana ghafla na kubanwa
kwa utoaji wa fedha na Serikali ya Marekani kwa ajili tu ya kutimiza malengo ya
kisiasa yaliyokuwa yamepangwa. Hatimaye,
kusinyaa na kubanwa huko kwa utoaji wa fedha kukafuatiwa na kuongezeka kwa hali
ya kukumbatia na kulinda mfumo uliopo kiasi ambacho dunia nzuri ilikumbwa na
hali ngumu ya uchumi na hali hiyo ilizidishwa kuwa mbaya zaidi na programu za Sheria ya Kufufua uchumi wa
Taifa, hasa Programu zilizolenga kupandisha bei za mazao ya shamba (kwa
kuharibu kiasi kikubwa cha mazao yatokanayo na kilimo na kuzuia usambazaji
holela), pamoja na “Programu nyingine mpya za kibiashara” ambazo zililenga
katika kuzuia mawimbi ya masoko yasiweza kusahihisha madhara makubwa
yaliyotokana na makosa ya sera za serikali.
Maanguko mabaya zaidi ya hivi karibuni ya kushuka kwa thamani ya pesa,
kama vile yale yaliyotokea Urusi mwaka 1997, yamesababishwa na kukosa umakini
katika sera za ubadilishaji fedha ambazo zilitoa ishara kwa wawekezaji. Mawimbi ya masoko yalisahihisha kushindwa
kisera kwa serikali, lakini mchakato huu ulikumbwa na upinzani mkubwa; chanzo
cha upinzani huo hakikuwa dawa iliyoponya ugonjwa ule, lakini uliweza kuponya
ugonjwa mbaya wa sera mbovu za kifedha na viwango vya ubadilishaji fedha
uliofanywa na serikali ambayo ndiyo
chanzo cha matatizo yote.
Kwa
kupitishwa kwa sera makini za kifedha na mamlaka za kifedha za serikali, tabia
hizo mbovu zimeanza kufutika taratibu. Pale ambapo kuna nguvu za urekebishaji zinazoletwa na
michakato ya masoko, matokeo yake yamekuwa mazuri ikiwa ni pamoja na kupungua
kwa kasi za kushuka kwa uchumi, ni kukua kuliko endelevu kwa uchumi wa zile
nchi zinazofuata sera za uhuru wa kibiashara, udhibiti mzuri wa bajeti na
kuzingatia utawala wa sheria.
11. Kutegemea
Masoko Kupita Kiasi ni Kubaya Kama Kulivyo Kutegemea mno Ujamaa: Kilicho Bora
ni Uchumi Mchanganyiko
Watu wengi wanajua kwamba si busara kuweka mayai yako yote kwenye kapu
moja: wawekezaji makini watatumia mbinu tofautitofauti na ni hekima kutumia
“sera zinazoendana na mabadiliko mbalimbali” vilevile, ikiwa na maana kwamba ni
mchanganyiko wa ujamaa na masoko.
Wawekezaji makini, wasiokuwa na taarifa sahihi wanaweza
kuchuja sera zao dhidi ya hatari. Kama bidhaa mojawapo itashuka nyingine
inaweza kupanda, hivyo kusababisha hasara kwa faida iliyopatikana. Kadiri muda unavyokwenda, mbinu mbalimbali
zilizoratibiwa vizuri kisera, lazima zitaleta faida iliyokusudiwa. Lakini sera hazifanyi kazi hivyo. Baadhi ya sera zimejaribiwa tena na tena
lakini zimeshindwa; wakati ambapo nyingine zimejaribiwa na zimefanikiwa. Isingeleta maana kuwa na “muundo wa uwekezaji
unaokubaliana na uanuwai” unaoundwa na bidhaa za makampuni ambazo zinajulikana
kwamba zimeshindwa kazi na bidhaa za makampuni yanayojulikana kwamba
yanaendelea kufanikiwa; sababu ya msingi kwa ajili ya “Muundo wa uanuwai”
unaoendana na mabadiliko ni kwamba huwezi kuwa na maarifa maalumu kuhusu ni
mampuni yapi yenye uwezekano mkubwa wa kufanikiwa ama yale yenye uwezekano
mkubwa wa kutofanikiwa.
Tafiti za miongo kadha wa kadha kuhusu takwimu za
kiuchumi zilizofanywa na chuo cha Fraser cha Canada na mtandao mpana wa taasisi
zimedhihirisha kuwepo kwa utegemezi mkubwa wa nguvu za soko unaopelekea kipato
kikubwa kwa kila mtu, kukua uchumi kwa kasi, kupungua kwa tatizo la ukosefu wa
ajira, kuongezeka kwa umri wa mtu kuishi, kupungua kwa vifo vya watoto wadogo,
kupungua kwa ajira ya watoto, kuongezeka kwa uhakika wa maji safi, afya ya
jamii ukiwemo uboreshaji wa nyanja mbalimbali za maisha kama vile utunzaji
mazingira, utawala bora, kupungua kwa tatizo la rushwa na kuongezeka kwa
uwajibikaji kidemokrasia. Masoko huria
huleta matokeo mazuri.
Zaidi ya hayo, hakuna mfumo wa uendeshaji “wenye mizania
wianifu” katika barabara. Kuingilia kwa
serikali suala la masoko lazima kutasababisha upotoshaji na hata migongano,
ambayo baadaye hutumiwa kama visingizio, kwa ajili ya afya zaidi, kwa hiyo
kuipindisha sera kwenda upande mmoja au mwingine. Kwa mfano sera ya fedha zinazowekwa kwa faida
isiyo makini, ambayo huongeza upatikanaji wa fedha kwa haraka zaidi kuliko
unavyokuwa, itasababisha kupanda kwa bei.
Historia imeonyesha mara kwa mara kwamba wanasiasa wana tabia ya
kushughulikia, sio kwa kulaumu sera zao zisizo makini, bali wanalaumu hali
“mbaya ya kiuchumi” au wanawalaumu watu “wapotoshaji waliokosa uzalendo”, nao
huweka mipango ya kudhibiti bei ya bidhaa. Wakati watu wanapokataa bei
zisirekebishwe kwa uzalishaji na mahitaji (kwa mfano wa hili ni kuongezwa kwa
upatikanaji wa fedha ambayo huwa na kawaida ya kusababisha thamani ya fedha,
inayopimwa kutokana na bei ya bidhaa kushuka), matokeo yake ni kuadimika kwa
bidhaa na huduma, kwa kuwa watu wengi watahitaji kununua bidhaa adimu kwa bei
ya chini kuliko ile ya bei halisi sokoni jambo ambalo wazalishaji hawatakuwa
tayari kulikubali kwa kuwa bei hiyo itakuwa haiwapi faida. Kwa kuongezea, kukosekana kwa masoko huria
hupelekea watu kuhamia kwenye masoko yasiyo rasmi ambapo kuna rushwa za
chinichini, pamoja na ukiukwaji mwingine wa utawala wa sheria. Mchanganyiko wa Matokeo ya kuadimika kwa
bidhaa na rushwa kutawala, hupelekea tabia mbovu zaidi ya kutwaa madaraka kwa
nguvu Madhara ya kubuni “sera mbadala”
ambayo imethibitishwa kuwa ni sera mbovu ni kuuzorotesha uchumi, kukaribisha
rushwa, na zaidi ni kuhalifu demokrasia ya kikatiba.
