Huu ni ukweli usio na nguo kutokana na tabia iliyojengeka na kuendelea kujengeka hata sasa kwa kusahau shida haraka, kudanganywa kwa vitu vidogo, hapa nikimaanisha kwamba unapewa starehe ya saa/siku moja tu halafu unateswa kwa miaka mitano, tunasahau matatizo yote na kumwona aliyetutesa kama hana hatia na chochote kinacho semwa juu yake ni propaganda-uongo na kumwonea.
Watanzania walio wengi tunapenda kulaumu, kutoa shutuma na kubeza harakati za vyama vya upinzani hapa nchini badala ya kujitoa kushauri na kupigania haki kwa nini kufanyike ili kusaidia kutukia kwa mambo tunayotaka.
Ukijaribu kufuatilia utagundua kwamba tulio wengi tumekuwa ni wa kwanza kuwalaumu wapinzani kana kwamba wao (Upinzani) ndio waliotutesa kwa miaka yote wakiwa madarakani na sasa ameingia msamaria mwema Chama Cha Mapinduzi (CCM) ili kukusaidia.
Wananchi tusibweteke na ukaribu tunaoonyeshwa sasa hivi na Chama Cha Mapinduzi (CCM) na badala yake tujiulize ni kwanini sasa na si hapo kabla?! Hii yote ni danganya toto kwasababu chaguzi zimekaribia na hayo mnayoyaona ni machozi ya mamba.
Tusijitie upofu kwenye matatizo yetu bali tujifunze kutokana na matatizo yaliyotupata
Baadhi yetu tukiacha tabia hizi tutafka tunapopataka.
Huu ni ushauri kutoka kwa mmoja kati ya wasomaji wa blog hii.
No comments:
Post a Comment