1. MV. BUKOBA 21/05/1996
Mv. Bukoba ambayo ilizama mnamo mwaka 1996 katika ziwa victoria na kuua watu zaidi ya 1000.
MV Spice Islander iliyozama katika bahari ya hindi huko Nungwi wakati ikiwa njiani kutokea Dar es Salaam kuelekea Pemba mnamo mwaka jana 2011 na kuua watu zaidi ya 250.
3. MV. SEAGULL 18/07/2012
Mv. SeaGull ambayo imezama leo mchana katika bahari ya hindi na kuua watu zaidi ya 200.
ILIANZA
AJALI YA MELI YA MV. BUKOBA, IKAFUATIA MELI YA MV. SPICE ISLANDER, LEO
MELI YA MV. SEAGULL. HIZI NI BAADHI YA AJALI ZILIZOWEZA KUBAHATIKA
KUSIKIKA NA KUTANGAZWA NA VYOMBO VYA HABARI!
USHAURI WA BURE: Ni wazi kwamba kuna haja na umuhimu mkubwa sana kwa Serikali kutupia jicho na kuwekeza katika sekta hii ya majini haswa kwa upande wa vyombo vya kisasa vya mawasiliano na vile vya uokoaji kwani ajali zimekuwa ni nyingi na zenye kuhitaji vyombo vya kisasa vya uokoaji ukilinganisha na vyombo duni vinavyotumiwa na Jeshi la uokoaji wa majini.
No comments:
Post a Comment