Natabiri "Civil War" kutokea Africa ndani ya miaka
michache ijayo na kuiathiri zaidi nchi ya Tanzania ambayo ndiyo haswa
inayogombewa na nchi tajiri kutokana na wingi wa rasilimali zake zenye utajiri
mkubwa ambao kiuhalisia Serikali yetu imejiaminisha kwa 100% kwamba haiwezi
kufaidi matunda ya rasilimali hizo hata kidogo pasipo wawekezaji ambao mara
nyingi na kwa kiasi kikubwa tumejikuta tukiwanufaisha wao zaidi kuliko hata
sisi wenyewe.
Kama ilivyokuwa enzi hizo wakoloni walipokuwa wanakuja
Afrika kwaajili ya kutafuta rasilimali mbalimbali ndivyo hali ilivyo hata sasa
na hakuna mabadiliko makubwa wala mbinu zenye utofauti kubwa wakoloni hao
wanazozitumia bali ni zilezile kwa kuamini kwamba pasipo akili-elimu yao
sambamba na vitendea kazi vyao kuendelea kwa nchi za kiafrika ni ndoto! jambo
ambalo kutokana na upofu na udhaifu wa Serikali za nchi mbalimbali barani
Afrika mf. Tanzania, Congo nk. limeonekana kuwa ni la kweli na hata kukubaliana
nalo na kupelekea Viongozi wa nchi zetu sio tu kutafutwa bali wao wenyewe na
heshima zao kuwatafuta na wenda kupiga goti kuwaomba Wakoloni hao walioficha
sura zao nyuma ya kivuli cha wawekezaji "Investors" kutoka nchi
tajiri kuja kujichukulia rasilimali zetu kwa bei sawa na bure huku sisi wenyewe
tukipata faida ndogo isiyoelezeka sawa na bure [Pitia mikataba mbalimbali ya
madini, Gesi, Mafuta-kati ya wawekezaji na Serikali ya Tanzania kama
utabahatika kuupata kwani Mikataba hiyo hufichwa na kufanywa "Siri"
kwasababu imejaa uozo mtupu].
Daima ili Nchi tajiri/Wawekezaji waweze kuiba Rasilimali
kutoka katika nchi yoyote ya Afrika njia pekee ni kuvifadhili baadhi ya vyama
vya Kisiasa au vikundi mbalimbali vya Kidini, Kikabila au Ukanda nk.
kuhakikisha kwamba vinaanzisha harakati mbalimbali ambazo malengo makubwa na
mwisho wake huwa ni vita jambo ambalo nchi tajiri kutumia nafasi hiyo ya
Migogoro, Vita nk. kupenya na kuchukua kile wanachokitaka mf. Madini, Gesi nk.
kadiri watakavyo kwa kuamini kwamba muda huo Serikali yaa nchi husika hatakuwa
makini bali itakuwa imeelekeza zaidi nguvu kubwa katika vita dhidi ya vikundi ambavyo
kinyume chake vinakuwa vimefadhiliwa na nchi hizo tajiri ili kuhakikisha kwamba
vita haikomi mpaka pindi malengo ya nchi hizo tajiri yanapokuwa yametimia.
[Congo ni moja ya nchi ambazo waasi wake wanafadhiliwa na nchi tajiri lakini
ukichunguza kiundani utagundua kwamba nchi tajiri inachokitaka ni madini ya
nchi hiyo na sio kitu kingine tofauti. Baada ya Congo hali hiyo [Vita] itafuata
kwa nchi ya Tanzania]
No comments:
Post a Comment