Advertise with Us

Advertise with Us

DHall

DHall

Pages

November 23, 2012

-§-Mkuu wa majeshi nchini Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo asimamishwa kazi!

 Generali Gabriel Amisi

Mkuu wa majeshi nchini Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo, amesimamishwa kazi huku uchunguzi ukiendelea kufuatia madai kuwa aliwauzia silaha makundi ya waasi yanaopambana na serikali ya nchi hiyo.
Ripoti moja ya Umoja wa Mataifa, imemtuhumu, Generali Gabriel Amisi kwa kuendesha mtandao wa kusambaza silaha kwa wawindaji haramu na makundi ya waasi, likiwemo kundi la Mai Mai Raia Mutomboki.
Msemaji wa serikali ya nchi hiyo amesema, maafisa kadhaa wa jeshi pia wanachunguzwa.
Serikali ya Rais Kabila imemfuta kazi mkuu huyo wa majeshi, siku chache baada ya waasi wa M23 kuuteka mji wa Goma Mashariki mwa nchi hiyo.
Waasi hao pia wameuteka mji wa Sake, lakini msemaji wa serikali ya Congo Lambert Mende amesema wanajeshi wa serikali wamefanikiwa kuumboa tena mji huo mdogo.
Ikiwa rais Joseph Kabila hatakubali kuanzisha mazungumzo ya amani waasi hao ambao inaaminika kwamba wanaungwa mkono na Serikali za Rwanda na Uganda, wametishia kuendeleza mapigano hayo mpaka mji mkuu wa Kinshasa.

No comments:

Post a Comment