Advertise with Us

Advertise with Us

DHall

DHall

Pages

September 6, 2012

-}i{- MAKANISA YACHOMWA MOTO BAGAMOYO!

 Moja ya mitaa mbalimbali katika wilaya ya Bagamoyo

Hofu kubwa imetanda katika wilaya ya Bagamoyo Mkoani Pwani baada ya makanisa mawili yaliyopo katika kijiji cha Matuli kata ya Bwilingu kuchomwa moto na watu wasiojulikana huku familia nyingine zikikimbia msituni kwa kuhofia kuchomewa ndani.

habari zaidi zinaeleza kwamba makanisa yaliyochomwa moto ni pamoja na lile la Free Pentekoste Church Tanzania [FPCT] na lile la Anglikana. Akizungumzia tukio hilo mchungaji wa Kanisa la Pentekoste alisema asubuhi ya Septemba6 akiwa katika shughuli zake za kawaida alikutana na mwenyekiti wa kijiji hicho, Shabaan minda na kumwelezea jinsi matukio hayo ya kuchomwa kwa makanisa hayo kilivyoleta hofu katika eneo hilo. Kwa upande wake mchungaji wa Kanisa la Anglikana Mchungaji Moses Lukanda alisema katika kanisa hilo kulikuwa na ujenzi uliokuwa unaendelea lakini walifika baadhi ya watu wakabomoa ukuta kisha kuchoma moto.

Kutokana na matukio hayo ikiwa ni baada ya kutoa taarifa na kuhojiwa katika kituo kikuu cha polisi Chalinze mchungaji Peter kazimoto na mwenzake Moses Lukanda wameiomba Serikali kutoa tamko kali kutokana na kitendo hicho ambacho kimeanza kuota mizizi katika mikoa kadhaa nchini.

Wakati hayo yakiendelea familia ya bwana Salehe Rais wa kitongoji cha Mnyembele katika kijiji cha Malivundo Kata ya bwilingu amelazimika kuikimbia nyumba yao na kulala porini wakihofia tishio la kuchomewa ndani ya nyumba wanayoishi. Akizungumza na chanzo chetu mtoto wa mzee rais aliyejitambulisha kwa jina la Lucian salehe alidai kwamba mnamo tarehe 05Septemba kulikuwa na vijana wanaoendesha pikipiki wa kituo cha Pera kwa Mwarabu Chalinze walifika katika nyumba yao na kuwaeleza kuwa usiku huo wasilale nyumbani kwani kuna hatari ya kuchomwa moto. Tunawashukuru vijana hao waendesha pikipiki kwa kututaarifu juu ya kuwepo kwa mpango huo kwani kama ungefanikiwa sijui kama mpaka sasa tungekuwa hapa", alidai Salehe. aliendelea na kusema kwamba baada ya taarifa hiyo yeye na familia yao walilazimika kwenda kulala kusikojulikana kwa kuhofia usalama wao.  

No comments:

Post a Comment