Tetesi zilizoifikia Maisha Times zinaripoti kwamba kutokana na hali mbaya ya kisiasa inayokikabili Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa kile kinachoonekana kuwa ni ukinzani mkubwa kutoka kwa chama kikuu cha upinzani (CHADEMA) imekilazimu chama hicho tawala kutafuta njia mbadala ya kurudisha imani na hata umaarufu wake kwa wananchi na kujidhatiti kungali mapema katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 hiyo ikiwa ni pamoja na kuandaa mipango ya kuja kivingine kabisa kwa kumpitisha mgombea mwananke (Asha Rose Migiro) ambaye labda kwa mitazamo ya chama hicho anaweza kuwa ni kivutio kikubwa kwa wananchi walio wengi haswa kina mama kuweza kumchagua na kunusuru kushindwa vibaya kwa chama hicho katika uchaguzi wa mwaka 2015.
Habari zaidi zinaripoti kwamba katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN), Ban Ki Moon, amemteua Naibu Katibu Mkuu anayemaliza muda wake, Dk. Asha-Rose Migiro, kuwa mjumbe wake maalumu katika masuala ya Ukimwi na ugonjwa wa Ukimwi barani Afrika.
Ban Ki Moon ametangaza uteuzi huo wakati wa hafla maalumu aliyoiandaa, kwa ajili ya kumuaga anayehitimisha utumishi wake wa miaka mitano na nusu katika nafasi ya Naibu Katibu Mkuu.
No comments:
Post a Comment