Advertise with Us

Advertise with Us

DHall

DHall

Pages

July 1, 2012

-§- Usaili-Interview zote nchini zifanyike kwa lugha ya Kiswahili!

Kama hali ni hii, Je ipi maana ya Kiswahili ni Lugha ya Taifa-Tanzania??

 -§- Ushauri wangu wa bure kwa serikali ya jamuhuri ya Muungano wa Tanzania ni huu: 
Usaili [Interview] zote nchini Tanzania zifanyike kwa lugha ya Kiswahili ili kutoa fursa zaidi kwa watanzania wengi ambao wanaimudu vyema lugha husika, kwani katika uhalisia usio na nguo kuongea lugha ya Kingereza pekee haimaanishi kwamba mtu ni msomi au mtaalamu katika kile alichonacho bali vitendo ndivyo vinavyoweza kuthibitisha uelewa na hata utendaji wake.

Itambulike kwamba hili ni tatizo kubwa linalochangia kwa kiasi kikubwa kuwanyima fursa mbalimbali Watanzania haswa ile ya ajira na bishara. Kingereza kinatoa fursa zaidi kwa wageni na sio Watanzania.
MFANO HAI. Hauhitaji kutumia nguvu nyingi wala gharama kubwa kufanya tafiti juu ya kile ninachokizungumzia bali ukitaka kuthibitisha kile ninachokizungumzia [Ukiwa ndani ya Tanzania] basi fanya utafiti huu mdogo sana kwa kuandaa mada yako kwa lugha ya Kingereza uitafsiri kwa lugha ya Kiswahili au mada yako ya Kiswahili uitafsifi kwa lugha ya Kingereza halafu chukua mada zote mbili uziandike katika mtandao wa kijamii mf. Facebook au Tweeter halafu chukua muda kidogo kufuzifuatilia mada zako, hakika utaona kati ya mada zote mbili [Ile ya Kingereza na ile ya Kiswahi] ile ya Kiswahili itapata wachangiaji wengi zaidi kuliko ile ya Kingereza [English] na hapo ndipo utakapoweza.

Kwa kiasi kikubwa Tanzania inajengwa na kuunganishwa na lugha ya Kiswahili na sio Kingereza.
Umuhimu wa lugha ya Kiswahili kutumika katika Jumuiya ya Afrika mashariki Binafsi siungi mkono ushirikiano kati ya nchi tano za Afrika ya mashariki kutokana na ukweli kwamba nchi husika bado hazijaweza kujisimamia zenyewe, na kinachofanyika ni kwa baadhi ya nchi hizo kugundua manufaa zitakayoyapata kutokana na kuungana nchi ambazo bado ziko usingizini mf. Tanzania kutambua kama jumuiya hiyo itazisaidia kuweza kunufaika au la. 
Vyovyote itakavyokuwa kama jumuiya hiyo itafanikiwa kuendelea lakini angalizo langu ni kwamba: Iwapo Serikali ya Tanzania isipokuwa makini kusimama kidete katika makubaliano ya sera ya matumizi ya lugha ya kiswahili katika Jumuiya ya Afrika ya Mashariki basi watanzania tusitarajie kunufaika kwa lolote lile kutokana na muungano wa nchi husika kwani ukijaribu kuangalia hata sasa katika makampuni na hata mashirika mbalimbali haswa yale ya binafsi na ya Kimataifa waajiriwa walio wengi ni majirani zetu wa nchi za jirani kama Kenya na Uganda, pia Africa Kusini kwa kutambua uhalisia na kutumia falsafa ya "Speak English and get a job in Tanzania" "Ongea Kingereza upate kazi Tanzania" falsafa ambayo ukiichunguza kwa undani ni kweli inawanufaisha zaidi raia wengi wa kigeni kuliko watanzania ambao wengi wetu hawaijui wala kuitumia kabisa lugha ya Kingereza.
Jumuiya ya Afrika ya Mashariki [East African Community - EAC] ni ushirikiano kati ya nchi tano za Afrika ya Mashariki, hususan Kenya, Uganda, Tanzania, Burundi na Rwanda.
Rais Jakaya Kikwete na viongozi wenzake wa Jumuiya ya Afrika Mashariki 


 Ushauri huu umetolewa Na. Ndg. Salvatory Mkami

 
 

No comments:

Post a Comment