Advertise with Us

Advertise with Us

DHall

DHall

Pages

June 23, 2013

Ushuhuda: Namna CCM inavyofanya ugaidi nchini!





HATI YA KIAPO.
[Made under Oaths (Judicial Proceedings) and Statutory Declaration Act, 1966]
Mimi ******************* S.L.P 163 Tarime Mkristo, mtu
mzima na mwenye akili timamu, ninaapa na kutamka kama ifuatavyo:-


  1. Kuwa mimi nilijiunga na Chama cha Mapinduzi toka 2003, na niliendelea kuwa Mwanachama mpaka tarehe 12 mwezi wa Septemba 2011 nilipoamua kwa hiari yangu binafsi pasi na kulazimishwa au kushinikizwa kwa namna yoyote na mtu yeyote kujiunga na Chama cha Demokrasia na Maendeleo na nilikabidhi kadi yangu ya uanachama,
  2. Kuwa katika wakati wote nilipokuwa mwanachama nilitumikia chama katika kitengo cha usalama wa chama (intelligence unit)
  3. Kwamba mnamo mwaka 2007 mimi nilikuwa ni miongoni mwa vijana tuliopelekwa Kawe jijini Dar es Salaam kwa ajili ya mafunzo ya kiusalama mwingine alijulikana kama Robert Mshana ambaye alikuwa mkufunzi wa mafunzo ya "green guards" wilaya ya Nzega ambaye baada ya kujiunga na Chadema akiwa Igunga siku chache baadaye alikamatwa na hajulikani alipelekwa wapi mpaka leo.
  4. K wamba baada ya kutoka Kawe tulipelekwa Dodoma na hapo mimi na wenzangu ndipo tulipoelezwa dhahiri na John Chiligati wakati huo akiwa kama katibu mwenezi wa C.C.M lengo la kupewa mafunzo yale, kuwa ni kwa ajili ya kulinda maslahi ya chama na kwamba mafunzo hayo yalikuwa yameandaliwa na chama cha Mapinduzi.
  5. Kwamba nia na madhumuni ya CCM ni kwamba kwa kutumia vijana ni lazima ishinde kwa vyovyote itakavyokuwa katika chaguzi mbalimbali ikiwemo kuiba kura kwa kupora visanduku vya kura ili upinzani usishinde au kuchukua nchi. Moja ya mbinu ya wizi ilikuwa ni kubadilisha masanduku ya kupigia kura yakiwa njiani, na hata mara nyingine tulilazimika kuwanywesha vil eo mawakala wa vyama vingine ili washindwe kuhimili kukaa muda mrefu wakiangalia uhesabuji wa kura, pia kuwahadaa mawakala kwa kuwafanya wajaze karatasi za matokeo kabla ya kutangazwa na zaidi kuahonga mawakala wa pesa ili wajiondoe katika kuwakilisha vyama vyao dakika za mwisho, mbinu hii hutumika sana maeneo ya vijijini.
  6. K wamba katika kutekeleza majukumu na maagizo ya Chama kila mara Kulipotokea uchaguzi tuliitwa na tulikabidhiwa silaha aina ya bastola mbazo tulikuwa tukikabidhiwa na mkurugenzi wa usalama wa C.C.M tuliyemfahamu kwa jina moja tu kama bwana MTENGA.
  7. Kwamba katika utekelezaji wa kuona kwamba C.C.M inashinda katika uchaguzi mdogo wa jimbo la Igunga, mnamo tarehe 10109/2011 tuliitwa na kukabidhiwa ten a Silaha iliyotengenezwa nchini China yenye yenye uwezo wa kubeba risasi 8 kwenye magazine yenye namba J 13 7 .
  8. K wamba silaha hizo zilikuwa zinatumika wakati maalumu hasa kipindi cha uchaguzi na chaguzi nyingine ndogo na mara baada ya kukamilika kwa zoezi husika tulikuwa na wajibu wa kuzirudisha kwa mkurugenzi wa usalama wa Chama ambaye ofisi zake ziko Dodoma.
