Advertise with Us

Advertise with Us

DHall

DHall

Pages

October 27, 2013

INASIKITISHA: Julius Nyaisanga alisalitiwa na wenzake!

Marehemu Julius Nyaisanga

Sio vyema kukumbushia habari zao waliolala mauti. Waacheni wafu wazike wafu wao, ndivyo maandiko yanavyosema. Lakini katika hili la Nyaisanga tuna la kujifunza hasa kwa sisi wenye taaluma ya habari..

Taarifa zilizopatikana kutoka ndani ya familia zinadai kuwa wakati Nyaisanga alipokuwa mgonjwa, hakuna hata mwanahabari mmoja aliyekuwa akijali afy
a yake.

Alisumbuliwa na kisukari kwa zaidi ya miaka 20 lakini hakuna aliyejali. Si waajiri wake (ambao Nyaisanga aliwaingizia mamilioni ya fedha kwa umahiri wake wa kazi), si wanahabari wenzie, wala marafiki zake.

Licha ya kusumbuliwa na maradhi muda mrefu na licha ya wenzie kutoonesha support lakini, hakujali, aliendelea na kazi zake.

Wakati Radio One inaanzishwa alikubali kujitoa sadaka na kuacha kazi RTD ili kuhakikisha Radio One inaanzishwa na inasimama imara. Wakati ule na kina Charless Hilary, Mickdady Mahmood, Flora Nducha, Abdalah Majura na wengine.

Mtangazaji mararufu wa BBC, Aboubakar Liongo anadai ni Julius aliyemshawishi kuingia kwenye taaluma ya habari. Ni yeye aliyempeleka Radio One kufanya majaribio yake ya kwanza kama Radio Presenter. Hata baba yake Liongo alipoonesha wasiwasi Nyaisanga ndiye aliyemtoa wasiwasi huo kwa kumhakikishia usalama wa mwanae.

Hata baadae iliporipotiwa amesimamishwa kazi Radio One licha ya kuitumikia kwa takribani miaka 15, hakukata tamaa, aliendelea kupambana. Hatimaye akapata ajira Abood Media Morogoro.

Alipokuwa Morogoro bado aliendelea kusumbuliwa sana na kisukari na pressure. Aliugua, alizidiwa, akalazwa, lakini hakuna aliyekuwa karibu yake zaidi ya familia yake. Si watangazaji wenzie maarufu aliokuwa nao enzi hizo, au waajiri wake aliowatumikia kwa uaminifu.

Hata aliporipotiwa kuzidiwa na kwamba hali yake ilikuwa "serious" hakuna aliyejali. Alihangaika na mkewe na wanae huku akipewa support "kidogo" na Mzee Abood.

Licha kuzidiwa na maradhi lakini alilazwa "zahanati" ya Mazimbu, inayodaiwa kuwa Hospitali. Na bila shaka kutokana na kutopata huduma alizostahili kwa maradhi yake akafariki dunia.

Lakini mi nadhani Nyaisanga alihitaji matibabu bora zaidi ya yale ya Mazimbu. Alihitaji hospitali kubwa zaidi ya ile dispensary inayodaiwa kuwa hospitali pale Mazimbu. Pengine asingefariki ikiwa angepata huduma "standard" kidogo kwenye hospitali ya kueleweka.

Haikuwa lazima apelekwe Muhimbimbi kwenye VIP wodi, kama aliyopo Ufoo Saro. Nyaisanga hakuhitaji wodi yenye TV set, flat screen kama aliyopo Ufoo.. Alihitaji wodi ya kawaida yenye madaktari wataalamu ambao wangeweza kutatua shida yake.

Lakini ndio hivyo uwezo wake haukuruhusu kufika huko. Akaishia Mazimbu. Akaugua, akateseka, akalazwa. Peke yake. Hata wandishi wenzake hawakuandika habari za mwenzao kuugua.

However hata hawakumtembelea japo tu kumjulia hali hata kama walikuwa hawataki kuandika. Nani angemtembelea na wote walikuwa busy na risasi za Ufoo Saro..???

