Advertise with Us

Advertise with Us

DHall

DHall

Pages

November 8, 2012

-§- Habari ya wawili waliokwamana huko Temeke ni "Uzushi"!

Eneo la nje ya Hospitali ya Temeke

Kuna taarifa za kuzushwa zilizotapakaa katika vyombo mbalimbali vya habari na mitandao ya kijamii zikiripoti kutoka katika Hospitali ya temeke kwamba kuna watu wengi waliofurika kwa kile kinachoaminika kwamba kuna mwanaume aliyekuwa na tabia ya kuiba mke wa mtu na baada ya mume wa mwanamke huyo kupata taarifa kuhusiana na tabia ya jamaa huyo kumwibia mke wake [Kuzini na mke wake kwa siri] ndipo jamaa huyo alipoamua kumwendea kwa mganga wa kienyeji na kumfunga mkewe-kumtegea mwizi wake dawa ambayo usiku wa kuamkia leo ilifanikiwa kupelekea wawili hao kukwamana sehemu zao za siri wakati wakiwa katika tendo la ndoa hatimaye kufikishwa katika Hospitali ya Temeke, hali ambayo ilipelekea kusambaa kwa haraka kwa "Uzushi" huo karibu kila kona ya jiji la Dar es salaam na kupelekea kufurika kwa wananchi wengi katika maeneo ya hosptali hiyo wakitaka kushuhudia na kupata ukweli juu ya tukio hilo.

UTHIBITISHO
 Akiongea kwa simu kaimu kamishna wa Polisi wa mkoa wa Temeke ameweza kuthibitisha na kusema kwamba habari hiyo sio ya kweli na imelenga kuwapotezea muda na kuwapa usumbufu Madaktari, Wauguzi, Wagonjwa na Wananchi kwa ujumla, hivyo amesisitiza na kuwataka Wananchi kupuuzia habari hiyo ambayo yeye ameiita ni uzushi huku akizidi kusema kwamba Jeshi la Polisi linaendelea kufuatilia ili kuweza kumnasa aliyesambaza Uzushi huo.

No comments:

Post a Comment