  9. Kwamba katika mchakato huo wa kupewa silaha na kuzitumia kwa maslahi ya C.C.M tulikuwa tukishirikiana na maafisa usalama na maaskari wengine mbalimbali katika kutekeleza hayo na kuhakikisha maslahi ya chama yanalindwa.
  10. K wamba, baada ya kupewa siri ya kuanzishwa kundi hilo la vijana wa usalama, tukapewa tahadhari na viongozi wetu wa mafunzo vilevile na viongozi wa chama na Serikali kwamba tunatakiwa kutunza siri ya mambo yote na atakaye thubutu kutoa siri kwa mtu asiye husika basi rntoaji siri atauawa kwa njia yoyote au kukatwa viungo.
  11. Kwamba katika wakati wote huu niliwahi kushiriki katika oparesheni mbalimbali na sehemu mbalimbali na kwa nyakati tofauti ikiwemo katika uchaguzi wa Tunduru, Tarime, Busanda na Igunga.
  12. K wamba baada ya kufahamu malengo ya kikosi hiki cha usalama wa C.C.M kwamba yamejikita katika kudidimiza demokrasia thabiti na kwamba inalenga kuwaathiri wananchi kwa kung'ang'nia madaraka na kuendesha shughuli za kijasusi dhidi ya vyama vingine vya siasa ndipo niliamua kujiondoa ndani ya chama cha Mapinduzi.
  13. Kwamba, kwa kuwa nilikabidhiwa silaha tajwa kwa ajili ya kutekeleza maslahi ya chama na kwa mujibu wa utaratibu wa chama, nimeona ni vema niirudishe kwa kuikabidhi kwa mlinzi wa amani ili ikabidhiwe kwa Chama cha Mapinduzi.
  14. Zaidi katika siku za hivi karibuni mara baada ya kutoka Igunga, na wakati nikijiandaa na kutafuta namna nzuri za kuirudisha silaha niliyopewa na uongozi wa C.C.M maisha yangu yamekuwa mashakani kwani mara kwa mara nimekuwa nikifuatiliwa nyumbani kwangu na hata sehemu mbalimbali ninazopita na watu nisiowafahamu vema.
  15. Kwamba, nimekuwa naishi bila amani na kwamba maisha yangu yako hatarini na hii yawezekana ni kutokana na silaha hiyo ya C.C.M waliyonikabidhi wenyewe kutekeleza matakwa yao.
  16. Kwamba nilichelewa kuikabidhi kutokana na kushikiliwa kizuizini Igunga kwa muda mrefu mpaka nilipoachiwa huru mimi na wenzangu watatu mnamo tarehe 18.12.2011.
  17. K wamba nakiri na kuthibitisha kwamba kazi tulizokuwa tunatumwa kuzifanya na chama ni za hatari na zenye lengo la kuathiri ukuaji wa demokrasia, ni za kikandamizaj i na za kiharifu na ndio maana hata tulivyokabidhiwa si1aha ilikuwa ni kwa usiri mkubwa na kwa ma1engo maa1umu.
Kuwa yote niliyoyaeleza kuanzia aya ya 1-18 ni ya kweli, kweli tupu na kuwa ninayathbitisha yote kwa nia ya kweli kutokana na ufahamu wangu mwenyewe
================


Chanzo Jf http://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/474279-ushuhuda-namna-ccm-inavyofanya-ugaidi-nchini.html

3 comments:

  1. Anonymous8:27 PM

    dah hivi kwanini tusiombe umoja wa mataifa watusaidie mana mahakama zetu ni kesi ya ngedere kumpelekea nyani


    rizo de bazil

    ReplyDelete
  2. Anonymous10:01 PM

    jeshi la polis la sisiem haliwezi kutenda haki kwa vyama pinzan

    ReplyDelete
  3. Anonymous10:01 PM

    chama cha majangili

    ReplyDelete