Ukosoaji
wa Maadili Mchanganyiko/Kiuchumi
12. Masoko
Husababisha Hali ya Kutokuwepo Usawa Kuliko Michakato Isiyo ya Kimasoko
Kwa mujibu wa maana yake, masoko huongezea nguvu ya ziada
juu ya uwezo wa kutimiza matakwa ya watumiaji, na kwa kuwa uwezo unatofautiana,
vivyo hivyo mapato nayo hutofautiana.
Mbali na hilo, kwa maana halisi, ujamaa ni hali ya kuwepo kwa usawa,
hivyo kila hatua inayoelekezwa kwenye ujamaa ni hatua inayoelekezwa kwenye
usawa.
Ikiwa
tunataka kuelewa mahusiano kati ya sera na matokeo ni vizuri akilini mwetu
ikaeleweka kwamba suala la mali ni dhana ya kisheria wakati ambapo utajiri ni
dhana ya kiuchumi. Haya mawili huwa yana kawaida ya kuchanganywa, lakini yanapaswa kutofautishwa. Michakato ya
masoko mara nyingi hugawanya tena utajiri kwa wingi mno. Kinyume chake, ugawanyaji tena wa raslimali
usiofuata matakwa ya wengi (unapofanywa na watu binafsi, unajulikana kama “wizi”)
hukatazwa chini ya kanuni inayoendesha soko huria, ambayo inahitaji kwamba mali
lazima ieleweke vizuri na iwe imewekewa ulinzi wa kisheria.
Masoko
yanaweza kugawanya tena utajiri, hata pale ambapo hatimiliki za mali zinabakia
kwenye mikono hiyohiyo. Kila wakati
thamani ya mali inapobadilika, (mali ambayo mwenye mali anayo hakimiliki)
utajiri wa mwenye mali nao hubadilika.
Mali iliyokuwa na thamani ya Yuro 600 jana inaweza kubadilika thamani
leo na kuwa Yuro 400 tu. Huko ni
kugawanywa tena kwa Yuro 200 za utajiri kupitia njia za masoko, ingawaje
hakukuwa na mgawanyo mpya wa mali. Kwa
hiyo, mara nyingi masoko husambaza utajiri na yakiwa katika mchakato huo huwapa
wenye mali vivutio kwa ajili ya kuongeza thamani za mali hizo ama kuzihamishia
kwa wale ambao wana utayari wa kufanya hivyo. Huko kusambazwa tena kwa utajiri
kunakozingatia kuongeza thamani ya jumla, huwakilisha kuhamishwa kwa utajiri
kwa kiwango kikubwa ambacho huwashangaza wanasiasa wengi. Kinyume chake, wakati ambapo michakato ya
masoko inapogawa tena utajiri, michakato
ya kisiasa hugawa tena mali, kwa kuzichukua kutoka mikononi mwa baadhi ya watu
na kuwagawia wengine, wakati mchakato huo ukiwa bado unaendelea, hufanya mali
hiyo kuwa na thamani ndogo zaidi, (mchakato) wa usambazaji huo ndio ambao
unaifanya mali kwa ujumla ikapungua thamani, maana yake, ni kuharibu utajiri.
Kadiri ugawaji tena unavyokuwa hauna
hautabiriki, ndivyo hasara ya utajiri inavyokuwa kubwa hali
inayosababishwa na hatari itokanayo na usambazaji wa mali.
Usawa ni
tabia ambayo inaweza kufikiwa kupitia viashiria mbalimbali, lakini kwa ujumla
si vyote. Kwa mfano, watu wote wanaweza
kuwa sawa mbele ya sheria, lakini kama hivyo ndivyo ilivyo, uwezekano ni mdogo
kwamba wote watakuwa na mvuto sawa kisiasa, kwa kuwa baadhi yao ambao watatumia
haki yao ya uhuru wa kutoa mawazo watakuwa wajasiri na nguvu zaidi kuliko
wengine, na kwa hivyo watakuwa na mvuto zaidi.
Vivyo hivyo, haki sawa ya kusambaza bidhaa na huduma kwenye masoko huria
si lazima ipelekee watu kuwa na mapato sawa, kwa kuwa baadhi wanaweza wasifanye
kazi kwa bidii au kwa saa nyingi (kwa sababu wanapenda mapato kuliko anasa)
kuliko wengine, ama wana stadi maalumu ambazo kwa wengine itawagharimu
kuzilipia ziada. Kwa upande mmoja wa
pazia, kujaribu kufanikisha kwa kutumia nguvu ya usawa kiuwezo ama usawa wa
kimapato kunamaanisha kwamba wengine watumie mamlaka yao zaidi au madaraka ya
kisiasa kuliko wengine, maana yake ni kuwa, mamlaka ya nguvu iliyo ya lazima
kusababisha kuleta matokeo hayo. Ili
kuleta mpangilio fulani wenye matokeo mazuri, mtu au kikundi cha watu lazima
kiwe na mtazamo wa kuona matokeo ya lazima kwa ajili kugawanya tena, kuona
upungufu hapa na ziada pale na hivyo kuweza kutoa huku na kupeleka kule. Kadiri ambavyo nguvu za kuanzisha matokeo
yaliyo sawa zinavyokuwa zimekabidhiwa kwa watu wanaoamikika, kama ilivyokuwa
kwa mfumo rasmi wa uchumi unaozingatia usawa kwa wote wa Umoja wa Kisovieti
wale watu wasio na mamlaka sawa kisiasa na kisheria walijikuta wakijaribu
kujipatia mapato au raslimali zisizo sawa. Mantiki pamoja na uzoefu vinaonyesha
kwamba jitihada za makusudi kupata mapato yaliyo sawa ama “yanayostahili”, ama
mpangilio mwingine wowote mbali na ule mpangilio wa kawaida unaosababishwa na
soko, huwa kwa kawaida unajichanganya, kwa sababu rahisi kwamba wale wenye
mamlaka ya kugawanya mali wanaitumia kujinufaisha wenyewe hivyo kugeuza
kutokuwa na usawa katika madaraka ya kisiasa kwa kutokuwa na usawa katika
maeneo mengine, iwe katika heshima, utajiri, au namna nyingine. Huo ndio
ulikuwa uzoefu walioupitia mataifa ya kijamaa, na ndiyo njia ambayo inafuatwa
na mataifa mengine kama vile Venezuela, ambapo madaraka yote yamelundikwa
mikononi mwa mtu mmoja, Hugo Chavez, ambaye amejichukulia madaraka makubwa
sana, kwa makusudi kwamba aweze kuleta usawa katika kuimiliki mali miongoni mwa
wananchi wote.