Aliugua, akateseka, akapita katika bonde la uvuli wa mauti. Licha ya kuwa alikuwa peke yake lakini hakuogopa, maaana "gongo na filmbo" yake BWANA vilimfariji.

Hatimaye akafariki usiku wa kuamkia October 20. Na hapo hasa ndipo ulipoonekana USALITI na Unafiki. Kila mtu alijifanya kumfahamu. Kila mtu alijifanya rafiki yake. Hata wale rafiki zake ambao pengine tangu waachane Radio One hawakuwahi hata kumpigia simu wakajifanya kuomboleza.

Viongozi wa serikali nao kama kawaida yao wakajitokeza na kudai wamepokea KWA MSHTUKO MKUBWA kifo cha Nyaisanga. Salamu za rambirambi zikatolewa kuanzia kwa Mh.Rais Kikwete hadi kwa MaDJs wa Radio Mbao. Wakapiga na nyimbo za kumuenzi mwenzao..

Lahaulah..!! Walikuwa wapi siku zote? Heshima zote hizi kwanini hawakumpa Nyaisanga angali hai, hadi wasubiri kuja kuipa maiti heshima?? Au ndo wanafikisha ujumbe kuwa WANAOKUDHARAU SIKU MOJA WATAKUSALIMIA KWA HESHIMA??

Lakini yote tisa, kumi ni vioja vilivyofanywa na waandishi wenzie. Aliokuwa nao RTD, wengine akaenda nao Radio One, wengine BBC, DW, Sauti ya Amerika etc. Watangazaji maarufu, wenye majina makubwa...wengine huwezi kuwaita majina yao kabla hujatanguliza neno "papaa" kwa sababu wana vitambi vikubwa, cha Idd Amin hakioni ndani..!! Wamekuwa mastar wa mjini..!!

Watangazaji hawa mapedeshee, ambao wengi walidai ni marafiki zake waliingia na mbwembwe Morogoro. Wakabadilisha kila kitu walichokikuta. Wakabadili ratiba ya mazishi na kuweka yao. Wakafuta kamati ya mazishi waliyoikuta Moro na kuunda yao..

Harakaharaka wakaweka na ratiba ya mwili wa Nyaisanga kuagwa Dar, tofauti na kamati ya Morogoro ambayo ilidhani kumuaga Morogoro peke yake ingetosha.

Mapedeshee wakasema lazima mwili wa Nyaisanga uletwe Dar. Watawezaje kuonesha mbwembwe zao mwili ukiagwa Moro?? Magari yao ya Vorgue, Discovery, Lexus hayawezi kwenda Moro. Suti zao kali za Dubai na Hong Kong haziwezi kuchafuka vumbi hadi Moro. Nyaisanga aletwe Dar.!

Waliposhauriwa kuwa mwili wa Nyaisanga ukitolewa Moro, upelekwe Dar kisha upelekwe Musoma kwa kupitia Morogoro utaharibika, hivyo ni bora waage kwa pamoja Moro kisha wapeleke mwili Musoma kwa maziko.. Haraka wakajibu "kama hofu ni mwili kuharibika tutakodi ndege, (Private Jet) itakayopeleka mwili hadi Musoma"

Kwa kauli hiyo Mjane wa marehemu hakuwa na pingamizi. Mapedeshee nao kufika Dar wakatangaza kwa haraka kuwa mwili wa Nyaisanga utaagwa Leaders kisha utasafirishwa kwenda Musoma kwa ndege. Kwa waliomfahamu Nyaisanga na alivyoteseka atleast hii ikawapa faraja kidogo.!

Lakini hawakutimiza ahadi hiyo ya kumpeleka kwa ndege zaidi ya kutafuta umaarufu tu pale Leaders. Baada ya kuaga, kila mmoja akadisappear na kuachia familia mzigo wa kusafisha maiti kwa gari hadi Musoma. What a shame..!! Kumbe wakati wanajinadi kupeleka mwili kwa ndege akili zao zilikuwa Mabwepande au??.

