Waziri wa Uchukuzi, Dk. Harrison Mwakyembe.
Dar es salaam, Tanzania
Waziri
wa Uchukuzi, Dk Harrison Mwakyembe amemsimamisha kazi Mkurugenzi Mkuu
wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA), Ephraim Mgawe na viongozi
wengine watatu kupisha uchunguzi wa tuhuma mbalimbali bandarini hapo.
Wengine waliosimamishwa kazi ni Wasaidizi wake wawili pamoja na Meneja wa Bandari ya Dar es Salaam.
Waziri
Mwakyembe alitoa kauli hiyo leo jijini Dar es Salaam alipozungumza na
waandishi wa habari baada ya juzi kuwa na kikao cha dharura na viongozi
wa mamlaka hiyo.
Alisema
kutokana na upungufu waliobaini wameona ni vema viongozi hao wakakaa
pembeni na kwamba ameunda kamati ya watu saba watakaochunguza masuala
hayo.
Hatua
hiyo ya kusimamishwa kazi kwa viongozi hao ni mwendelezo wa mikakati ya
waziri huyo kusafisha uozo katika taasisi mbalimbali kwani hivi karibuni
kumsimamisha kazi Kaimu Mkurugenzi wa Shirika la Ndege Tanzania
(ATCL), Paul Chizi na wakurugenzi wanne kutokana na ukiukwaji wa
sheria, kanuni na taratibu za utumishi wa umma, ambao umetishia uhai wa
shirika hilo.
Akizungumza
jana, Mwakyembe alisema nafasi ya Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TPA
inashikiliwa na Mhandisi Madeni Kipande kutoka Wizara ya Ujenzi na kwa
nafasi nyingine akasema wawekwe watu wenye uadilifu.
“Nimeamua
kumchukua mtu nje ya bandari kukaini nafasi ya Mkurugenzi Mkuu ili
kuondoa wasiwasi, maana angetoka ndani angeshindwa hata kuingia ofisi.
“Najua uamuzi huu utahojiwa, lakini tuendelee kuzumiliana, kwani ukweli haupingwi,” alieleza.
Pamoja na hatua hiyo, alisema ameunda kamati ya watu saba kuchunguza tuhuma mbalimbali bandarini hapo.
“Wajumbe
wa kamati hiyo sitawataja majina, kwa sababu tuna deal na watu wenye
hela…hadidu rejea itakiwa na maswali 50,” alisema.
Mbali na kuwasimamisha kazi watumishi hao, pia alisema ameiagiza bodi ya mamlaka hiyo kuwasimaisha kazi watumishi wa kituo cha kupokea mafuta cha Kurasini (KOJ) ambao ni Meneja, Meneja wa Jet na Injinia wa mafuta wa kituo hicho.
Aidha,
aliitaka kampuni ya Singirimo iliyokuwa inaendelea na zabuni ya
kuchukua mafuta machafu, iache kufanya kazi hiyo mara moja, kwani
inachunguzwa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) na
Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (Ewura).
“Kwanza
muda wa kampuni hii kufanya kazi hiyo umekwisha, hivyo kampuni
nyingine iliyoshinda zabuni imepewe nafasi ifanye kazi hiyo. Singirimo
ikae pembeni kupisha uchunguzi.
Akizungumzia
wizi wa mafuta, alisema suala hilo limekuwa vita kubwa na kwamba
kampuni inayochukua mafuta hayo hudai ni machafu, lakini mwisho wa siku
wanayepeleka vituo vya mafuta.
“Pale
hayatoki mafuta machafu, yanapakwa rangi yaonekane machafu…. Zabuni ya
mafuta hayo inagombewa mno. Tumefuatilia tumegundua kuwa magari
yanayochukua mafuta hayo huishia Petrol Station,” alisema.
Pamoja
na hilo, alisema malori yanayochukua mafuta hayo hayafahamiki kiwango
kichochukua na kuongeza kuwa loro moja lililodai kubeba lita 9,000 za
mafuta, lilipopimwa na Kamishna wa Vipimo lilibainika kubeba lita
26,000.
Kuhusu
kukosekana na flow mitres ambazo zinapima kiwango cha mafuta,
Mwakyembe alisema ameuagiza uongozi wa mamlaka hiyo kuhakikisha ndani
ya mwezi mmoja zinapatikana.
“Nimeaagiza watumie single sorce katika kuangiza flow mitres, lakini pia wazingatie sheria ya manunuzi inasemaje,” alisema.
Pamoja
na hayo, ameagiza mamlaka hiyo kuacha malipo ya fedha taslimu
dirishani kuanzia Septemba mosi mwaka huu na kwamba watumie benki ama
njia njingine za kisasa.
No comments:
Post a Comment