Kwa mujibu
wa takwimu ya Economic Freedon of the World Report ya 2006, kutegemea soko
huria hupatana kidhaifu na kukosekana kwa
usawa (kutoka katika uchumi usio huru kwenda kwenye uchuni ulio huru kabisa
duniani kote ukigawanywa katika qurtiles asilimia ya mapato yanayopokelewa na
watu maskini sana asilimia kumi hutofautiana kutoka katika wastani wa 2.2% hadi
wastani wa asilimia 2.5%), lakini hufanana kwa kiasi kikubwa na viwango vya
wastani vya mapato vya asilimia kumi ya
watu maskini sana (kutoka katika uchumi usio huru hadi kwenye uchumi ulio huru
kabisa duniani kote, ukigawa katika quartiles wastani wa viwango vya mapato
wanavyopata asilimia kumi ya watu
maskini sana ni dola za Kimarekani $ 826,
$ 1,186, $ 2,322, na $ 6,519).
Kutegemea sana masoko huonekana kuwa na matokeo madogo katika mgawanyo
wa mapato, lakini huongeza sana mapato ya watu maskini na inawezekana kabisa
kwamba wengi kati ya watu maskini kwa vyovyote vile wangeona hilo kuwa ni jambo
zuri kwao.
13. Masoko
Hayawezi Kutosheleza Mahitaji ya Mwanadamu kama vile Afya, Nyumba, Elimu, na
Chakula
Bidhaa hazina budi kusambazwa kulingana na kanuni
zinazokubalika kiasili. Masoko hugawanya
bidhaa kulingana na uwezo wa kulipia alionao mtu, lakini afya, nyumba, elimu,
chakula, na mahitaji mengine ya msingi ya mwanadamu kwa uhalisia wake kwa kuwa
ni mahitaji ya msingi, yanafanywa kugawanywa kulingana na mahitaji, na sio
uwezo wa kulipia alionao mtu.
Ikiwa masoko
yatafanya kazi nzuri ya kutosheleza mahitaji ya mwanadamu kuliko kanuni nyingine
kwa maana kwamba, kama watu wengi watafaidika na maisha bora katika kuwepo kwa
soko huria kuliko kuwepo chini ya ujamaa, inaonekana kwamba njia za mgawanyo
chini ya soko huria hufanya wajibu wake vizuri katika kutimiza kigezo cha
mahitaji, vilevile. Kama ilivyobainika
katika angalizo hapo juu, mapato ya watu masikini huwa yana kawaida ya kupanda
kwa kasi kulingana na kiwango cha uhuru wa soko huria, hii ina maana kwamba
watu masikini wanakuwa na raslimali nyingi zaidi kwa ajili ya kutosheleza
mahitaji yao. (Kwa kawaida, si mahitaji yote yana uhusiano wa moja kwa moja na
mapato, urafiki wa kweli na upendo, havina uhusiano huo kabisa. Lakini hakuna sababu ya msingi ya kufikiri
kwamba hayo yanagawanywa kwa usawa zaidi kwa taratibu za udhibiti au kwamba
yanaweza kugawanywa kwa njia hizo).
Aidha,
wakati ambapo madai ya “uhitaji” yana kawaida ya kutokuwa na msingi wa hoja,
kama yalivyo madai ya “uwezo”, utashi wa kulipa ni rahisi zaidi kuupima. Wakati watu wanaposhindania zabuni kwa fedha
zao wenyewe kwa ajili ya bidhaa na huduma, wanatuthibitishia jinsi
wanavyothamini bidhaa na huduma hizo kulinganisha na bidhaa na huduma
nyingine. Chakula ambacho kwa hakika ni
hitajio la msingi kuliko hata elimu na huduma ya afya hutolewa kwa utoshelevu
zaidi kupitia njia za masoko huria. Kwa
kweli katika nchi zile ambazo umiliki wa mali binafsi ulifutwa na nafasi yake
kuchukuliwa na serikali hadi suala la (masoko huria, matokeo yake yakawa ni baa
la njaa na ulaji wa nyama za watu. Soko
hutosheleza mahitaji muhimu ya mwanadamu kwa bidhaa nyingi zaidi, zikiwemo zile
bidhaa ambazo hulenga zaidi mahitaji ya msingi ya mwanadamu kuliko njia
nyingine zozote.
Utoshelevu
wa mahitaji unahitaji matumizi sahihi ya bidhaa adimu, hii ikiwa na maana
kwamba, lazima maamuzi sahihi yafanyike katika usambazaji wa bidhaa hizo. Mahali popote ambapo soko huria halijapewa
nafasi ya kujiendesha, mifumo mingine na vigezo vingine hutumika katika ugawaji
wa bidhaa adimu, kama vile ugawaji uliotawaliwa na urasimu, nguvu ya ushawishi
wa kisiasa, uanachama katika chama cha siasa, uhusiano wa karibu na rais au
wale walioko madarakani, au hongo na aina nyingine za rushwa. Ni vigumu kutokea kwamba vigezo hivyo vikawa
bora kuliko vile vinavyosababishwa na soko huria, wala kisingizio kwamba
vinaleta usawa zaidi; mara nyingi uzoefu unaonyesha kwamba ni kinyume kabisa.
14. Masoko Hujikita katika Kanuni
ya Mwenye Nguvu Ndiye
Anayefaidi
Kama ilivyo katika sheria ya mwituni, mwekundu kwenye
jino na kwenye kucha, sheria ya soko huria humaanisha mwenye nguvu ndiye
anayefaidi. Wale watu ambao hawawezi
kuzalisha kwa ubora wa hali ya juu kutosheleza mahitaji ya viwango vya soko
huangukia njiani na kukanyagwa na wengine.
Madai ya
kanuni ya nadharia kama vile “mwenye nguvu ndiye anayefaidi” tunaposoma habari
za mifumo ya viumbe hai na tunaposoma kuhusu mahusiano ya kimawasiliano
miongoni mwa jamii ya wanadamu hupelekea katika upotoshaji hadi pale
watakapobainisha hasa ni nani anayefaidi katika kila mfano wanaoutoa. Katika mfano wa elimu biolojia, ni mnyama husika
na uwezo alionao katika kuzaliana.
Sungura anayeliwa na paka kwa sababu tu si mwepesi wa kutoroka hawezi
tena kupata watoto. Sungura wenye kasi
zaidi ya wengine ndio watakaoweza kuzaliana kwa wingi zaidi. Kanuni hii inapotumiwa katika mabadiliko ya
jamii, hata hivyo hali ya kuendelea kuishi ni tofauti sana; sio mtu binafsi
tena bali ni aina ya mfumo wa mahusiano ya kimawasiliano ya jamii kama vile
mila, taasisi, au kampuni, ambayo huchaguliwa” katika mapambano ya kutafuta
mabadiliko. Wakati kampuni ya biashara
inapofilisika, “inakufa”, hii ni sawa na kusema, huo mfumo wa ushirika wa
(“kijamii” “hufa”, lakini hiyo haina maana ya kwamba wanadamu waliouunda
ushirika ule – kama wawekezaji, wamiliki, mameneja, waajiriwa, na kadhalika –
nao hufa vilevile. Mfumo ulio imara
zaidi huchukua nafasi ya mfumo usio imara.
Ushindani wa Masoko yanayotawaliwa na soko huria ni tofauti na
mashindano yaliyoko mwituni. Kule
mwituni wanyama hushindana kwa mnyama kumla mnyama mwingine, au kwa ajili ya
kuchukua nafasi ya mnyama mwingine. Katika soko, ni wajasiriamali na makampuni
ndio wanaoshindana wao kwa wao kwa haki ya kushirikiana na walaji na pia
wajasiriamali wengine na makampuni mengine.