Kwa nini basi, waliamua kuuleta mwili Dar? Je, kulikuwa na shinikizo la nani? Au walikuwa wanatafuta umaarufu? Hii ni dharau..

Nani aliwalazimisha waandishi kuleta maiti Dar na kuja kuitelekeza Leaders?? Kama walishindwa kumheshimu Nyaisanga akiwa hai, kwanini hawakuheshimu hata maiti yake?? Enyi Waaandishi na Watangazaji wa Tanzania, nani aliyewaloga??

Pili, kamati hii ya watangazaji na wandishi iliyoleta msiba Dar waliidharau kamati ya mazishi ya Morogoro kwa kubadilisha jeneza na kumweka katika jeneza lingine. Kamati iliyokuwa inaratibu mazishi Morogoro ilimuweka kwenye jeneza alilokuja nalo hadi hospitali ya Muhimbili.

Lakini Kamati ya "Waandishi" wakaenda na jeneza jingine Muhimbili na kumbadilisha Nyaisanga. Mwanakamati mmoja alipohojiwa kuhusu kukataa jeneza la Morogoro alijibu hivi “Lile lililotoka na mwili Morogoro lilionekana kukosa ubora halafu lilitengenezwa ‘chapchap’ ndiyo ikaamriwa linunuliwe jingine zuri zaidi.” (Risasi, 26,October 2013).

Kwa upande wangu this is illogical statement ever made. Ubora uliokuwa unazungumzwa ni nupi? Jeneza lisilo bora lingewezaje kumleta kutoka Morogoro hadi Dar.?? kama ubora walimaanisha nakshi na marembo, ya kazi gani hayo?? Kwanini hizo hela zisingesaidia mjane na watoto walioachwa badala ya kutafuta sifa za kijinga??

Jeneza la gharama ili iweje? Ili tuone kuwa Nyaisanga alikuwa na maisha ya kifahari kumbe sivyo??

Prof.Lipumba aliwahi kusema Watanzania hatuwezi kuendelea kiuchumi kwa sababu tumeendekeza maisha ya bandia. Hatutaki kuishi maisha yetu halisi.. Hatutaki kujikubali.

Mtu anasoma BAED lakini ukimuuliza atakuambia LLB. Hajikubali, atafanikiwaje?? Mtu analipwa Laki 5 kwa mwezi lakini anataka kudrive after two months. Hajikubali.. hataki kukubali kuwa hali yake ni duni na anatakiwa kustrive ili kufanikiwa.

Sasa Nyaisanga amekufa bila msaada wa maana kutoka kwa waandishi wenzie, leo mnamnunulia jeneza la Milioni na ushee, upuuzi..!!

Lakini kama kweli kamati hii ya waandishi walikuwa na uchungu na Julius na hawakutaka awekwe kwenye jeneza cheap, kwanini hawakuungana na kamati ya mazishi ya Morogoro na kuangalia upungufu uliopo na kuurekebisha. Bila shaka wangeweza kuwashauri wenzao wa Morogoro aina ya jeneza la kununua ili wasipoteze hela mara mbilimbili.

Lakini maziko ya Wakristo hufanywa na jeneza moja tu. Jeneza linalotumika kubebea mwili wa marehemu ndilo hilohilo huingizwa kaburini na marehemu akiwemo ndani, tofauti na Waislamu ambao jeneza hurudi msikitini.

Sasa jeneza la Nyaisanga lililokataliwa na Kamati ya Dar litaenda wapi? Mwanakamati mmoja alipoulizwa alijibu kwa kujiamini "Lile tuliliacha Muhimbili ,ndugu watajua cha kufanyia" (Risasi 26, October 2013).

Kwangu mimi hii ni kauli ya dharau. Ndugu watajua cha kufanyia?? What does it mean? Kwamba ndugu walipeleke jeneza nyumbani kujiandaa na msiba mwingine au?

