Mkurugenzi mtendaji wa Benki ya CRDB Dkt. Charles Kimei alipokuwa akielezea kwa ufupi Huduma itolewayo na Benki ya CRDB ijulikanayo kama "FahariHuduma"
Msanii
wa muziki wa kizazi kipya Mataluma akiwa na wacheza shoo wake wakitoa
burudani katika uzinduzi wa huduma za kibenki kupitia mawakala
(FahariHuduma) kutoka Benki ya CRDB.
Afisa wa Benki ya CRDB anayehusika na huduma
za uwakala wa Benki, Donat Mushi akielezea juu ya njia hiyo mpya ya
utoaji huduma kupitia kwa mawakala iliyoasisiwa nchini jana na Benki ya
CRDB.
Jana
Benki ya CRDB ilizindua kwa mara ya kwanza nchini njia mpya ya utoaji
huduma za kibenki kupitia mawakala iliyopewa jina la FahariHuduma ikiwa
na kauli mbiu ya Ulipo Tupo ambapo Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB
hiyo Dkt. Charles Kimei alielezea sababu kubwa ya kuanzishwa kwa njia hiyo ni kwa lengo la kuwafikia watanzania wengi zaidi ambao bado hawajafikiwa na huduma za
kibenki pamoja na kusogeza huduma karibu zaidi na wateja.
No comments:
Post a Comment