Ushindani wa Masoko huria si mashindano kwa ajili ya kupata fursa ya
kuishi, bali ni mashindano kwa ajili ya fursa ya kushirikiana.
15. Soko Hushusha hadhi ya Utamaduni na Sanaa
Sanaa na utamaduni ndizo zenye mwitiko mkubwa kwa
vipengele vya nafsi ya mwanadamu, na kwa maana hiyo, haviwezi kuuzwa na
kununuliwa kama vile nyanya au vifungo vya shati. Kuiachia sanaa sokoni ni sawa
na kuiachia dini sokoni, ambako ni kuusaliti utu tuliourithi wa sanaa, kama ule
wa dini.
Licha ya
hayo, kadiri sanaa na utamaduni vinavyofunguliwa milango ya kuingizwa kwenye
mashindano ya soko la kimataifa, matokeo yake ni kung’olewa kwa misingi yake
kwa kuwa, mihimili ya asili hutupwa mbali kwa ajil ya bidii ya dola au yuro
ambazo zina nguvu za kuvuta watu kama za Mwenyezi Mungu.
Sehemu kubwa
ya sanaa imekuwa ikitengenezwa na itaendelea kutengenezwa kwa ajili ya
soko. Kwa kweli, kwa kiwango kikubwa,
historia ya sanaa imekuwa ndiyo historia ya ubunifu kupitia njia za masoko kupitia mahitaji ya teknolojia mpya, falsfa
mpya, mionjo mipya na mifumo mipya ya kiroho.
Sanaa, utamaduni na soko vimekuwa na mahusiano ya karibu mno kwa karne
nyingi. Wanamuziki hutoza kiingilio
kutoka kwa watu wanaoangalia maonyesho yao kama vile wauzaji wa mboga za majani
wanavyochukua fedha za mauzo au mafundi cherehani wanavyowalipisha wale watu
wanaowashonea vifungo kwenye suti zao.
Kwa kweli, kufungua milango kwa ajili ya soko la muziki, filamu, na aina
nyingine za sanaa kwa njia ya kubuni rekodi, kaseti, kanda za CD, DVD, na kwa
hivi karibuni mafaili ya “Times” na MP3, huwapelekea watu wengi zaidi kuwa na
mwanga mkubwa kuhusu sanaa nyingi mbalimbali, na pia kwa wasanii kupata fursa
za kujiongezea ujuzi mwingi zaidi, kubuni aina haibridi za sanaa, na kwa jinsi
hiyo kujiongezea mapato zaidi. Si ajabu
kabisa, kwamba kazi nyingi za sanaa zinazotengenezwa kwa mwaka haziwezi kudumu
bila kupitwa na wakati; na jambo hilo husababisha mtazamo potofu kwa upande wa
wale wanazoilaumu sanaa za kisasa kwamba ni za hali ya chini, ukilinganisha na
kazi za sanaa za miaka ya nyuma wanacholinganisha ni zile kazi za zamani zenye
ubora wa hali ya juu zilizochujwa,
kutokana na kazi zilizofanywa kwa miaka mia iliyopita na kuwa nyingi za sanaa
zilizotengenezwa katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita. Kama wangelijumuisha kazi zote ambazo
hazikuweza kuhimili ubora uliopo na unaoenda na wakati, na hazijakumbukwa, basi
hilo ulinganifu ungelionekana kuwa na tofauti kabisa.
Kile
kinachohitajika ili pawe na mwenye nguvu ndiye atawale kimsingi ni mchakato wa
ushindani wa soko huria la sanaa. Kule
kulinganisha kazi za kisasa za sanaa zilizotengenezwa katika ujumla wake na
kilicho bora kuliko zote kutoka karne zilizopita si kosa pekee wanalotenda watu
pale wanapotathmini soko la sanaa. Kosa
lingine wanalofanya watazamaji wote kutoka katika jamii zilizo tajiri ambao
wanazitembelea jamii masikini ni kule kuuchanganya umaskini wa hao wanajamii
maskini pamoja na tamaduni zao. Pale
ambapo watalii matajiri wanatembelea watu walioko katika nchi maskini ambazo
zinapiga hatua nzuri kiuchumi na wanawaona watu maskini wakiwa na simu za
mkononi (laputopu), wanajikuta wakijilaumu kwamba safari hii “haikuwa nzuri”
kama safari iliyotangulia. Kadiri watu
wanavyozidi kuwa matajiri kutokana na mahusiano ya kimawasiliano
yanayosababishwa na soko huria linalochangiwa zaidi na uchumi huria na
utandawazi, kama vile kuzuka kwa mawasiliano ya simu ya mkononi, wanaharakati
wa nchi tajiri wanaopinga utandawazi wanatoa shutuma kwamba maskini “wanaporwa”
utamaduni wao. Lakini ni kwa nini
ulinganishe utamaduni na umaskini?
Wajapani walivuka kutoka katika umaskini hadi kwenye utajiri mwingi na
ni vigumu kukubali kwamba ni wajapani walewale wanaofahamika kutokana na
matokeo hayo ya kushangaza. Ukweli ni
kwamba, utajiri wao mkubwa umesababisha kuenea kwa kasi kwa utamaduni wa
Kijapani duniani kote. Kule India kadiri
mapato yanavyozidi kuongezeka, kiwanda cha kutengenezea nguo za mitindo
mbalimbali ya kisasa, kimelazimika kugeukia mitindo asilia ya mavazi, kama vile
“sari”, pamoja na kwenda na yale yanayokubalika katika jamii, kuyaweka katika
hali ya kisasa zaidi na kuongezea kigezo cha uzuri wa umbo na mwonekano. Nchi ndogo ya Iceland imefanikiwa kudumisha
utamaduni wao wa sanaa ya fasihi na sanaa zao za maonyesho na filamu, kwa
sababu pato la mtu mmoja mmoja liko juu sana, hali ambayo imewafanya wawekeze
mali zao katika kuendeleza na kudumisha utamaduni wao.
Aidha,
ingawa amani za dini si kwa “ajili ya biashara”, jamii zilizo huru zina kawaida
ya kuipa dini misingi ileile – haki sawa na uhuru wa kuchagua – kama vilevile
ilivyo kwenye misingi ya soko huria.
