Advertise with Us

Advertise with Us

DHall

DHall

Pages

January 5, 2014

CHADEMA yawavua uanachama Dr. Kitila Mkumbo na Samson Mwigamba!

Dr. Kitila Mkumbo


Samson Mwigamba

Habari kutoka katika chanzo chetu kilichobahatika kupenya na kuingia katika Kikao cha Kamati kuu ya CHADEMA leo tarehe 04.01.2014 saa2:00 usiku zinaripoti kwanba kutokana na kuzijadili kwa kina tuhuma kadhaa zinazowakabili wahusika hatimaye kamati hiyo imefikia hitimisho na kuwavua uanachama Dr. Kitila Mkumbo na Samson Mwigamba, hivyo kuanzia sasa Dr. Kitila Mkumbo na Samson Mwigamba sio wanachama wa CHADEMA!

Update ya Press Conference ya leo alasiri tarehe 05.01.2014 kutoka CHADEMA-Makao Makuu

M/Kiti wa Chama Taifa ndio ameingia maeneo haya ya Ofisini akitokea Viwanja vya Karimjee muda wowote kuanzia hivi sasa Mkutano huu na Waandishi wa Habari utaanza rasmi ndugu Wananchi.

Viongozi Wakuu akiwemo Katibu Mkuu, Mwanasheria Mkuu wa Chama, Mkurugenzi wa Mawasiliano, Wajumbe wa Kamati Kuu na Viongozi wameshawasili hapa na sasa Mh. John Mnyika ndio anawakaribisha Waandishi wa Habari na Kutoa salamu za utangulizi

Mnyika anaanza kwa kuomba radhi kwa press kuchelewa anasema ni kwasababu ya uzito wa hoja zenyewe kwasababu Kamati Kuu iliiagiza Sekretarieti kuandaa tamko la leo. Pia Mnyika amewatambulisha Viongozi wa Kanda waliopo mahali. M/Kiti hayupo hapa mbele na badala yake Katibu Mkuu Dr. Wilbrod Slaa ndie anazungumza na Waandishi wa Habari na tayari ameshaanza kuzungumza.


Katibu Mkuu anasema Watuhumiwa wawili yaani Dr. Kitila Mkumbo na Samsoni Mwigamba waliitikia wito wa Kamati Kuu lakini aliyehojiwa na Kamati Kuu ni Dr. Kitila Mkumbo pekee ambaye katika utetezi wao walikana kuvunja katiba ya Chama na Kanuni zake.

Katibu Mkuu anasema Dr Kitila Mkumbo alikiri kumfahamu M2 na anamjua fika lakini hawezi kumtaja mpaka awasiliane nae kwanza. Pia Dr Kitila Mkumbo alisema yeye na Mwandishi wa waraka ule walimpa briefing Mh. Zitto Kabwe kwa hiyo alikuwa anaufahamu waraka huo.


Kuhusu madai ya Mwigamba juu ya kipengele cha Katiba Dr Slaa anaonyesha baraua ya tarehe 13 July 2006 iliyosainiwa na Ndugu Shaibu Akwilombe aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wakati huo kwenda kwa Viongozi wa Mikoa nchi nzima ambayo ilionyesha mabadiliko ya kipengele hicho pamoja na kipengele kilichomruhusu M/Kiti kuteua Manaibu Katibu Wakuu na Katibu Mkuu ambacho kwa makusudi hawakilalamikii kwasababu kilimnufaisha Zitto Kabwe.

Dr. Slaa anamkaribisha Mh. Tundu Lissu ili kuongezea taarifa. Lissu anasema kuwa mkakati wa kuwachafua viongozi ni wa siku nyingi ambapo Chama kimefanikiwa kunasa mawasiliano ya Zitto tangu mwaka 2009 alipokuwa akiwasiliana akina Denis Msack wa Mwananchi. Lissu anasema njama hizi ndio zilizopelekea mpaka mashtaka ya ugaidi ambapo katika mahojiano yake ya Star Tv akiwa na akina Mwigulu Nchemba zitto hakukanusha, pia aliandika kwenye mitandao kuwa Chadema imtose Wilfred Lwakatare.

Lissu anaongeza kuwa Zitto mpaka sasa ana magari mawili ya Nimrod Mkono na Mkono mwenyewe ndie amewaambia taarifa hizo. Mkono amewaambia kuwa amempa Zitto hela nyingi sana na Zitto alishiriki moja kwa moja kumzuia mgombea wa Chadema katika Jimbo la Nimrod Mkono wakati Nimrod Mkono alikuwa ni namba sita katika orodha ya Mafisadi iliyotajwa pale Mwembeyanga.


Dr. Slaa anasoma mawasiliano kati ya Zitto na Mtu anayejiita Chadema Mpya. ambapo anasisitiza kuwa Mkakati ulianza kutekelezwa mapema kwa hiyo hoja kuwa Zitto alikuwa hajui Mkakati ni ya Uongo.

Mnyika anamalizia kwa kusema kuwa tuko katika vita dhidi ya maadui wa Chama walioko nje na ndani ya Chama. Hivyo falsafa yetu ya Nguvu ya Umma ndio itakayotusaidia kwa hiyo anatoa wito kwa Wanachama nchi nzima kuitumia falsafa hiyo katika hatua zote ili kushinda vita hii.

Pia anawaomba Wanachama wote kujitokeza kwa wingi mahakamani siku ya kesho katika kusikiliza maamuzi ya Mahakama. 


Mwisho wa Press Conference 

No comments:

Post a Comment