Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Dk. Wilbrod Slaa amewahakikishia Wananchi wa jimbo la Arumeru
kwamba hakuna kura yoyote itakayoibiwa katika uchaguzi mdogo wa Ubunge utakaofanyika jimboni hapo kwani Chama Cha Demokrasia na Maendeleo [CHADEMA] kimejipanga vyema kudhibiti wizi
wa aina yoyote ile utakaofanyika katika uchaguzi huo. Dk.Slaa aliongeza na kusema kwamba wamefanikiwa kudhibiti ongezeko la Vituo
50 ambavyo Chama Cha Mapinduzi [CCM] wakishirikiana na Tume ya Uchaguzi walikuwa kwenye mchakato wa kuviongeza ili kukipa Chama Cha Mapinduzi [CCM] ushindi.
Kwa habari zaidi fuatilia kwa makini hotuba ya Dr. Slaa hapo juu.
No comments:
Post a Comment