Makanisa misikiti, masinagogi, na mahekalu hushindana wao kwa wao kwa
kutafuta waumini walio wengi zaidi na hata kuungwa mkono. Ni jambo la ajabu
kuona kwamba, zile nchi za Ulaya zinazotoa misaada kwa makanisa – msaada rasmi
wa serikali – ndizo zenye waumini wachache zaidi Kanisani, wakati ambapo nchi
zisizo na msaada rasmi na serikali ndizo zinakuwa na waumini wengi zaidi. Sababu yenyewe si ngumu kuielewa: Makanisa ambayo yana ushindani katika kutafuta
waumini lazima yatoe huduma zilizo adimu na muhimu kwa waumini wao – kama vile
sakramenti, huduma za kiroho, na komunyo – kwa waumini wao, na ukweli ni kwamba
kadiri viongozi wanavyojali zaidi mahitaji ya waumini wa hali hiyo husababisha
watu kupenda kujishughulisha zaidi na mambo ya kikanisa na kuhudhuria mara kwa
mara. Kwa kweli, ndiyo maana kanisa
lililojengwa kwa msaada wa serikali nchini Sweden liliomba liondolewe kutoka
katika hali ya kusaidiwa na serikali moja kwa moja mnamo mwaka 2,000; kwa kuwa
lilikosa mwitiko wa wanachama kutokana na urasimu wa serikali, kanisa lilijikuta
linakosa mshikamano wa moja kwa moja na waumini wake na hasa wale waumini walio
hai, na kwa hivyo lilikuwa linaelekea kufa kutokana na hali hiyo.
Hakuna hali
ya kupingana kati ya soko, sanaa na utamaduni.
Ubadilishanaji unaofanyika katika mchakato wa soko sio sawa na ujuzi wa
kisanaa au uboreshaji wa utamaduni, lakini ni kitendea kazi muhimu sana kwa
ajili ya kuviendeleza vyote viwili kwa pamoja.
16. Soko Huwanufaisha matajiri na Wenye Vipawa vya Asili
Matajiri wanazidi kuwa tajiri na maskini wanazidi kuwa
maskini. Ukitaka kupata pesa nyingi
zaidi, lazima uanze na kiwango kikubwa zaidi.
Katika mashindano ya soko la kupata faida kubwa, wale wanaoanza mbio
kabla ya wengine kufika haraka kwenye mstari wa umaliziaji katika mashindano.
Michakato ya
soko huria si sawa na mbio za riadha, ambapo kunakuwa na washindi na wale
wanaoshindwa. Wakati ambao pande mbili
zinapokubali kwa hiari yao wenyewe kubadilishana vitu vya thamani (katika
biashara), wanafanya hivyo kwa sababu wote wawili wanategemea watanufaika, haina
maana kwamba wanategemea mmoja wao atapoteza na mwingine apate. Mategemeo ni kwamba wote wawili lazima
wanufaike au wapate faida. Tofauti na
mashindano ya riadha katika biashara kama mmoja atafaidika, haina maana kwamba
mwingine lazima apoteze. Hapa suala la
msingi si “kumshinda” mwingine, bali ni kupata faida kutokana na ushirikiano wa
hiari wa kubadilishana; ili uweze kumshawishi mwingine afanye biashara na wewe,
huna budi kumpa kitu cha thamani cha kumnufaisha yeye, vilevile.
Kuzaliwa
katika hali ya utajiri kunaweza kuwa kwa manufaa, kitu ambacho wananchi walioko
katika nchi tajiri hawakitambui kama ambavyo wale wanaotoka nchi maskini
wanavyotamani kuhamia kwenye nchi zilizo tajiri; hawa waliozaliwa katika jamii
maskini wanaelewa manufaa ya kuishi katika jamii tajiri kuliko wale waliozaliwa
katika utajiri. Lakini katika soko
huria, huku kukiwa na uhuru wa kuingia na haki sawa kwa wanunuzi na wauzaji
wote, wale ambao walikuwa makini katika kukidhi mahitaji ya soko jana wanaweza
wasiwe makini tena kukidhi mahitaji ya soko kesho. Wanasayansi ya Jamii huuita
“Mzunguko wa watu walioelimika” ambao ndio sifa kubwa ya jamii zilizo huru; kuliko wasomi wanaobakia
hapohapo bila kwenda na mabadiliko wanajikita kwenye nguvu za kijeshi,
uanachama au mahusiano ya kikabila
ama ya kifamilia, watu walioelimika katika jamii zilizo huru – wakiwemo
wasanii walioelimika wanaozingatia utamaduni, wanasayansi walioelimika na
wachumi walioelimika – wako tayari kuwapokea wanachama wapya na mara chache
hurithisha uanachama kwa watoto wa wanachama ambao wengi wao huhama kutoka
tabaka la juu na kuwa kwenye tabaka la kati.
Jamii zilizo
tajiri zimejaa watu waliofanikiwa wengi ambao wameacha nchi zao ambapo soko
hudhibitiwa sana au huwekewa vikwazo kwa kuwapa upendeleo maalumu wenye uwezo,
kwa kulindana, na kwa ukiritimba na udhibiti wa biashara ambapo fursa za
kustawi katika soko la wazi hria huwa chache.
Wamelazimika kuziacha jamii hizo zilizo na rasilimali kidogo au zisizo
na kitu chochote kidogo na mafanikio katika jamii iliyo wazi zaidi na
iliyotumia vizuri fursa za soko huria, kama vile Marekani, Uingereza na
Kanada. Je, kulikuwa na tofauti gani
kati ya zile jamii walizoziacha na zile walizojiunga nazo? Jibu ni kwamba walifuata uhuru wa
kushindana kwa uhuru katika soko
huria. Inasikitisha kiasi gani kwa nchi
maskini kuhodhiwa biashara katika nchi zao kunakowapelekea wao kuzikimbia nchi
zao na kwenda nchi za nje, kwa maana
hiyo hawawezi kubaki katika nchi zao na kuwatajirisha majirani na marafiki zao
kwa kuweka ujuzi wa ujasiriamali wao katika vitendo.
Kwa ujumla,
katika nchi zenye soko huria, zaidi, fursa nyingi zinatengenezwa, si kwa ajili
ya kuwaridhisha matajiri na matakwa yao,
bali kwa kutimiza matakwa ya matabaka ya kati.
Kupanda ngazi kutoka Ford Motors hadi Sony hatimaye Wal-mart, Makampuni
makubwa, yanayotengeneza faida kubwa, ni yale ambayo kwa kawaida hutenga
kutosheleza mahitaji ya watu wa tabaka la chini na ya kati na siyo kwa kutosheleza matakwa ya
matajiri.
Kwa kawaida,
soko huria huwa na tabia ya mzunguko wa watu walioelimika, bila kuwa na hata
mtu mmoja aliyehakikishiwa sehemu ya kuingia au anayezuiwa kuingia kwa bahati
mbaya kutokana na kuzaliwa. Dhana
kwamba, “tajiri anazidi kuwa tajiri na maskini anazidi kuwa maskini” inafanya kazi, si katika mazingira ya soko
huria ila katika ukiritimba wa biashara na mfumo wa kisiasa, ikiwa na maana
kwamba, ukaribu wa mtu na wenye madaraka makubwa ndio utakaomfungulia milango
mtu huyo kupata utajiri.