Mi nadhani kamati iliyoundwa Moro ingeachwa ifanye kazi yake bila kuingiliwa kila kitu kingekamilika. Hii kamati iliyoundwa Dar ilikuwa ya kisiasa au kutaka umaarufu. kila mtu anajidai kuwa ndugu, rafiki na wa kumuonea huruma. Mlikuwa wapi Nyaisanga alipokuwa mgonjwa?

Lakini hii si mara ya kwanza mambo haya kutokea kwenye tasnia ya habari nchini. Wapo waandishi wameugua muda mrefu, wameteseka na wengine wamekufa vifo vya mateso, lakini ni nadra kusikia wandishi wenzake wakiripoti habari hizo.

Adam Mwaibabile alifungwa bila hatia, hakuna mwandishi aliyekuwa na habari nae. Hata aliposhinda kesi baada ya kukaa gerezani mwaka mmoja, waandishi wenzie hawakuona ile ni story. Walikuwa busy na story za wanasiasa maana ndio zinamake "headlines"

Hata Mwaibabile alipotoka gerezani na kuandika kitabu chake kuelezea aliyokutana nayo huko jela na namna alivyofungwa kwa uionevu wa RC wa Lindi, hakuna Mwandishi aliyempa suport hata ya kukipa promo kitabu chake.

Hakuna hata gazeti lililodiriki kumpa free space atangaze kitabu chake. Alikuwa akihangaika mwenyewe kama tiara kutafuta market ya kitabu chake.

Hakuna mwandishi aliyemfanyia interview.. Hakuna mwandishi aliyekuwa na muda nae..

Kwani yeye amepigwa risasi na jamaa kutoka Sudan?? kwani yeye amemwagiwa tindikali? Kwani yeye alinyofolewa jicho na kupelekwa S.Africa??

However hata wangedeal nae Mwaibabile hakuwa na 10% ya kuwapa kama waliyozoea kupewa na Wanasiasa kwenye bahasha za khaki..

Wenyewe wanasema si rushwa, bali ni posho tu inaitwa "brown envelop" Huwa wanapewa wakiripoti habari za Vyama vimegoma kukaguliwa fedha za ruzuku, au wakiripoti Mabilioni yaliyofichwa Uswisi..!

Hata hivyo licha ya kuteseka kote huko Mwaibabile akaja kufariki kifo chenye utata na ilidaiwa ameuawa lakini kwa waandishi wenzie ile haikuwa habari kubwa kama ya kukamatwa kwa "Masamaki ya Magufuli"

Waandishi hawakuthamini maisha ya mwenzao kisa Vibua na Pereje za Magufuli ndio ilikuwa "habari ya mjini".

Hadi leo hakuna mwandishi aliyewahi kudevelop story au makala kujaribu kureflect maisha ya Mwaibabile na kifo chake cha utata...

MY TAKE..!!
Waandishi hatuthaminiani.. Hatujaliani.. Hatupendani.. Tumebaki kuchumia matumbo na kutafuta umaarufu wa kijinga mjini. Tupo busy kuripoti habari za wanasiasa na kupiga ramli za kutabiri wagombea urais 2015.

Ifike mahali tujijali na kujipenda. Tujithamini..Tuache uzandiki huu wa kuithamani maiti na kutomjali mtu wakati akiwa anaumwa.

Tusipojijali sisi hata hao wanasiasa tunaowatetemekea hawawezi kututhamini. wataendelea tu kututumia kama "BIG G" ambayo utamu ukiisha hutupwa, hata aliyekuwa anaitafuna asijue alipoitupa.

MSIBA HUU WA NYAISANGA UWE FUNDISHO KWA WANAHABARI WOTE WA TANZANIA.. (mimi nikiwemo). Tutengeneze image itakayotufanya tukumbukwe hata tutakapoondoka hapa duniani.

Mwanaharakati Che Guevara aliwahi kusema "Im not afraid of death. Because i know when my Heart will beat no more, I wont die. I will continue living in the heart of other people for the Principles, Rules and Beliefs that I lived for..."


No comments:

Post a Comment