Angelina
Jolie
Angelina
Jolie na Mume wake Brad Pitt
Mcheza filamu mashuhuri duniani bibie Angelina Jolie amesema kwamba amekatwa matiti yake yote pamoja na kuondoa mfuko wake wa uzazi. Kwenye taarifa aliyoandika kwenye gazeti la New York Times, Bi Jolie amesema alifanyiwa uchunguzi wa celi zake na kugunduliwa kwamba alikuwa katika hatari kubwa sana ya kupata saratani ya matiti. Ndipo akaamua kukatwa matiti yake mawili.
Angelina mwenye umri wa miaka 37 na mama na watoto sita, alimpoteza mamake mzazi kutokana na maradhi ya saratani ya matiti. Anasema aliandika taarifa hiyo kuwahakikishia watoto wake kwamba hakuwa kwenye hatari ya kupata saratani tena. Kulingana na Jolie madaktari walisema kuwa uwezekano wake kupata Saratani ya matiti ni asilimia 87 huku akiwa na asilimia 50 uwezo wake wa kuugua Sarati ya mfuko wa uzazi. ''Niliamua kuchukua hatua mwenyewe ili kuzuia uwezekano wowote wa kuugua Saratani hiyo,'' alisema Jolie. Alisema kuwa shughuli hii ilianza mwezi Februari na kukamilika mwishoni mwa mwezi April.
Katika taarifa iliyoandikwa na Bi Jolie na yenye kichwa, 'Uamuzi wangu wa kimatibabu', Bi Jolie alieleza kuwa mamake alipambana na Saratani kwa miaka kumi na kufariki akiwa na umri wa miaka 56. Alisema kuwa alielewa fika kuwa siku moja atawahi kuugua Saratani na ndio maana akachukua uamuzi wa kufanyiwa upasuaji huo mgumu wa wiki tisa ambao ulihitaji kukatwa matiti.
Uwezekano wake wa kuugua saratani sasa umeshuka kutoka 87% hadi 5%. Alimsifu mumewe Brad Pitt, kwa kumuunga mkono na kumfariji kwa kila aliyopitia, na kusema kuwa ametulizwa na kuwa wanawe hawakupata lolote katika matokeo ya uchunguzi wa madaktari tangu kufanyiwa upasuaji. "ninahisi kuwa na nguvu kwa uamuzi niliofanya, na kwa kuwa ninasalia kuwa mwanamke hata baada ya kuondoa viungo hivyo,'' alisema Bi Jolie. "kwa mwanamke yeyote anayesoma maneno haya, natumai ataweza kujua kuwa wanaweza kufanya uamuzi.'' Muigizaji huyo, ambaye ameshinda tuzo nyingi kwa uigizaji wake, pia ni mtunzi wa filamu na mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa anayehusika na harakati za kibinadamu. Wakati alipokuwa anafanyiwa upasuaji, Bi Jolie alizuru Jamuhuri ya Kidremokrasia ya Congo pamoja na waziri wa mambo ya nje wa Uingereza William Hague.
No comments:
Post a Comment