Katika mfumo
wa soko huria, uzoefu unaofanya kazi kila mahali ni kwamba matajiri wanafanya
vizuri lakini wanaweza wasidumu katika “utajiri” kulingana na hali ya maisha ya
Jamii zao) na maskini hugeuka kuwa matajiri zaidi huku wengi wao wakipanda
daraja na kuingia kwenye tabaka la kati na la juu. Wakati wowote ule, kwa ufafanuzi asilimia
ishirini (20%) ya idadi ya watu itakuwa katika kundi lenye mapato ya chini
zaidi na asilimia ishirini (20%) itakuwa katika kundi lenye mapato ya juu
zaidi. Na si lazima pia kwamba hivyo vipimo
(quintiles) vitapima kiasi hichohicho cha mapato kwa kuwa ya makundi yote
hupanda kadiri uchumi unavyokua au kwamba mgawanyo wa mapato utajazwa na watu
haohao. Makundi kulingana na mapato ni
kama vile vyumba katika hoteli au siti kwenye basi; yanajazwa na mtu fulani,
lakini si lazima kila wakati yatajazwa na watu haohao. Pale utafiti unapofanyika juu ya mgawanyo wa
mapato kwa kulinganisha na muda unavyokwenda, sehemu kubwa ya mabadiliko ya
mapato hudhihirika, huku idadi kubwa ya watu wakipanda na kushuka katika
mgawanyo wa mapato. Kitu cha msingi,
hata hivyo, ni kwamba uchumi wa masoko huria uliofanikiwa una kawaida ya
kuhakikisha mapato yote yanaongezeka, kutoka kima cha chini kabisa hadi kima
cha kabisa.
17. Bei zinapoachwa Kudhibitiwa na Kutawaliwa
na Nguvu za Masoko,
Zitapanda tu
Ukweli ni kwamba bei zinapoachwa zitawaliwe na nguvu za
masoko, bila udhibiti wa serikali, zitapanda tu, hii ina maana kwamba watu
watakuwa na uwezo mdogo wa kununua bidhaa.
Upangaji bei huria maana yake, ni jina lingine lenye maana ya bei ghali.
Bei ambazo
zinadhibitiwa chini ya kiwango cha bei halisi ya soko, huwa na kawaida ya
kupanda kiholela, angalau kwa kipindi cha muda mfupi, hasa pale zinapoachwa
bila kudhibitiwa. Lakini kuna hadithi
nyingi kuliko hali inavyoonekana kwa nje.
Mojawapo ni kwamba, baadhi ya bei zinazodhibitiwa huachiwa katika
kiwango cha bei ya soko, ili kwamba pale zitakapoachwa bila udhibiti zipate
kushika. Zaidi ya hayo, tunapoangalia
suala la bei za fedha zinazodhibitiwa kwa nguvu ya dola ni muhimu kukumbuka
kwamba fedha inayotolewa mezani wakati wa kununua kitu siyo gharama inayotolewa
na wale waliofanikiwa kununua bidhaa.
Kama bidhaa zingekuwa zinagawanywa kwa watu kupanga mistari, basi muda
ambao ungetumika katika kusubiri wakiwa katika mistari, ni sehemu ya gharama
ambayo watu wanapaswa kulipa ili wapate zile bidhaa. (Angalizo, hata hivyo, ule muda wa kusubiria
unawakilisha muda unaopotea ambao ni hasara, kwa kuwa siyo muda ambao unaweza
japo kuhamishiwa kwa wazalishaji ili kuwashawishi wapate kuzalisha bidhaa nyingi
zaidi kwa lengo la kutosheleza mahitaji ambayo bado hayajafikiwa). Kama viongozi wala rushwa wamekunjua mikono
yao, kuna malipo yanayofanyika kupitia chini ya meza ambayo lazima yaongezwe
kwenye malipo yale yanayofanyika juu ya meza.
Jumla ya malipo ya halali, hongo na muda unaotumika kusubiria kwenye
mstari wakati bei ya juu inapopangwa na serikali kwa ajili ya bidhaa na huduma
mara nyingi huwa ghali zaidi kuliko bei ambayo watu wangekubaliana kwa kupitia
katika soko huria. Hali kadhalika, fedha
zinazotumika kwa ajili ya kuhonga na muda unaotumiwa kusubiri katika mstari ni
hasara zinatumiwa na walaji lakini hazipokelewi na wazalishaji, kwa hiyo
hazitoi motisha kwa wazalishaji ili wazalishe zaidi ambapo wangepunguza uhaba
wanaoupata kutokana na udhibiti wa bei.
Wakati
ambapo bei za viwango vya fedha huongezeka kwa muda mfupi pale bei zinapoachwa
kudhibitiwa, matokeo yake ni kuongeza uzalishaji na kupunguza utumiaji ovyo na
rushwa huku tukiwa na hakika kwamba matokeo ya jumla ya bei halisi zinazopatikana
kwa kuangali bidhaa kama hitaji ya lazima, muda anaoutumia mtu kufanya kazi –
hupungua. Kiasi cha muda anachotumia mtu
kuhangaika kwa ajili ya kutafuta kipande cha mkate mwaka 1800 ni sehemu kubwa
ya siku yake nzima anayotumia katika kuhangaika; kwa kuwa mishahara imepanda
juu sana, kiasi cha muda wa mtu kufanyakazi ili kupata kipande cha mkate
umepungua hadi kufikia dakika chache katika nchi tajiri.
Baada ya
kupimwa kwa kutumia nguvukazi, bei za bidhaa nyingine zote zimeshuka kwa namna
ya kushangaza, isipokuwa: Kazi yenyewe.
Kadiri ufanisi wa kazi na mishahara inavyozidi kupanda, kulipia
nguvukazi huwa ni ghali zaidi, ndiyo sababu inayofanya matajiri katika nchi
maskini kila mahali wanafanya kazi (watumishi wa kazi), wakati ambapo matajiri
wakubwa kabisa katika nchi zilizo tajiri wanaona ni gharama nafuu kununua
mashine za kwa ajili ya kuosha nguo zao na vyombo vyao. Matokeo ya masoko huru ni kuanguka kwa bei za
kila kitu inapopimwa kwa kuangalia gharama za nguvukazi na kupanda kwa gharama
ya nguvukazi kwa ajili ya shughuli zozote zile.
18. Ubinafsishaji
na Mchakato wa Soko Huria Wakati wa Kipindi cha
baada ya
Ukomunisti kilikuwa Wala Rushwa Hali Ambayo
Inaonyesha
kwamba Masoko Yanasbabisha Rushwa
Kampeni za ubinafsishaji karibu wakati wote hazifuati
utaratibu (ni chafu). Ni mchezo mchafu
ambao huwapa rasilimali ya taifa watu wasio na maadili na wala rushwa na wenye
uchu wa madaraka. Mchezo wote wa ubinafsishaji
na mchakato wa soko huria ni mchafu na hauwakilishi chochote kizuri zaidi ya
wizi toka kwa watu.
Nchi
mbalimbali zilizokuwa chini ya mfumo wa kijamaa hapo awali ambazo zilibuni
kampeni za ubinasishaji zimekuwa na matokeo tofautitofauti. Baadhi ya nchi hizo zimefanikiwa kuunda
mipangilio bora ya masoko. Wengine wamejikuta wakirudia mfumo wa utawala wa
mabavu na wameshuhudia michakato ya “ubinafsishaji” imesababisha watu wachache
wenye nguvu wateule wakiwa wameshikilia usukani wa kuongoza serikali na
biashara kubwa za binafsi kama ulivyoibuka wa “Siloviki” nchini Urusi Uchafu uliotokana na mikono michafu
iliyonufaika na kutokana na mifumo mibovu ya ubinafsishaji ndio matokeo ya
kutokuwepo kwa taasisi za msingi katika masoko zaidi kikiwa ni utawala wa
sheria ambao ndio mhimili muhimu kwa ajili ya masoko. Uundwaji wa vyombo hivi si kazi rahisi hata
kidogo na hakuna mbinu ya jumla inayoweza kulifanikisha hilo ambalo linaweza
kutumika katika mazingira yote. Lakini
kushindwa kufanikisha uundwaji wa taasisi za utawala bora katika mazingira
fulanifulani si sababu ya msingi inayowazuia wasiweze kujaribu tena hata kwa
mfano wa Urusi, Mifumo mibovu ya ubinafsishaji iliyoanzishwa ilikuwa ni
maboresho tu kutokana na ukandamizaji uliosababishwa na utawala wa chama kimoja
iliyokuwepo awali na iliyokuja kuanguka kutokana na udhalimu wao wenyewe pamoja
na kukosekana kwa mipango sahihi.
“Ubinafsishaji”
pekee bila kuwepo kwa mifumo bora ya kisheria si sawa na uundwaji wa
masoko. Masoko hufanikiwa pale ambapo
kuna misingi imara ya kisheria; ubinafsishaji ulioshindikana siyo kushindwa kwa
masoko, ila ni kushindwa kwa serikali katika kuunda misingi ya kisheria kwa
ajili ya masoko.
Utetezi wenye Shauku Kupita Kiasi
19. Mahusiano yote Miongoni mwa Wanadamu
Yanaweza Kutafsiriwa
kama Mahusiano ya Kupanua Masoko
Shughuli zozote zile zinazofanyika ni kwa sababu watu
wanaozifanya hulenga kupata faida yao wenyewe.
Hata
kuwasaidia watu wengine ni kujipatia faida wewe mwenyewe, kama sivyo
usingelifanya hivyo. Urafiki na upendo
huwakilisha ubadilishanaji wa huduma kwa
manufa ya pande zote mbili, kama ilivyo (ni sawa na) watoto wanapobadilishana
magunia ya viazi. Licha ya hayo, mifumo
yote ya mawasiliano ya wanadamu inaweza kueleweka vizuri zaidi kama sehemu ya
kupanua wigo wa masoko, ikiwemo siasa, ambapo kura zinazotumika kama ishara ya
kubadilishana kati yake na ahadi zinazotolewa kwa ajili ya manufaa fulani, hata
na uhalifu, ambapo wahalifu na waathirika hubadilishana maneno, yanayotumika
wana mfano, “fedha zako au uhai wako “Tupe pesa vinginevyo tunataka uhai wako
“chagua kutupa pesa au uhai wako” “chagua moja kutupa pesa au uhai wako”.
Kulazimisha
matendo yote ya mwadamu na kuyaweka katika kusudi moja ni upotoshaji wa
makusudi ya mwanadamu.
Wazazi
hawafikirii faida yao wenyewe pale wanapojitoa sadaka kwa ajili ya watoto wao
au wanapowaokoa katika hatari fulani.
Wakati watu wanapoomba ili wapate wokovu au mwangaza wa kiroho, makusudi
yao sio sawa na pale wanaponunua nguo.
Kitu walichonacho wote kwa pamoja ni kwamba wote wana makusudi fulani,
na kwamba wanafanya jambo fulani ili kufanikisha kusudi fulani. Lakini haiwezi ikahitimishwa tu kwa mantiki
hiyo kwamba makusudi yao yana kiwango sawa ya kile kinachowavutia kutekeleza
kujiridhisha. Makusudi na nia zetu zinaweza
kuwa tofauti tunapokwenda sokoni kununua nyundo, tunapongia kwenye makumbusho
ya sanaa, tunapombusu mtoto mchanga, tunagundua kwamba makusudi yanatofautiana
sana, ambayo siyo yote yanaweza kuelezewa vizuri kama ilivyo katika suala la
kununua na kuuza sokoni.
Ni kweli
kwamba mbinu za nyenzo za kitaalamu zinaweza kutumiwa katika kuielewa na kuzipa
mwanga njia mbalimbali za mawasiliano ya kimahusiano. Dhana za kiuchumi, kwa
mfano, ambazo zinatumika katika kuelewesha ubadilishanaji katika masuala ya
masoko, inaweza kutumiwa vilevile kuelezea taaluma ya sayansi ya siasa au hata Dini. Hali ya kuchagua katika siasa inaweza kuwa na
hasara (gharama) na faida, kama ilivyo katika uchaguzi wa biashara, vyama vya
kisiasa au vikundi vya mafia vinaweza kulinganishwa na kampuni za Biashara
katika masoko. Lakini haina maana kwamba kwa kutumia mifano ya dhana hizo
lazima mifano hiyo iwe inafanana moja kwa moja kimaadili na kisheria. Mhalifu anayekupa nafasi ya kuchagua kati ya
kubaki na fedha zako au kuchagua uhai wako hawezi kufananishwa na mjasiriamali
anayekupa fursa ya kuchagua kati ya kubaki na hela yako ama kuitumia katika
kuinunulia bidhaa, kwa sababu iliyo wazi kwamba mhalifu anakulazimisha
katika maamuzi mawili ambayo yote una
haki kimaadili na kisheria, ambapo mjasiriamali anakupa haki ya kuchagua kati ya mambo mawili ambapo mojawapo
wewe ndiyo una haki au mamlaka ya kuchagua wakati huohuo jambo lingine hilo ni
yeye ndiye ana mamlaka nalo. Katika
mazingira ya mifano hii miwili unapaswa kufanya maamuzi na kuchagua la kufanya,
kwa makusudi fulani, lakini katika mfano ule wa kwanza yule mhalifu
amekulazimisha wewe kuchagua, wakati ambapo katika mfano wa pili yule
mjasiriamali amekupa tu fursa ya kuchagua; kwa hiyo yule wa kwanza amepunguza
haki yako, wakati wa pili anakupa fursa ya kuongeza haki hiyo, kwa kukupa kitu
ambacho huna lakini ambacho unaweza
kukithamani ubadilishe na kitu ambacho unacho lakini unaweza kukipa
thamani ndogo.
Mahusiano
yote ya mwanadamu hayawezi kupunguzwa thamani hadi kufikia namna ambayo masoko yanachukulia
mahusiano yake, kwa kiwango cha chini kabisa, mahusiano yale ambayo yanahusisha
“ubadilishanaji” usio wa hiari ni ya tofauti sana, ikiwa sababu inayohusisha
hasara ya pamoja na thamani, badala ya fursa za kuongeza thamani.
20. Masoko Yanaweza Kutatua Matatizo Yote Bila
Serikali
Serikali ina umilisi mdogo kiasi kwamba haiwezi kufanya
chochote kwa usahihi. Somo kuu la masoko ni kwamba lazima tuidhoofishe serikali
wakati wote, kwa sababu serikali kwa maneno rahisi ni kinyume na hupingana na
masoko). Kadiri unavyokuwa na serikali
isiyotumia nguvu ndivyo unavyoshamiri katika masoko.
Wale
wanaotambua manufaa ya masoko, wanapaswa kutambua kwa sehemu kubwa duniani,
pengine sehemu zote, tatizo la msingi si tu kwamba serikali zinafanya mambo
mengi mno, lakini pia hufanya sehemu ndogo sana katika kundi hilo la kwanza –
mambo ambayo serikali haipaswi kufanya, yanajumuisha A). Shughuli ambazo hazipaswi kufanywa na mtu
yeyote yule, kama vile usafishaji wa kikabila wizi wa Ardhi, na kuunda
upendeleo maalumu wa kisheria kwa watu wenye nguvu/wenye nazo/wasomi na B)
Mambo ambayo yangeweza au yanapaswa kufanywa kupitia katika mawasiliano ya
hiari kati ya makampuni na wajasiriamali katika masoko, kama vile utengenezaji
wa magari, uchapishaji wa magazeti, na kuendesha migahawa. Serikali inapaswa kuacha kujishughulisha na mambo hayo. Lakini pale wanapoacha kufanya shughuli
ambayo haipaswi serikali inapaswa kuanza kufanya baadhi ya shughuli kadhaa
ambazo kwa kweli zingeongeza haki na kuweka mazingira mazuri kwa ajili hasa ya
kutatua matatizo ambapo kuna mahusiano ya karibu baina ya haya mawili.” Serikali ambazo hutumia rasilimali yao kwa
ajili ya kuendeshea viwanda vya magari au uchapishaji wa magazeti, au mbaya
zaidi – kutaifisha mali na kujenga misingi ya kisheria inayopendelea wachache –
yote haya hupunguza uwezo wao wa kutoa
huduma zenye thamani halisi ambazo serikali zina uwezo wa kuzitoa. Kwa mfano, serikali katika nchi maskini
zaidi, ni mara chache sana zinafanya kazi nzuri ya kutoa hati sahihi ya
kisheria (hatimiliki), achilia mbali suala la kuipata ile mali kutoka katika
mikono ya wengine. Mara nyingi, mifumo ya kisheria imekuwa mibovu, yenye utata,
na imekosa uhuru na ile hali ya kutokupendelea ambayo ni ya lazima kwa ajili ya
uwezeshaji wa mahusiano ya hiari katika mazingira ya kufanya biashara kwa
hiari.
Ili Masoko
yaweze kutoa mwongozo kwa ajili ya kuratibu jamii, Mali na mikataba lazima
iweze kuwekewa misingi mizuri ya kisheria.
Serikali inayoshindwa kutoa hizo huduma zenye manufaa kwa jamii huzuia
masoko yasishamiri. Serikali inaweza
kutimiza matakwa ya umma kwa kutumaini mamlaka yake kuunda mfumo bora wa sheria
na haki, siyo kwa ulegevu, ila ni kwa
kutumiza wajibu wake kwa mujibu wa sheria na wakati huo ijue kuheshimu mipaka
katika kutumia madaraka yake. Serikali
dhaifu si sawa na serikali inayoheshimu mipaka ya madaraka yake. Serikali dhaifu ambayo haiheshimu mipaka ya
madaraka yake inaweza kuwa hatari sana kwa sababu ifatanya mambo ambayo
haipaswi kufanya lakini pia inakuwa haina mamlaka ya kusimamia sheria inayo
kanuni za mwenendo wa haki na kutoa huduma ya hifadhi ya jamii, uhuru na mali
isiyohamishika ambavyo ni ya lazima kwa ajili ya ubadilishanaji huru na kuwepo
na kustawi kwa masoko huria. Masoko
huria si sawa na kutokuwapo kwa serikali.
Si kila mapinduzi huleta matokeo mazuri.
Masoko huria
hufanya kazi vizuri zaidi kwa kule kuwepo kwa serikali inayoongozwa kwa misingi
ya utawala bora na inayosimamia na kutekeleza utawala wa sheria bila upendeleo
katika uendeshaji wake.
Ni vizuri
ikakumbukwa pia kwamba yapo matatizo mengi ambayo yanapaswa kutatuliwa kwa
harakati za makusudi); haitoshi tu kusisitiza kwamba michakato ya masoko huria
itatatua matatizo yote. Kwa kweli, kama mshindi wa “tuzo ya Nobeli” mchumi
Ronald Coase, alivyoelezea katika kitabu chake cha Market and the Firm (Soko na
kampuni za biashara), makampuni huwa na kawaida ya kutegemea zaidi upangaji
mipango wa kimkakati na uratibu ili kufikia malengo ya pamoja, kuliko kutegemea
zaidi njia mbadala kwa ajili ya ubadilishanaji katika masoko, kwa kuwa kule tu
kwenda kufanya biashara kuna gharama zake.
Kila mkataba uliopangiliwa una gharama katika kuuingia, kwa mfano, ndiyo
maana mikataba ya muda mrefu hutumiwa ili kupunguza gharama za kufanya
mikataba. Katika makampuni ya biashara,
mikataba ya muda mrefu hutumiwa kama njia mbadala za ubadilishanaji wa papo kwa
papo, na unajumuisha mahusiano mema kazini, yanayozingatia kanuni, sheria na
tartibu za kazi), yanayohusisha mshikamano na kuzingatia usimamizi mzuri,
kuliko kutafuta tenda kwa ajili ya huduma ya aina fulani tu. Makampuni – ya Title Islands of Teram Work
and Planning – yana uwezo wa kufanikiwa kwa sababu wanaendesha shughuli zao kwa
kuzingatia mipango mipana inayohusisha masuala yanayoibuka bila kutarajiwa
kwenye ubadilishanaji katika soko huria.
Kosa kubwa walilokuwa wanafanya nchi zilizokuwa chini ya mfumo wa
kijamaa ni kujaribu kusimamia uchumi wote kana kwamba ni kampuni moja kubwa,
inaweza ikawa ni kosa hilohilo kutokutambua kwamba nafasi ya usimamizi na
mshikamano wa kufanya kazi kama timu una mipaka yake ndani ya mipango tofautitofauti
inayofanya kazi katika masoko huria.
Kwa kiwango
hichochicho, ambacho masoko yanaweza kutoa mwongozo wa ubunifu na usimamizi wa
kanuni za mwenendo wa uendeshaji wenye kuzingatia haki, wale wanaharakati wa
Masoko Huria wanapaswa kufanya hayohayo.
Kampuni Binafsi za Ulinzi mara nyingi zimekuwa Bora kuliko Polisi wa
Serikali (na hazitumii nguvu zaidi, kama si kwa sababu nyingine yoyote zaidi ya
kwamba gharama za utumiaji nguvu hazihamishiki kirahisi kwa “mtu wa tatu”.
Isipokuwa
serikali pekee inaweza kufanya hivyo; usuluhishi wa migogoro ya hiari mara
nyingi hufanikiwa zaidi kuliko kutumia mahakama. Lakini kutambua hilo ni kutambua wajibu
muhimu wa kanuni za uendeshaji katika uundwaji wa Masoko na, kwa namna hiyo,
kuunga mkono kanuni za sheria zinazolinda haki, kwamba zinatolewa na serikali
au na masoko huria, kuliko kuwa tu kinyume na serikali.
No comments:
Post a Comment